Je! Kuna dhambi kubwa na ndogo, na kama hakuna je! Mtu aliyeua na aliyetukana je watapata adhabu sawa?

Je! Kuna dhambi kubwa na ndogo, na kama hakuna je! Mtu aliyeua na aliyetukana je watapata adhabu sawa?

JIBU: Dhambi ni dhambi iwe kubwa au ndogo, zote ni kosa, biblia inasema.
 
Yakobo 2:10 “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
 
11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. “
 
Unaona hapo? Kwahiyo mtu akitenda dhambi iwe kubwa au ndogo ataadhibiwa. lakini adhabu zitatofautiana huko waendako, kwasababu Bwana Yesu pia alisema aliyeua kwa upanga atauawa kwa upanga, apandacho mtu ndicho atakachovuna. adhabu ya shetani haiwezi ikawa sawa na adhabu ya mwanadamu. Biblia inaeleza..
 
Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, ATAPIGWA SANA.
 
48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, ATAPIGWA KIDOGO. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi. “
 
Kwahiyo mapigo yanatofautiana kulingana na matendo ya mtu aliyoyatenda akiwa hapa duniani, ni kama tu vile thawabu zitavyotofautiana kwa mtu na mtu mbinguni kwa jinsi alivyotaabika katika kumtumikia Bwana vivyo hivyo na jehanamu adhabu zitatofautiana kulingana na dhambi mtu alizotenda akiwa ulimwenguni. Hivyo hatupaswi kuipima dhambi kwa namna yoyote, ni kukaa nayo mbali kwasababu iwe ni kubwa au ndogo mshahara wake ni MAUTI, Warumi 6:23.
 
Dhambi kubwa na ndoto zote zina adhabu ya mauti.
 
Mungu akubariki.


Mada zinazoendana:

DHAMBI ISIYO NA MSAMAHA.

DHAMBI ZINAZOTANGULIA NA ZINAZOFUATA.

DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI.

DHAMBI YA MAUTI


Rudi Nyumbani:Print this post

About the author

Admin administrator

Leave a Reply