Je wale waliomsulubisha Bwana, wataenda mbinguni, kwakuwa walisamehewa?

Je wale waliomsulubisha Bwana, wataenda mbinguni, kwakuwa walisamehewa?

Bwana Yesu alisema “Baba uwasamehe kwakuwa hawajui walitendalo (Luka 23:34)”. Je kwa kusema hivyo ina maana wote walisamehewa dhambi zao, kiasi cha kwamba hata wangekufa pale wangeenda mbinguni?.


Jibu: Dhambi waliyosamehewa ni hiyo ya kumsulibisha Bwana, na Bwana Yesu aliwasamehe kutoka moyoni, na hivyo Baba aliwasamehe pia.
Lakini kusamehewa kosa hilo, haimaanisha wamesamehewa na mengine yote..haimaanishi wamesamehewa uuaji waliofanya jana, au matusi waliyotukana juzi, au mauaji waliyoyatekeleza wiki iliyopita, au wizi walioufanya mwezi uliopita.

Hapana!..walichosamehewa ni hicho kimoja tu!..yaani kosa hilo la kumsulubisha Bwana Yesu!.

Ni sawa na wewe leo umsamehe mtu aliyekutapeli jana, na hivyo ukaghairi kumpeleka polisi, hiyo haimaanishi kasamehewa dhambi zake zote za utapeli alizowafanyia na wengine. Wewe umemsamehe kweli na Mungu pia kamsamehe.

Lakini hatia za makosa mengine aliyowafanyia wengine bado hajasamehewa mpaka atakapotubu.

Vile vile na waliomsulubisha Bwana walisamehewa tu dhambi hiyo moja ya kumsulubisha Bwana, nyingine zilizosalia walipaswa watubu.(Waungame dhambi zao zote, ndipo wawe salama).

Zaidi sana kama walikufa bila kumwamini Yesu, vile vile watahukumiwa kwa dhambi hiyo, hatakama walisamehewa ile kumsulubisha Bwana.

Yohana 3:18 “Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu”.

Hivyo kama Bwana Mungu alipanga kuwapiga kwa kosa la kumsulibisha Bwana, alighairi na kuyaondoa hayo madhara, lakini ghadhabu ya makosa mengine waliyoyafanya ilikuwa pale pale, na zaidi sana ghadhabu ya wao kutomwamini Bwana bado haikuondolewa. Hiyo inaondolewa kwa mtu kuyasalimisha maisha yek kwa Yesu.

Hiyo ikitufundisha kuwa tunapaswa tuungame dhambi zetu zote kwa Bwana.

1 Yohana 1:9 “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote”.
Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.

HUYU MELKIZEDEKI NI NANI?

YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.

Hema ya kukutania ni nini, na ilikuwaje?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
M
M
2 years ago

Ubarikiwe