Jina la Mwokozi wetu YESU KRISTO, libarikiwe, Karibu tujifunze Neno la MUNGU wetu lililo taa na Mwanga wa Njia zetu (Zab. 119:105)
Ipo Minara inayoinuliwa na ibilisi katika maisha ambayo inaweza kuangushwa/kuharibiwa kwa LUGHA na USEMI tu, maana yake pale lugha inapobadilika au usemi unapobadilika minara hiyo inakufa au kupotea.
Mfano wa minara hiyo ni ule wa Babeli..
Mwanzo 11:1 “Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. 2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko. 3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. 4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. 5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. 6 BWANA AKASEMA, TAZAMA, WATU HAWA NI TAIFA MOJA, NA LUGHA YAO NI MOJA; NA HAYA NDIYO WANAYOANZA KUYAFANYA, WALA SASA HAWATAZUILIWA NENO WANALOKUSUDIA KULIFANYA. 7 HAYA, NA TUSHUKE HUKO, TUWACHAFULIE USEMI WAO ILI WASISIKILIZANE MANENO WAO KWA WAO. 8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. 9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote”.
Mwanzo 11:1 “Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.
2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.
3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.
4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.
5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.
6 BWANA AKASEMA, TAZAMA, WATU HAWA NI TAIFA MOJA, NA LUGHA YAO NI MOJA; NA HAYA NDIYO WANAYOANZA KUYAFANYA, WALA SASA HAWATAZUILIWA NENO WANALOKUSUDIA KULIFANYA.
7 HAYA, NA TUSHUKE HUKO, TUWACHAFULIE USEMI WAO ILI WASISIKILIZANE MANENO WAO KWA WAO.
8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.
9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote”.
Umeona lugha jinsi ilivyo na nguvu?.. Ni hivo hivyo katika ulimwengu wa roho ipo minara ya dhambi, magonjwa, na matatizo ya kila aina, ambayo ili iweze kuharibika inahitajika badiliko la Lugha.
Kauli zinazotoka kinywani mwako zinaweza kuangusha minara ya maadui, hivyo ukiweza kubadilisha lugha yako na kuwa ya staha, heshima, na hekima isiyo ya kejeli, dharau au matukano utaweza kumpiga ibilisi pakubwa sana, na kuangusha minara yako yote ya fitna, shida, adha na aibu.
Lakini pia tunapokuwa katika maombi, kunena kwa lugha kuna maana sana kwa mwamini, kwani tunaponena kwa lugha ibilisi hajui ni nini tunaomba kwani muda huo Roho Mtakatifu ndiye anayetuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, hivyo adui hajui ni wapi mashambulizi yatamjia, na minara yake yote inaanguka.
Ndio maana ile siku ya Pentekoste Roho Mtakatifu aliwashukia mitume, na kuanza kunena kwa lugha mpya, adui alichanganyikiwa na kushindwa kujua ni nini kinaendelea, na pale pale Mitume walipata nafasi ya kuhubiri kwa ujasiri na watu elfu tatu wakaongezeka kwa Bwana na kubatizwa.
Matendo 2:41 “Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. 43 Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume”. Omba kubadilishwa lugha yako na usemi wako, omba kujazwa Ujazo wa Roho Mtakatifu unene kwa lugha (1Wakorintho 14:5), na minara yote ya adui itatoa moshi. Yoeli 2:28 “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; 29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu. 30 Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, NA MINARA YA MOSHI”.
Matendo 2:41 “Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.
42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
43 Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume”.
Omba kubadilishwa lugha yako na usemi wako, omba kujazwa Ujazo wa Roho Mtakatifu unene kwa lugha (1Wakorintho 14:5), na minara yote ya adui itatoa moshi.
Yoeli 2:28 “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.
30 Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, NA MINARA YA MOSHI”.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://chat.whatsapp.com/L3ysoFZcz058XCX9oLvKL1?s=cl&p=a&mlu=4&ilr=4
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
ZIDI KUTAFUTA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU.
FUNGUA KINYWA CHA ROHO MTAKATIFU KIHUDUMU.
ONGEZA NGUVU ZAKO ZA ROHONI.
MUNGU HAJARIBIWI NA MAOVU BALI MEMA.
Je ni kweli Bwana YESU hajui siku ya kuja kwake? (Mathayo 24:36)
Shalom nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
Ukichunguza utagundua kuna mahali ambapo watumishi wa Mungu, kwa namna fulani wanakwazika, hadi wengine wanaanzisha mashambulizi ya wazi kabisa pale wanapoona baadhi ya vitu ambavyo si vya kiungu vinasimama kwenye eneo la Injili au kazi ya Mungu.
Tengeneza picha wacha Mungu wa kweli wakati ule wanawaona mamajusi (wasoma nyota), wanawaletea habari za kuzaliwa kwa Yesu duniani, unadhani lilikuwa na ladha nzuri kwao? mchawi wa Endori analeta taarifa za Samweli, Koreshi mfalme wa kipagani Mungu anamwita mchungaji wake? Ni kama mambo yanachanganyikana hivi.
Wakati mwingine unaweza kusema mbona Mungu anajipinga mwenyewe?
Tunasoma katika maandiko..
Wakati fulani Mungu alimtokea Musa katika giza nene sana, na sisi tunajua Mungu ni nuru hakai gizani, ni wazi kuwa wote wanaotokewa na Mungu ni lazima nuru iwaangazie kama kiwakilishi chake mfano Paulo alivyotokewa na Yesu kule Dameski, lakini tunaona hapa Mungu anamwita Musa katika giza nene.
Kutoka 20:21
[21]Basi hao watu wakasimama mbali, naye Musa akalikaribia LILE GIZA KUU MUNGU ALIPOKUWAPO. [22]BWANA akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli hivi, Ninyi wenyewe mmeona ya kuwa nimenena nanyi kutoka mbinguni. [23]Msifanye miungu mingine pamoja nami; miungu ya fedha, wala miungu ya dhahabu, msijifanyie.
[21]Basi hao watu wakasimama mbali, naye Musa akalikaribia LILE GIZA KUU MUNGU ALIPOKUWAPO.
[22]BWANA akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli hivi, Ninyi wenyewe mmeona ya kuwa nimenena nanyi kutoka mbinguni.
[23]Msifanye miungu mingine pamoja nami; miungu ya fedha, wala miungu ya dhahabu, msijifanyie.
Hili ni jambo gumu ambalo huwenda liliwashangaza sana wayahudi, je Musa anaitwa na Mungu gizani? Mbona Mungu anajitokeza mahali pa ajabu hivi, gizani?
Kwanini asingemwita ndani ya mawingu meupe? Kwenye mwali wa moto kama afanyavyo? Ni kwanini Mungu afanye vile?
Ni kwasababu anataka tufahamu kuwa njia zake hazichunguziki. Yeye hakaririki.
Warumi 11:33
[33]Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!
Tukijua kuwa Mungu ni zaidi ya upeo wetu, basi tusimfunge Mungu katika namna fulani moja, kwamba ili Mungu kumbariki fulani ni lazima awe mtoaji mkubwa sana, ili Mungu ampe yule miujiza mikubwa ni lazima awe mwombaji na mfungaji.
Ili yule awe mtumishi wa kweli wa Mungu ni lazima apite chini ya walezi wa kiroho, kama hana huyo basi hawezi tumiwa na Mungu.
Ni kweli kwa sehemu kubwa ya wito wa ki-Mungu hufuata mikondo hiyo, lakini alikuwepo yule mtu anayefanya miujiza kwa jina la Yesu lakini hafuatani na Yesu kabisa wala mitume wake, mpaka mitume wakaanza kumpiga vita..baadaye wakaja kujua kuwa walikuwa wanashindana na kusudi la Mungu.(Marko 9:38-39)
Tafsiri yake ni nini?
Kuna mahali sisi kama watoto wa Mungu tunalazimika kuikubali mipaka na kukiri kuwa si kila njia ya Mungu tutaielezea ipasavyo, kwasababu anaweza kujitokeza pia katika giza nene, Hivyo tukijua hilo hatupaswi kupoteza muda wetu mwingi kupambana na watu, bali tutumie nguvu zetu nyingi kusimama na kweli, mengine yabaki kwa Mungu tukijua kuwa Iwe kwa hila au kwa nia njema, injili itahubiriwa tu, sisi tutasimama katika njia yetu aliyotuonyesha Bwana.
Shalom
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>
https://chat.whatsapp.com/L3ysoFZcz058XCX9oLvKL1?s=cl&p=a&mlu=4&ilr=4
Shekemu alikuwa ni kijana wa mkuu wa nchi ya Wahivi. Biblia inamtaja kama kijana aliyekuwa na heshima kuliko vijana ndugu zake wote.
Lakini pamoja na heshima aliyokuwa nayo kwa wazazi, ndugu na jamii iliyomzunguka, alifanya kosa moja lililosababisha mauti, si kwake tu bali na kwa familia yake yote na Taifa kwa ujumla.
Na kosa lenyewe lilikuwa ni kufanya “Uasherati” na binti wa nyumba ya “kikuhani” ya Yakobo aliyeitwa Dina.
Na baada ya kufanya uasherati mara moja tu alijua ataendelea kuwa salama kwani binti aliyelala naye hakuwa kahaba, bali alimkuta bikra, na kwasababu ni bikra alijua kuwa huyo ndie mke wa kuoa, lakini ndoto zake hizo hazikutimia.
Mwanzo 34:1 “Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka kuwaona binti za nchi. 2 Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri. 3 Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri. 4 Shekemu akamwambia Hamori, babaye, akasema, Unipatie msichana huyu awe mke wangu. 5 Basi Yakobo akasikia ya kwamba amembikiri Dina, binti yake. Na wanawe walikuwako pamoja na wanyama wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hata walipokuja. 6 Akatoka Hamori, babaye Shekemu, kumwendea Yakobo, aseme naye. 7 Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka nyikani; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, neno lisilojuzu kutendeka. 8 Hamori akasema nao, akinena, Roho ya Shekemu, mwanangu, inamtamani binti yenu, tafadhalini, mpeni amwoe. 9 Mkaoane na sisi, mtupe sisi binti zenu, nanyi mkatwae binti zetu. 10 Nanyi mtakaa nasi, na nchi hii itakuwa mbele yenu; kaeni, na kufanya biashara humo, mkapate mali humo. 11 Shekemu akamwambia babaye yule msichana na nduguze, Na nikubalike machoni penu, na mtakavyoniambia nitatoa. 12 Mjapoongeza sana mahari na zawadi, nitatoa kadiri ya mtakavyoniambia, lakini mnipe huyu msichana, awe mke wangu”…
Mwanzo 34:1 “Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka kuwaona binti za nchi.
2 Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri.
3 Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri.
4 Shekemu akamwambia Hamori, babaye, akasema, Unipatie msichana huyu awe mke wangu.
5 Basi Yakobo akasikia ya kwamba amembikiri Dina, binti yake. Na wanawe walikuwako pamoja na wanyama wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hata walipokuja.
6 Akatoka Hamori, babaye Shekemu, kumwendea Yakobo, aseme naye.
7 Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka nyikani; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, neno lisilojuzu kutendeka.
8 Hamori akasema nao, akinena, Roho ya Shekemu, mwanangu, inamtamani binti yenu, tafadhalini, mpeni amwoe.
9 Mkaoane na sisi, mtupe sisi binti zenu, nanyi mkatwae binti zetu.
10 Nanyi mtakaa nasi, na nchi hii itakuwa mbele yenu; kaeni, na kufanya biashara humo, mkapate mali humo.
11 Shekemu akamwambia babaye yule msichana na nduguze, Na nikubalike machoni penu, na mtakavyoniambia nitatoa.
12 Mjapoongeza sana mahari na zawadi, nitatoa kadiri ya mtakavyoniambia, lakini mnipe huyu msichana, awe mke wangu”…
Baada ya kijana Shekemu kuomba sana kupewa binti Dina, kwa mahari nyingi na kwa kusihi sana, majibu yake yalikuwa tofauti, kwani wana wa Yakobo walimwua Shekemu na baba yake pamoja na watu wote wa nchi ile na mali zao zote wakazichukua.
Mwanzo 34:26 “Wakawaua Hamori, na Shekemu mwanawe, kwa makali ya upanga, wakamtwaa Dina katika nyumba ya Shekemu, wakatoka. 27 Wana wa Yakobo wakawajilia hao waliouawa, wakauteka nyara mji kwa sababu wamemharibu umbu lao. 28 Wakachukua kondoo zao, na ng’ombe zao, na punda zao, na vitu vilivyokuwamo mjini, navyo vilivyokuwako kondeni. 29 Wakatwaa na mali zao zote, na watoto wao wote, na wake zao, na vyote vilivyokuwamo nyumbani mwao wakavichukua mateka”
Mwanzo 34:26 “Wakawaua Hamori, na Shekemu mwanawe, kwa makali ya upanga, wakamtwaa Dina katika nyumba ya Shekemu, wakatoka.
27 Wana wa Yakobo wakawajilia hao waliouawa, wakauteka nyara mji kwa sababu wamemharibu umbu lao.
28 Wakachukua kondoo zao, na ng’ombe zao, na punda zao, na vitu vilivyokuwamo mjini, navyo vilivyokuwako kondeni.
29 Wakatwaa na mali zao zote, na watoto wao wote, na wake zao, na vyote vilivyokuwamo nyumbani mwao wakavichukua mateka”
Huo ndio ulikuwa mwisho wa Shekemu ambaye anatajwa kuwa kijana mwenye heshima kuliko watoto wote wa mzee Hamori (Mwanzo 34:19).
Shekemu alitanguliza zinaa kabla ya ndoa, na baadae alipoitafuta ndoa kwa gharama kubwa aliiokosa na kulipwa mauti.
Yawezekena nawe ni kijana ambaye una heshima, huwenda huna rekodi yoyote ya uzinzi, wala huna sifa mbaya mtaani wala kwa wazazi, fahamu kuwa wewe ni windo kubwa la ibilisi kuliko wale ambao maisha yao yote ni zinaa,
Labda na wewe upo katika hatua kama ya Shekemu, umemwona binti tena wa imani na mwenye heshima na asiye na rekodi yoyote chafu, na moyoni unasema “nilale naye kwanza halafu nitamwoa”..kabla haujafikiria kufanya hivo mkumbuke Shekemu.
Inawezekana wewe binti unafuatiliwa na kijana mwenye heshima zake na hadhi zake, na moyoni unasema ngoja nimkubalie kwani atakuoa, Ni kweli wote mnaweza kuwa na malengo ya kuoana, hata Shekemu na Dina baada ya zinaa bado waliendelea kupendana, pasipo kujua kuwa dhambi haijui viapo mlivyoahidiana, bali yenyewe inaleta mauti iliyoumbiwa.
Leo utalala na huyo kijana lakini ndio heshima yako imeisha hapo hatuoni mahali panatajwa Dina kuolewa, zaidi imebaki kumbukumbu ya sifa mbaya ambayo mpaka sasahivi tunaisoma na itaendelea kusomwa vizazi vyote.
Na wewe aibu yako itaendelea kwa vizazi vyako vyote,
Binti jitunze, kijana jitunze..kuchochea mapenzi kabla ya wakati wake ni sawa na kuchochea moto huku umeshika galoni la mafuta ya petroli.
Wimbo Ulio Bora 2:7 “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe”
Zipo hatua za kufuata ikiwa unahitaji kuingia katika ndoa, wasiliana na viongozi wako wa kiroho watakufundisha hatua kwa hatua, usikurupuke na kutanguliza zinaa kabla ya ndoa.
Kijana ni nani kibiblia?
KAMA WEWE NI KIJANA, BASI FAHAMU YAFUATAYO NA UCHUKUE TAHADHARI!
kwanini yule kijana aliitupa ile nguo ya kitani chini na kukimbia uchi?
PALE WATUMISHI WANAPOSHINDWA KUTOA PEPO.
NENO NA MAOMBI~ Sehemu ya 2 (AMRI YA UPENDO)
Ukisoma Injili ya Luka utaona Bwana Yesu anafundisha vitu vitatu tofauti vinavyopotea.
1) Kondoo: Luka 15:3-7
2) Shilingi: Luka 15:8-10
3) Mwana: Luka 15:11-32
> Kondoo anapotea kutoka kwenye kundi, na kuishi maporini, anaanza kutafutwa na mchungaji.
> Shilingi inapotea ndani ya nyumba, inaanza kutafutwa na mwanamke.
> Lakini mwana anamwacha makusudi baba yake anachagua kwenda nchi ya mbali. Anangojewa na baba yake.
Haya ni makundi matatu ya watu ndani ya nyumba ya Mungu.
Kundi la kwanza ni aina ya watu ambao hutoweka katikati ya jamii ya waaminio, ukichunguza sababu sio kwamba wamedhamiria wao kuwa hivyo, lakini udanganyifu wa dhambi, anasa za kidunia, na mafundisho ya uongo, huwapoteza, na kutokomea huko. wakati wa mwanzoni hawajijui kama wanapotea…lakini baadaye wanapojikuta katika ukame wa kiroho, katika kuharibika, kuvurugwa, ndio wanagundua kuwa njia waliyoiendea sio sahihi.
Wanaanza kutaabika huku na huko, kutafuta msaada lakini hawaupati, mpaka watakaporudi kwenye zizi lao. Sasa Hapa ni wajibu wa kanisa kuwafuatilia, watu na namna hii.
Ndio hapo Bwana Yesu anasema ……
Luka 15:4-6
[4]Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone? [5]Naye akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi. [6]Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea.
[4]Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?
[5]Naye akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi.
[6]Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea.
Lakini kundi la pili hufananishwa na ile shilingi iliyopotea. Kumbuka ilipotelea ndani, sio nje.
Hili ni kundi la watu ambalo haliondoki ndani ya kanisa, lakini linapotelea likiwa huko huko. Hawa ndio wapo kwenye hatari kubwa zaidi kwasababu wanaweza wakawa wanaendelea kuwa viongozi, wazee wa kanisa, waimba kwaya lakini maisha yao yapo mbali na Kristo, ni wazinzi, walevi, washirikina.
Kama wewe ni mmojawapo, tubu haraka kwasababu kuwa katikati ya kundi haimaanishi umekubaliwa na Mungu, Yuda aliishi na Bwana Yesu miaka yote, na akafanya miujiza lakini bado alikuwa upotevuni.
Halikadhali kanisa linapowagundua watu kama hawa, ni wajibu wao kuwarejesha aidha kwa mafundisho, au maonyo, au makaripio ili wapone.
Ndio hapo Bwana Yesu akasema..
Luka 15:8-10
[8]Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione? [9]Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea. [10]Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.
[8]Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione?
[9]Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea.
[10]Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.
Lakini kundi la tatu, ni wale ambao kwa makusudi kabisa wanaamua kumwacha Mungu na kurejea ulimwenguni. Ndio mfano wa yule mwana mpotevu.
Hawa ni wale wanaosema kuanzia leo mimi sipo nanyi, habari za wokovu sitaki. Wanaamua kujiachanisha moja kwa moja na kanisa au habari za kiroho.
Hawa ni kuwaombea, Bwana awape moyo wa kuzingatia wenyewe mioyoni mwao warejee, lakini kanisa linapaswa lifahamu wanaporejea hawapaswi kuwatenga au kuwaona hawafai…kanisa halipaswi kuwa kama yule mwana mkubwa, bali linapaswa liwapokee na kuwajenga upya, kwasababu Mungu anawapokea.
Luka 15:28-32
[28]Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi. [29]Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu; [30]lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona. [31]Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako. [32]Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.
[28]Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi.
[29]Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu;
[30]lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona.
[31]Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako.
[32]Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.
Je mahali ulipo umemwona aliyemmoja wa kundi hili?
Mfuatilie, mwonye, mwombee.
Jibu ni ndio endapo hatutajua tabia za Roho Mtakatifu.
Katika biblia tunaona Petro alipokea Roho Mtakatifu, siku ile ya Pentekoste pamoja na watu wengine, lakini baadaye mtume Paulo anamkemea kwa dhambi ya unafki, ya kula na mataifa, wakati akaapo nao lakini pale wayahudi wanapokuja kuketi naye anajitenga nao.(Wagalatia 2:11-14)
Hiyo ni kutuonyesha kuwa mtu anaweza akapokea kweli Roho Mtakatifu lakini bado akasumbuliwa na dhambi fulani.
Je! Hiyo husababishwa na nini, ilihali tunajua alipo Roho Mtakatifu dhambi haimtawali mtu?
Ni vema kujua kuwa ipo tofauti ya mtu kuwa na Roho Mtakatifu, kujazwa Roho na kuenenda kwa Roho.
Pale mtu anapookoka moja kwa moja hupokea Roho Mtakatifu, lakini ili Roho huyo awe na nguvu ndani ya Mtu, kupokea tu haitoshi bali anapaswa ajazwe, (Waefeso 5:18) lakini sio tu kujazwa bali ajifunze kuenenda kwa Roho, akihakikisha kuwa hamzimishi ndani yake.
Kuenenda kwa Roho ni kutembea na Roho Mtakatifu wakati wote. Ni rahisi mtu kujazwa Roho awapo katika mazingira fulani tu maalumu labda kanisani, au kwenye mifungo au maombi. Lakini kuenenda kwa Roho ni kumruhusu atembee na yeye kila mahali awapo. Ambapo itathibitika kwa tabia ya mtu ya kujikana nafsi, kujichunguza, kuomba, kujitahidi kuliishi Neno katika mwenendo wake wa kila siku. Mtu wa namna hii akisimama vema Roho wa Mungu humjawa na kumsaidia kushinda wingi wa dhambi.
Na hivyo kamwe hataweza kusumbuliwa na dhambi ya namna yoyote. Hivyo tukirudi kwa Petro. Ni wazi kuwa eneo mojawapo alilegea ndio maana akanaswa na dhambi ya unafki.
Wagalatia 5:16
[16]Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
Hivyo tujue kuwa kwa jinsi tunavyompa Roho Mtakatifu nafasi mioyoni mwetu ndivyo ambavyo, tunapokea nguvu ya kuzishinda dhambi kirahisi, lakini pale tunapomzuia ndivyo tunavyoanza kulemewa na dhambi.
Pokea Roho, jazwa Roho, enenda kwa Roho, usimzimishe Roho, usimhuzunishe Roho. Utaushinda ulimwengu.
Tukitembea na mambo yote hayo. Roho ni thabiti kwetu
Jina la Bwana YESU libarikiwe, karibu katika kujifunza Neno pamoja na Maombi.
Utangulizi: Kusoma Neno bila Kuomba, au kuomba bila Neno la kusimama nalo ni sawa na kitamba cha bendera kisicho na mlingoti, kitapelekwa huku na kule na kupotea…
Kupitia mfululizo huu na tafakari hizi tutapata mwongozo sahihi wa kuomba kwa kusimama na maandiko matakatifu ya Biblia.
Yuda 1:2 “MWONGEZEWE REHEMA na AMANI na UPENDANO”.
Mambo haya matatu ni muhimu kuwa nayo kama watu tuliookoka
1. OMBI LA REHEMA (Tumia dk 45):
Rehema kwa tafsiri rahisi ni kibali ambacho mtu anaweza kukipokea kutoka kwa MUNGU au kwa Mtu mwenzake, ambacho kinazaa Msamaha, ufadhili, huruma, au msaada.
Kwamfano Mtu aliyerehemiwa na MUNGU, anakuwa amesamehewa makosa yake, au kupewa kibali na Baraka..
Zaburi 78:8 “Lakini Yeye, KWA KUWA ANAYO REHEMA, Husamehe uovu wala haangamizi. Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake, Wala haiwashi hasira yake yote”.
Na rehema za MUNGU ni mpya kila siku.. na zilikuwepo tangu zamani (Zab. 25:6) na zitaendelea milele..
Maombolezo 3:22 “Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu”
Kwahiyo chukua nafasi hii kuomba REHEMA za MUNGU ziongezeke juu yako, kwani utazipokea ikiwa utaomba kwa kumaanisha na kwa imani..
Kutoka 20:6 “nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu”.
Waebrania 4:16 “Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji”
Lakini pia tunaweza kuwa watu wa Rehema kwa wanadamu wenzetu.
Kama MUNGU anavyoturehemu tunapomwomba, ni lazima na sisi tuwe watu wa kurehemu wengine,
Mathayo 8:32 “Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; 33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?”.
Mathayo 8:32 “Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi;
33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?”.
Faida ya kuwa watu wa rehema kwa wenzetu, ni sisi pia kurehemiwa na MUNGU..
Kwahiyo chukua nafasi hii kuomba MUNGU akakuongezee Rehema ndani yako kwa wengine.
2. OMBI LA AMANI. (Tumia dk. 45)
Ipo amani ya MUNGU na amani ya ulimwengu.
Yohana 14:27 “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga”.
Maandiko yanasema pasipo upendo sisi sio kitu, katika Sehemu ya pili ya darasa letu hili la Neno na Maombi tulijifunza mwongozo sahihi wa kuombea Upendo..Kwahiyo fungua link ifuatayo kupata mwongozo huo.
Usikose sehemu ya tano (05) ya darasa letu hili la Neno na Maombi.
NENO NA MAOMBI~ Sehemu ya 1 (MAPENZI YA MUNGU)
NENO NA MAOMBI~ Sehemu ya 3 (UTAKASO WA KINYWA)
FAIDA ZA MAOMBI YA USIKU
MWONGOZO WA MAOMBI YA ASUBUHI.
WhatsApp