Kuhusu sisi

 

Wingu la Mashahidi  ni huduma iliyo chini ya kanisa la NURU YA UPENDO WA KRISTO.

yenye lengo la kusambaza  habari njema za wokovu ulioletwa na Bwana wetu Yesu Kristo, kwa njia mtandao

Tunaamini katika Biblia Takatifu kama ndio  kitabu pekee kilichovuviwa na Roho Mtakatifu kwa lengo la kuwakomboa na kuwakamilisha wanadamu. Hivyo mafundisho yote yaliyo katika tovuti hii huegemea hapo.

Tunaamini kuwa wokovu unatoka kwa mtu mmoja tu naye ni YESU KRISTO, Na huo unapatakana kwa kumwamini, kisha kubatizwa kwa jina lake, na kisha kupokea Roho Mtakatifu sawasawa na  Matendo 2:38

Tunaamini kuwa Tupo katika nyakati za mwisho, na Hivyo tunatazamia kutokea kwa Bwana wetu Yesu Kristo kwa tukio la unyakuo.

Zingatia: Wingu la Mashahidi wa Kristo Sio dhehebu la “Mashahidi wa Yehova”. bali jina hili limetoka katika kitabu cha Waebrania 12:1

 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

Hivyo mimi na wewe pia tunaweza tukawa sehemu ya wingu hilo la mashahidi wa Bwana wetu Yesu Kristo, kama walivyokuwa wale wa wakati ule. Na ndio lengo la huduma hii, kuwakaribisha watu wote waliookoka kutoka katika pande zote za ulimwengu wenye imani moja na sisi kushirikiana katika kuipeleka injili ya Bwana wetu Yesu kwa watu wote.

Tunapatikana Tegeta, Tanzania.

Kwa maswali au msaada wa wokovu basi piga namba zifuatazo, au tuandikie  kwenye boxi la maoni chini. +255789001312/+255693036618

    Print this post

    Tutumie ujumbe au Piga

    Mawasiliano

    Je! utapenda kujumuika nasi? tutumie ujumbe wako

    +255-789-001-312

    Tunapatikana

    Dare es salaam, Tegeta, - Tanzania

    Barua pepe

    info@wingulamashahidi.org

    Utapenda kuchangia?

    Mchango wako utaifanya neema ya Bwana wetu iwafikie na wengi zaidi, na hivyo pale watakapomshukuru Mungu basi ni kwa ajili yako pia, Na Mungu atakubariki