Yesu alimaanisha nini kusema ‘haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemu’?

Yesu alimaanisha nini kusema ‘haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemu’?

SWALI: Bwana Yesu alikuwa na maana gani kusema ‘haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemu’.

Luka 13:33

[33]Pamoja na hayo imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa; kwa kuwa haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemu.


JIBU: Bwana Yesu alikuwa anaeleza asili ya mji wa Yerusalemu nyakati zote ulivyokuwa wa mauaji, mji ambao ungepaswa uwe wa kupokea manabii wa Mungu, lakini kinyume chake uligeuka mji wa kuwaua Manabii…

Sasa kusema maneno yale ni kutokana na taarifa aliyoletewa na wale mafarisayo kuwa Herode anataka kumwangamiza, hivyo aondoke pale aende mji mwingine…ndipo Bwana Yesu akawaambia ‘haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemu’ yaani haipaswi nabii afe nje ya Yerusalemu…

Akimaanisha nini?

Manabii wengi wa Mungu, waliuliwa pale pale Yerusalemu hivyo hata na yeye kuangamia hapo si jambo geni, …

Na ndivyo ilivyokuwa

Mfano wa hao katika maandiko alikuwa;

Zekaria mwana wa Yehoyada (2Nyakati 24:20-21). Ambaye aliuliwa hekaluni

Mwingine ni Uria nabii (Yeremia 26:20 – 24)

Na manabii wengine wengi ambao hawajatajwa, moja kwa moja katika maandiko waliuawa Yerusalemu…ndio sababu ya Yesu kusema maneno Haya;

Mathayo 23:37-39

[37]Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!

[38]Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa. 

[39]Kwa maana nawaambia, Hamtaniona kamwe tangu sasa, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana. 

Jambo hili hujirudi sasa rohoni..

Watu wote ambao wanaipinga injili mioyoni mwao leo, hata kama hawajashiriki moja kwa moja kuwarushia mawe watu wa Mungu, ni shirika moja tu na wale waliokuwa wanawaua manabii wa Bwana zamani.

Ndivyo walivyodhani mafarisayo kwamba wenyewe hawahusiki na mauaji ya manabii wa Bwana, angali wanampinga yeye waziwazi, kwa unafiki wao aliwaambia maneno haya..

Mathayo 23:29-36

[29]Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki,

[30]na kusema, Kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii.

[31]Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii.

[32]Kijazeni basi kipimo cha baba zenu.

[33]Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?

[34]Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;

[35]hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.

[36]Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.

Hii ni hatari kubwa sana kwa walio nje ya Kristo.

Mwamini Yesu leo uoshwe dhambi zako. Upokee uzima wa milele. Kwingineko si salama.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Yesu alikuwa na maana gani aliposema ‘tena siku ile hamtaniuliza neno lolote (Yohana 16:23)

MAUTI NA KUZIMU ZIKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE.

Kwanini MUNGU aangamize watoto kwenye gharika ya Nuhu?

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments