Bwana  alikuwa na maana gani aliposema. “leo na Kesho natoa pepo na kuponya siku ya tatu nakamilika?”

Bwana  alikuwa na maana gani aliposema. “leo na Kesho natoa pepo na kuponya siku ya tatu nakamilika?”

JIBU: Tusome:
Luka 13:32 “Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika.
33 Pamoja na hayo imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa; kwa kuwa haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemu”.
Ili kuelewa vizuri sentensi hiyo vizuri, hebu tafakari mfano huu.. Mwalimu kawaambia wanafunzi wake “leo na Kesho tunazungumza lakini siku ya mtihani hamtaniona” Kwa sentensi hiyo, huwezi kusema kuwa baada ya siku ya Kesho kutwa basi siku inayofuata ndiyo siku ya Mtihani mwalimu anayoizungumzia! Bali utajua mwalimu anamaanisha kuwa siku hizi ambazo sio za mtihani ndio siku ambazo wapo huru kuzungumza na mwalimu wao, kazipa jina la ujumla Lakini itakuja siku moja maalumu huko mbeleni labda baada ya miezi kadhaa, au miaka ambayo wanafunzi hawatapata nafasi tena ya kuzungumza na mwalimu…na hiyo itakuwa siku ya mtihani..ambayo inaweza kuwa ni baada ya miezi kadhaa mbeleni au miaka kadhaa..Hivyo neno “leo na Kesho na Kesho kutwa” halimaanishi kipindi cha siku mbili au tatu, bali kipindi cha muda fulani mrefu kidogo.
Na hapo Kristo alimaanisha vivyo hivyo, kwamba leo na Kesho na Kesho kutwa (yaani kipindi chote ambacho yupo na wanafunzi wake) atakuwa anatoa pepo na kuponya lakini “siku ya tatu”, ambayo itakuja huko mbeleni kipindi atakapofufuka baada ya kusulubiwa na kukaa kaburini siku tatu..Hiyo ndiyo itakuwa siku yake ya kukamilka..
Kristo alipofufuka ndio ulikuwa Ukamilifu wa Huduma yake, asingefufuka basi ushuhuda wake ungekuwa wa Uongo, Lakini alifufuka kutuhakikishia sisi kuwa Yeye katumwa kutoka mbinguni, na kashinda mauti, hivyo anaweza kutuondolea nasi pia mauti ya rohoni, inayotokana na dhambi.
 
Bwana akubariki.
 

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

 

Mada Nyinginezo:

ULE MSALABA UNAOWEKWA KWENYE KABURI, NA ILE IBADA INAYOFANYWA VINA UMUHIMU WOWOTE KWA MKRISTO?

KIFAA BORA CHA MATUMIZI.

JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?. NA JE! TUKIFIKA MBINGUNI TUTAFANANA WOTE?

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

NG’OMBE MWEKUNDU ALIYEZALIWA ISRAELI, ANAFUNUA NINI?

UNYAKUO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments