NG’OMBE MWEKUNDU ALIYEZALIWA ISRAELI, ANAFUNUA NINI?

NG’OMBE MWEKUNDU ALIYEZALIWA ISRAELI, ANAFUNUA NINI?

Utakumbuka tarehe 28/8/2018 kulitokea tukio la kihistoria Israeli la kuzaliwa kwa ng’ombe mke mwekundu. Kulingana na chuo cha kidini kijihusishacho na mambo ya Hekalu kinasema jambo hilo halikuwahi kutokea kwa zaidi ya miaka 2000, tangu kuharibiwa kwa hekalu la pili pale Yerusalemu. Wanaamini tangu wakati wa Musa hadi kuharibiwa kwa hekalu la pili jumla ya ng’ombe tisa tu wa namna hiyo ndio waliotolewa sadaka kwa ajili ya kuwatakasa watu.
 
Tunasoma wakati wana wa Israeli walipokuwa jangwani Mungu alitoa maagizo kwa kuhani mkuu, kwamba atwae ng’ombe mmoja wa kike, mwekundu, asiye na mapungufu ya aina yoyote, yaani asiwe na jeraha au kilema chochote, asiwe na manyoya ya rangi nyingine yaliyochangikana na hayo mekundu hata kama likionekana nyoya moja tu tayari huyo hafai, anapaswa awe hajazaa, pia anapaswa awe bado hajapandwa na mtu yeyote, au hajatumika kwa kazi yoyote ile, hata kama atakuwa ni mwekundu lakini akiwa ameshawahi kuwekewa hata tambara tu la mizigo juu yake au amefungwa nira shingoni mwake huyo tayari hastahili…
 
Sasa hiyo ndio iliyokuwa inamfanya ng’ombe huyu awe adimu, atakayekidhi vigezo vyote hivyo.. ng’ombe huyo alikuwa anatumika kuwasafisha wana wa Israeli, baada ya kuteketezwa nje ya kambi, majivu yake yalikuwa yanachukuliwa na kuchanganywa na maji masafi, kisha mtu yeyote ambaye alikuwa amenajisika aidha kwa kuishika maiti, au kushika kaburi, au kuwa na maiti nyumbani, au alishika maiti ya mnyama aliyekufa au mzoga basi alinyunyiziwa maji hayo yaliyochanganywa na hayo majivu kwanza kwa muda wa siku tatu, kisha siku ya saba anakuwa safi ndipo aruhusiwe kuingia hemani au hekaluni. Hiyo ilikuwa ni sheria mtu yeyote na aliyekiuka amri hiyo ilikuwa adhabu yake ni kifo.
 
Hivyo ng’ombe huyo alikuwa ni wa muhimu sana katika ibada za hekaluni, yaani kwa namna nyingine bila kuwepo ng’ombe huyo hakuna shughuli zozote za hekuluni zinaweza kuendelea.
 
Hesabu 19:1 “Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
 
2 Hii ndiyo amri ya sheria Bwana aliyoagiza, akisema, Waambie wana wa Israeli wakuletee ng’ombe mke mwekundu asiye na kipaku, mkamilifu, ambaye hajatiwa nira bado;
 
3 nanyi mtamleta kwa Eleazari kuhani, naye atakwenda naye nje ya kambi, na mtu mmoja atamchinja mbele yake”;
 
Lakini Kama wengi tunavyofahamu ng’ombe huyu katika agano jipya anasimama kama Bwana wetu Yesu Kristo, yeye ndiye dhabihu iliyotolewa isiyokuwa na ila wala mawaa, Bwana Yesu alikuwa mkamilifu sana hakuna asiyejua hilo, alikuwa hana doa la kasoro yoyote katika mwili wake wala katika roho yake, alikuwa ni dhabihu iliyokamili tayari kwa kafara kwa ajili yetu.
 
Ni ng’ombe mwekundu kwasababu ni ng’ombe wa damu, kumfunua Bwana wetu Yesu Kristo kwamba agano atakaloingia na sisi ni damu yake mwenyewe. Na ndio maana hata tukisoma katika ufunuo, tunamwona siku ile atakaporudi mara ya pili atakuwa na vazi jekundu lililochovya katika damu, kufunua ni jinsi gani alivyotukomboa sisi kwa damu yake..
 
Ufunuo 19:11 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
 
12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
 
13 Naye amevikwa VAZI LILILOCHOVYWA KATIKA DAMU, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.”
 
Sasa leo hii kwanini tukio kama hilo limejirudia Israeli?, Kumbuka Wayahudi ni watu wa mwilini, na pale walipo wanajiandaa kwa kuja kwa masihi wao na kwa ujenzi wa hekalu la tatu, ambalo wanaamini kwa kupitia hilo Masihi ndipo atakaposhukia..Na kwa muda mrefu walikuwa wakijiuliza hata hekalu litakapojengwa, tutampata wapi huyu ng’ombe mwekundu wa ajili ya utakaso wa watu watakao najisika kwa zile sababu tulizozitaja hapo juu.
 
Lakini mwaka jana tarehe 28/8/2018 tendo hilo lilitimia, Na hiyo ilikuwa ni Mungu kuwathibitishia kuwa hivi karibuni Hekalu litajengwa, Kumbuka ndugu kwetu sisi wakristo kinaweza kisiwe kitendo cha maana sana kwani sisi tunafahamu kuwa dhabihu halisi ni YESU KRISTO na sio ng’ombe. Lakini wayahudi bado hawajapata neema hiyo, hivyo Mungu pia anasema nao kwa ishara wanazoziamini ili tu kuwathibitishia kuwa wakati wao upo karibu sana..Hata siku ile watakapofumbuliwa macho na kumwamini masihi, ndipo watafahamu kila kitu.
 
Ni wakati gani huu tunaishi? Una habari kuwa neema itahama na kuiendea Israeli? Na ikishahamia Israeli, sisi huku mlango utakuwa umeshafungwa? Ni dhiki kuu ya mpinga kristo itakuwa inaendelea, wakati huo Unyakuo utakuwa umeshapita.. Leo hii unaichezea hii neema laiti ungeona ni wayahudi wangapi wanalia usiku na mchana pale YERUSALEMU kwenye ukuta wa maombolezo, wanamlilia Mungu wao aje kuwaokoa na kuwapigania kama ilivyokuwa katika enzi za kale, ambapo kimsingi ni kweli watarudiwa. halafu sisi huku watu wa Mataifa tunachezea wokovu, siku zimeshakaribia sana, watauona wokovu ambao wanautaabikia sasa.
 
Wayahudi leo hii wanasema ikiwa Mungu hakutuletea ng’ombe huyu kwa muda wa zaidi ya miaka 2000 na amemleta leo, ni ishara kuwa huu ndio wakati aliouandaa wa sisi kumjengea hekalu.
 
Ndugu hatuna mengi ya kuzungumza hapo, huu ni wakati wa kuchagua ni upande upi wa kusimama, Kipindi hichi kifupi tulichobakiwa nacho kitumie vizuri, maana hatujui kesho ni nini kitatokea? tubu dhambi zako zote leo kwa Bwana Yesu kama bado hujafanya hivyo, jitwike msalaba wako umfuate, kisha ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi kwa jina la YESU KRISTO upate ondoleo la dhambi zako, kulingana na Matendo 3:38 ili Mungu akupe Roho wake mtakatifu ambaye atakulinda na kukuongoza katika kuijua kweli yote ya Biblia..Kumbuka pasipo Roho Mtakatifu hakuna Unyakuo..Unasubiri nini?
 
Bwana akubariki.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP 

Mada Nyinginezo:

WAISRAELI WENGI SANA WANARUDI KWAO SASA.

AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA.

SIKU YA TAABU YA YAKOBO.

NOTI YA UFALME WA MBINGUNI.

SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!

UNYAKUO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Amani Tipaay
Amani Tipaay
11 months ago

Kijana anaongelewa kama nani kibiblia

Emirates
Emirates
3 years ago

Is this going to happen next year