Category Archive Uncategorized @sw-tz

KUFAHAMU SIO KUJUA

Jina la Bwana na Mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze maandiko..

Ipo tofauti kati ya “kufahamu jambo” na “kulijua jambo”.. Unaweza kulifahamu jambo lakini usilijue kwa undani, vivyo hivyo kuna tofauti ya “kuyafahamu maandiko” na “kuyajua maandiko”.  Hivi ni vitu viwili vyenye tofauti kubwa sana, hebu tujifunze kidogo kwa namna gani.

Tusome habari ifuatayo kisha tufafanue..

Mathayo 22:23 “Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza,

24 wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao.

25 Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake.

26 Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba.

27 Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.

28 Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye.

29 Yesu akajibu, akawaambia, MWAPOTEA, KWA KUWA HAMYAJUI MAANDIKO WALA UWEZA WA MUNGU.

30 Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni”.

Nataka tuzingatia hilo neno “MWAPOTEA, KWA KUWA HAMYAJUI MAANDIKO WALA UWEZA WA MUNGU”.

Kumbuka hawa watu waliokuja kumwuliza Bwana hilo swali ni MASADUKAYO, ni watu wa dini, wanayoyafahamu maandiko karibia yote ya kwenye torati, na hapa wanamjia YESU kwa swali linalotoka katika maandiko ya MUSA (torati), wakisema “Mtu akifa basi mke wake anaruhusa ya kuolewa na ndugu wa karibu”.. jambo ambalo ni kweli kabisa lipo kwenye Biblia.

Lakini pamoja na kwamba walikuwa wanayafahamu hayo maandiko, bado Bwana YESU anawaambia “Hawayajui maandiko” na tena wanapotea sana.

“29 Yesu akajibu, akawaambia, MWAPOTEA, KWA KUWA HAMYAJUI MAANDIKO WALA UWEZA WA MUNGU.

30 Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni”.

Tuirudie tena habari hii katika Marko..

Marko 12:24 Yesu akajibu, akawaambia, JE! HAMPOTEI KWA SABABU HII, KWA KUWA HAMYAJUI MAANDIKO wala uweza wa Mungu?

25 Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni.

26 Na kwa habari ya wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa, Sura ya Kijiti, jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?

27 Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Hivyo mwapotea sana”.

Kumbe wakati ambao wanajidhania kuwa wanayajua maandiko kwa wingi wa mistari wanayoifahamu vichwani mwao, Kristo alikuwa anawaona hawajui chochote, na hiyo ndio sababu kuu ya kupotea kwao, hawayajui maandiko bali wanayafahamu tu.

Ndugu hatupaswi kuwa kama compyuta au simu ambao inaweza kuwa na vitu vingi pamoja na biblia nzima, lakini haiyajui maandiko, na wala yale maandiko hayaisaidii kwa chochote.

Hatupaswi kuwa na idadi kubwa ya mistari vichani ambayo haina ufunuo wowote. Mistari yenye nguvu na ibilisi anayoigopa ni ile iliyopo moyoni iliyobeba ufunuo, maana yake yenye uhai katika maisha ya mtu, na inayomwongoza, na yenye nguvu, na inayothibitisha imani.

Masadukayo walikuwa wanafahamu tu Musa kasema, na kujitamba katika hayo, pasipo kujua kuwa andiko bila ufunuo ni bure..

Sasa swali ni je!, tutayajuaje maandiko badala ya kuyafahamu tu?

Kinachotangulia ni kuyafahamu, ni lazima tuyafahamu na kufahamu kunakuja kwa kuyasoma au kuyasikia yanaposomwa.. baada ya kuyafahamu hatua inayofuata ni kuyajua. Na njia pekee ya kuyajua maandiko ni kwa kupitia Roho Mtakatifu..

Huyu peke yake ndiye anayeweza kutuhamisha kutoka katika kuyafahamu maandiko mpaka kuyajua, kwani anapoingia ndani ya Mtu, anakuwa ni Mwalimu mwingine wa ziada, kukufundisha maana za ndani ya maandiko uyasomayo, anakuchambulia na kukufundisha mambo ambayo hata ukirudia kusoma tena hilo andiko ulilolisoma utaona kama vile ni jingine kabisa, na huo ndio uhudumu wa agano jipya unaotajwa katika 2Wakorintho 3:6, ambao unatutosheleza.

2Wakorintho 3:6 “Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha”.

Je tayari umempokea Roho Mtakatifu?.. kama bado mwamini YESU na tubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha, kisha tafuta ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU KRISTO, baada ya hapo Roho Mtakatifu ataingia ndani yako na kukaa na wewe siku zote, kwani ahadi ya Roho Mtakatifu ni kwa kila mtu.

Matendo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE UNAZAA MATUNDA NA KUWAPONYA MATAIFA?

Ipi tofauti ya “Majibu” ya Maombi na “Majaribu”.

Ipi Tofauti ya Agano jipya na Agano la Kale?.

TOFAUTI KATI MAASKOFU, MASHEMASI, WAZEE WA KANISA NI IPI?

Nini tofauti kati ya kileo na divai ?

Je watu watu wasio haki hawatahukumiwa kabisa kulingana na Zaburi 1:5?.

Swali: Turejee…

Jibu: Zaburi 1:5 “Kwa hiyo wasio haki HAWATASIMAMA hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki”.

Andiko hili halimaanishi kwamba wasio haki (yaani watu waovu) hawatasimamishwa siku ya hukumu, La! haimaanishi hivyo, bali kinyume chake inamaanisha “watasimamishwa” lakini hawataweza kujitetea wala kushinda hukumu.

Neno “kusimama” linamaanisha “kushinda au kufanikiwa”… kwahiyo Wasio haki wote watahukumiwa, na sehemu nyingine nyingi katika maandiko zinathibitisha hilo..

2Petro 2:9 “basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, NA KUWAWEKA WASIO HAKI KATIKA HALI YA ADHABU HATA SIKU YA HUKUMU;

10  na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu. na kudharau mamlaka”.

Ni njia moja tu mtu anaweza kuitumia kuepuka hukumu ya MUNGU, nayo ni Kumwamini Bwana YESU KRISTO na kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, na kubatizwa kwa maji na kwa Roho Mtakatifu (Marko 16:16).

Yohana 5:24 “Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; WALA HAINGII HUKUMUNI, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Ni kwa namna gani YESU KRISTO atawahukumu walio hai na waliokufa?

Je biblia inajichanganya kwa habari ya hukumu ya Mungu (Yohana 12:47 na Yohana 5:22, 27).

Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.

Nini maana ya Hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma?

Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.

Je! Hayo Mambo ya duniani na ya mbinguni ni yapi?

Yohana 3:12

[12]Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni? 

SWALI: Je! Hayo Mambo ya duniani ni yapi? Na hayo mambo ya mbinguni pia ni yapi Yesu aliyoyamaanisha?


JIBU: Ukianza kusoma tokea vifungu vya juu utaona sababu ya Bwana Yesu kusema maneno hayo, ni baada ya yule Nikedemo mkuu wa mafarisayo kumfuata usiku ili kumuuliza maswali, lakini Yesu akamjibu kwa kumwambia kuhusu habari za kuzaliwa mara ya pili, lakini jambo hilo likawa gumu sana kwa nikodemu kulipokea…akamweleza Bwana yawezekanikaje mambo hayo? …Ndipo Yesu mwishowe akayasema maneno hayo;

12]Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni? 

Sasa hapo hamaanishi alikuwa anafundisha mambo ya duniani, hapana…bali alikuwa anatumia mifano ya duniani kueleza yale ya rohoni ili iwe rahisi watu kuelewa..kwamfano hapo alitumia mifano ya mtu kuzaliwa, vilevile akatumia mifano ya tabia ya upepo kumfafanulia Nikodemu aelewe mtu wa rohoni naye anavyopaswa awe…mahali pengine alitumia mifano ya wakulima, wafanyabiashara, maharusi, wavuvi, wafalme. wanyama n.k.

Ilikufundisha ufalme wa Mungu ulivyo na unavyofanya kazi..

Lakini mambo ya mbinguni ni yale ambayo hayana uhalisia na maisha yetu ya duniani kabisa…mambo hayo huwezi yaeleza kwa mifano ya kidunia..Hivyo ni kuyapokea tu kwa imani.

Kwamfano jinsi gani hekima ya Mungu isipopatikana popote isipokuwa ndani ya Yesu Kristo. Na jinsi gani Mungu aliumba ulimwengu kwa kupitia Kristo, ambaye alikuja kama mwana aliye Mungu yuleyule (Yohana 1:1-4).

Mambo hayo hayakuweza kusadikika kwa hekima za kibinadamu, ndio maana yalifichwa yakaja kufunuliwa baadaye kwa Roho Mtakatifu kwa mitume kuwa ndiye Mungu mwenyewe katika mwili( 1Timotheo 3:16)

Ndio maana wayahudi na hata watu wengine leo hii wa dini wanashindwa kuelewa iweje Mungu awe na mtoto, wakati hana mshirika…halafu huyo huyo mtoto awe ndio yeye tena.

Jambo kama hili halina mifano ya kibinadamu ya kujitosheleza kuelezea, ni kuamini tu!…lakini kwa imani waziona kazi zake na kujua hakika Kristo ndiye Mungu mwenyewe bila tashwishwi…Hivyo amini tu, uelewa kamili utaufahamu ufikapo mbinguni, ni sawa na Yesu alivyomwambia Nikodemu upepo huvuna upendako, hujui utokako vilevile hujui uendako, lakini sauti yake waisikia…ndivyo ilivyo katika asili ya uungu wa Mungu.. Tunamjua Kristo kuwa ni Mungu kwa kazi zake kuu na timilifu juu ya maisha yetu.. 

Ni nini Bwana anataka wewe ujue.

Sehemu kubwa ya mambo yanayotuzunguza yanahubiri habari za ufalme wa mbinguni. Kama hatutaelewa kwa kuitafakari mifano hii, kamwe tusidhani tutaelewa yale yasiyoingia maanani kabisa tuyasikiapo.

Je! Umempa Yesu maisha yako? Kumbuka hizi ni siku za mwisho na Yesu amekaribia kurudi, unasubiri nini usiokoke?

Tubu sasa upokee uzima wa milele. Ikiwa unahitaji msaada huo wa kuokoka basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi;

Kwa ajili ya mwongozo wa sala ya Toba na ushauri.

+255789001312 / +255693036618

Bwana akubariki.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UNAWAZA NINI SASA, JUU YA UFALME WA MBINGUNI?

BALI WANA WA UFALME WATATUPWA NJE!.

JIFUNZE KUTOA KATIKA HAZINA YAKO VITU VIPYA NA VYA KALE.

Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu. 

2 Yohana 1:10-11

[10]Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu. 

[11]Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu. 

 Ni salamu ya namna gani ambayo ililengwa hapo?

JIBU: Ukisoma habari yote tokea juu utaona mtume Yohana anazungumzia kundi la wadanganyifu ambao walitokea wengi duniani wakati ule, ni kundi la watu waliopinga kuja kwa Yesu katika mwili kwa namna ya kibinadamu, akasema hao ndio wapinga Kristo.

 Na mbeleni akatoa katazo la kutowakaribisha hata majumbani kwao, wala kuwapa salamu, maana kuwapa salamu ni kushiriki kazi zao mbovu.

Swali je ni salamu ya namna gani ililengwa hapo.?

Salamu zinazozungumziwa hapo si salamu hizi za kijamii za “umeamkaje, au shikamoo, au za mchana” hapana bali ni salamu za kiroho ambazo hata wakati ule wayahudi walipozisema zilimaanisha ushirika mmoja katika kiimani. Kwamfano, walipokutana walibusiana na kusema “Amani ya Bwana iwe pamoja nawe”..

Sasa salamu kama hiyo utajiuliza ni bwana yupi ikiwa huyo mwingine haamini katika fundisho kama lenu.. ukimsalimia basi unakubaliana na bwana wake ambaye hajaja katika mwili. Tayari umeshazishiriki kazi zake.

Ni sawa na leo labda tuseme unakutana na watu wanaomwamini kweli Yesu, lakini Yesu ambaye hajafufuka, yupo kaburini mpaka sasa, halafu anakuja anakusalimia “Bwana Yesu asifiwe” na wewe unasema Amina..Mtu mgeni akipita akakusikia atajua kuwa mna imani moja kuhusu Yesu Kristo ambaye hajafufuka.

Hivyo hata kwa wakati huu, salamu zetu za kiroho zisimame mahali ambapo tunajua imani tulio nayo kuhusu Kristo ni moja.

Kwasababu salamu tu, hutangaza, zina nguvu kama lilivyo fundisho. 

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

ANDALIZI LA MWISHO LA UJIO WA MPINGA KRISTO.

JAWA SANA MOTO ULAO.

Fanyeni Yote kwa Jina la Yesu Kristo

Mfundishe mtoto namna ya kutumia jina la Yesu katika kutenda mambo yake yote.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

 

MAUMIVU YA DHAMBI

Tambua Dhambi inaua chini kwa chini..

Je unajua ni kwa namna gani?….

Hebu fikiri kama mwili wako usingewekewa hisia ya maumivu kabisa, maana yake ukijikata na kisu hauhisi maumivu, ukipigwa husikii maumivu, ukinywa kitu chenye kudhuru husikii maumivu yoyote ya tumbo, ukiwa na vidonda vya tumbo husikii maumivu yoyote..

Unadhani ni nini kingetokea baada ya muda fulani?..bila shaka ni “kifo cha ghafla”.. kwanini? Kwasababu ungepata majeraha ambayo yangeendelea kukuharibu ndani kwa ndani, na usingekujua kama kuna tatizo kwasababu hakuna hisia yoyote ya maumivu utakayokupa taarifa ya tatizo mahali fulani, hali kadhalika usingekuwa mtu wa kujijali, kwani maumivu yanasaidia kujijali na kujihadhari.

Sasa dhambi iko hivo hivyo…haina hisia yoyote ya maumivu katika mwili, kiasi kwamba mtu anapoifanya anaweza kudhani hajaingiza madhara yoyote katika maisha yake, lakini mwisho wake ni kifo cha ghafla.

Hiyo ndio saababu ya Bwana MUNGU kumwambia Adamu pale bustanini kuwa asile  yale matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, kwani atakufa, agizo hilo halikuwa kwa faida ya MUNGU bali kwa faida ya  ADAMU na kizazi chake, ili waishi na wasife.

Mwanzo 2:17 “walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika”.

Na vinyo hivyo maandiko yanasema kuwa mshahara wa dhambi ni “MAUTI”

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Ndugu, dhambi haina maumivu mwilini, hautasikia maumivu yoyote mwilini ukishamaliza kuzini, au ukishafanya anasa, ukitukana, ukiishi maisha ya dhambi, n.k lakini madhara yake yanakuja ghafla utaona amani uliyokuwa ndani yako inakufa ghafla, furaha yako inakufa ghafla, Baraka zako zinazima ghafla, na mwisho kifo cha mwili kinahitimisha ikiwa mabadiliko hayatafanyika mapema.

Lakini habari njema na nzuri ni kwamba kwa YESU hata kama mambo baadhi yameshakufa kutokana na dhambi, ipo ahadi ya ufufuo wa mambo hayo endapo mtu atamkimbilia YESU kwa njia ya kutubu na kujinyenyekeza mbele zake, ile amani iliyokufa inarudi mara dufu, ile furaha iliyokufa inafufuka, ule ushindi ulioupoteza unarudi, ile afya iliyopotea inarudi na mambo mengine mazuri..

Je ni wewe leo ambaye dhambi imekuulia mambo yako mazuri, na ni ghafla?.. na hujui nini cha kufanya?.. hakuna atakayekutoa hapo, hata upate pesa kiasi gani bado shida itakuwepo, hata dunia nzima ije upande wako na kukufariji bado utaona kuna kupungukiwa mahali fulani..

Suluhisho lipo kwa mmoja tu, nakuambia ukweli.

Na huyo si mwingine zaidi ya YESU MNAZARETI,  huyo atakugeuzia ukurasa wa maisha na kukupa uzima wa hapa duniani na ule wa milele ujao (uzima tele).

Yohana 10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

11 Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo”.

Unachopaswa kufanya ni kukiri kuwa wewe ni mkosaji, na dhamiria kuacha dhambi, yeye atashughulika kukuongezea nguvu ya kushinda dhambi, na pia tafuta ubatizo sahihi wa maji mengi kwa jina la Bwana YESU KRISTO, (Matendo 2:38), hapo utakuwa umekamilisha hatua zako za wokovu, kwani yule Roho Mtakatifu ataingia ndani yako, na kukufanyia miujiza ambayo hata ukihadhithia huwezi kueleweka.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UVUKISHE MIPAKA UPENDO WAKO.

JINSI YA KUACHA DHAMBI INAYOKUTESA.

SHUGHULIKA NA HASIRA INAYOKAA KIFUANI

SAFARI YA KUUONA USO WA MUNGU.

MKATAE MWAJIRI HUYU MBAYA.

EPUKA UVUGUVUGU.

Uvuguvugu ni ile ya hali ya  kuchanganya mambo mema na mazuri (mema na mabaya kwa wakati mmoja).. Na roho ya uvuguvugu ilianzia EDENI, ndiyo shetani anayoitumia kuangusha watu.

Kwa namna gani?

Turejee mojawapo ya miti iliyokuwepo Edeni, Biblia inatuambia kulikuwepo na “Mti wa Ujuzi wa MEMA na MABAYA” ambao Bwana MUNGU alitoa maagizo wasiuguse wala kula matunda yake.

Huu ulikuwa ni mti wenye sifa ya UVUGUVUGU, yaani wenye “Mema na Mabaya wakati huo huo”.. Na ibilisi alijua mwanadamu anapenda Uhuru wa kufanya mambo yote kwa pamoja, (mema kidogo na mabaya kidogo).. na alianza kupitisha ushawishi huo kwa Hawa, na pasipo kuzitambua hila za ibilisi, tukaingia katika kosa la moja kwa moja.

Ndugu ibilisi hamtegi mtu wa Mungu (aliyesimama) kwa mabaya.. bali atamtega kwa “Mabaya yaliyochangamana na mema”.. Ni ngumu kwa ibilisi kumwachisha mtu wa MUNGU mema!.. hawezi kumfundisha moja kwa moja aache mema, ni jambo gumu sana kwake, ingekuwa ngumu kwa shetani kumshawishi HAWA pale bustanini amwambudu yeye na aache kumwambudu MUNGU, Hawa asingeweza kumsikiliza nyoka)..ni jambo gumu sana.

Lakini adui alikuja na injili ya uvuguvugu, kwamba aendelee na mema, lakini na mabaya pia ayafanye kidogo na MUNGU atamkubali!.. kwaufupi afanye mema kidogo na mabaya kidogo, asiwe moto, awe vuguvugu kwani bado MUNGU atamkubali..pasipo kujua ni mtego mbaya, sana wa kutapikwa moja kwa moja na MUNGU.

Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, KWA SABABU UNA UVUGUVUGU, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu”.

Ni jambo hilo hilo, analiendeleza leo katika kuwaangusha watu wa MUNGU waliosimama, anawashawishi kuamini kuwa Ukiwa mtu wa kiMungu sana utachanganyikiwa, ni lazima uchanganye na mambo mengine madogo madogo ya kiulimwengu..

Ijapokuwa umeshakuwa mkristo, unaenda kanisani, unatoa sadaka, basi siku moja moja onja mvinyo, ijapokuwa hutukani, huna ugomvi na mtu na unasaidia masikini sio mbaya pia siku mojamoja kwenda kwenye dansi za starehe, ijapokuwa huibi, hudhulumu sio mbaya ukifanya uasherati mara moja moja..Hii ni sumu hatari sana, iliyowaangusha wazazi wetu wa kwanza.

Jihadhari na roho ya uvuguvugu, kwani unamtoa mtu moja kwa moja kutoka katika Neema ya MUNGU.

Je umempokea YESU?. Unao uhakika wa uzima wa milele baada ya maisha haya?..Fahamu kuwa uzima wa milele upo kwa YESU tu, na si mwingine.

Yohana 17:3 “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KUJITAKASA NI MUHURI WA UTAKATIFU

MAANA HUYAWAZI YALIYO YA MUNGU, BALI YA WANADAMU

Biblia inamaana gani inaposema “Mungu wa neema yote” (1Petro 5:10)

Je Sulemani alifuga nyani? (2Nyakati 9:21)

MAISHA YA UVUGUVUGU, YANAMFANYA MUNGU AUMWE.

NINAYEPENDEZWA NAYE

Mathayo 3:16 “Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;

17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, huyu ni mwanangu, mpendwa wangu, NINAYEPENDEZWA NAYE”.

Nataka tuone hiyo sehemu ya mwisho ya andiko inayosema.. “NINAYEPENDEZWA NAYE”.. hasemi ninayefurahiwa naye, au ninayeshangiliwa naye, au ninayetukuzwa naye, au ninayeshabikiwa naye, au ninayeburudishwa naye, bali ametumia neno “NINAYEPENDEZWA NAYE”.. Hili ni neno kubwa sana.

Ni lazima tutafute “kumpendeza Mungu” siku zote hilo ndio jambo kuu na Mungu analolihitaji kutoka kwetu…

Waefeso 5:9 “kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli;

10 MKIHAKIKI NI NINI IMPENDEZAYO BWANA”.

Kumpendeza MUNGU maana yake ni kufanya mambo yanayoufanya moyo wa MUNGU kukufurahia na hayo si mengine zaidi ya matendo ya UTAKATIFU.

1Wathesalonike 4:2” Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.

3 Maana haya NDIYO MAPENZI YA MUNGU, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;

4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake KATIKA UTAKATIFU NA HESHIMA;

5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.

Na utakatifu ni ule wa nje na ndani, sio tu wa ndani bali pia wa nje, maana yake jinsi unavyouweka mwili wako pia.

Warumi 12:1” Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe DHABIHU ILIYO HAI, TAKATIFU, YA KUMPENDEZA MUNGU, ndiyo ibada yenu yenye maana.

2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu”.

Epuka kuwa mshabiki wa MUNGU bali tafuta “kumpendeza Mungu”.. Mtu ambaye ni mshabiki wa Mungu ni yule anayejua sana mambo ya Mungu na sheria zake, lakini hazifanyi na pia hazipingi huyu ni mfano wa mtu ambaye ni mshabiki.

Ni yule mtu ambaye anakubali Mungu ni mwenye nguvu, ni wa upendo, ni mwenye haki na hata kumsifia mbele za watu, lakini kimaisha na mwenendo hamfuati MUNGU, bali anafuata njia yake, na ibilisi ndiye anayemtumikia. (huyu ni mshabiki)

Epuka kuwa mshabiki, bali kuwa mwana wa MUNGU ambaye UNAMPENDEZA MUNGU aliyekuumba. Kuwa mtakatifu mwilini na rohoni.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

FUNGUA KINYWA CHA ROHO MTAKATIFU KIHUDUMU.

KUJITAKASA NI MUHURI WA UTAKATIFU

MAPENZI YA MUNGU NI YAPI?

YAFAHAMU MAPENZI KAMILI YA MUNGU KWA MAADUI ZAKO.

ANDALIZI LA MWISHO LA UJIO WA MPINGA KRISTO.

Nini maana ya kuinuliwa juu ya nchi? (Yohana 12:32).

Swali: Bwana YESU alikuwa na maana gani aliposema “Nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu”?


Jibu: Turejee..

Yohana 12:32 Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu”.

Kuinuliwa juu kwa Bwana YESU, kupo kwa namna mbili (02), namna ya kwanza ni “KUINULIWA MSALABANI” na namna ya pili ni “KUINULIWA NA WINGU kwenda mbinguni”.

Tuangalie maana moja baada ya nyingine..

     1. KUINULIWA MSALABANI.

Hii ndio maana ya kwanza kabisa ya “Kuinuliwa kwa Bwana YESU”.. Na kunafananishwa na wakati ule Musa alipomwinua nyoka wa shaba jangwani, ili kila mtu amtazamapo apone..

Yohana 3:14 “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;

15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye”.

Kwa nguvu ile ile iliyowavuta watu wenye majanga ya kuumwa na nyoka jangwani, ndio nguvu hiyo hiyo iliyoachiwa pale msalabani, kwamba kila mtu mwenye mzigo wa dhambi na vifungo, autazamapo msalaba wa Bwana YESU kwa ufunuo, basi atapata msaada wa kufunguliwa kutoka katika dhambi, magonjwa na kila aina ya mateso ya ibilisi.

      2. KUINULIWA NA WINGU.

Hii ni maana ya pili ya kuinuliwa juu kwa Bwana YESU, kulikotoa nguvu ya kuwavuta watu kwa Mungu..

Turejee Matendo 1:8..

Matendo 1:8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, AKAINULIWA, wingu likampokea kutoka machoni pao”.

Kwa namna gani au kwa njia gani, baada ya kuinuliwa Bwana YESU juu katika wingu watu walivutwa kwake na hata sasa tunavutwa kwake, si kwa njia nyingine zaidi ya Roho Mtakatifu.

Kwasababu alisema baada ya kupaa kwake atashuka Roho Mtakatifu, ambaye huyo ataushuhudia ulimwengu kwa habari ya dhambi, haki na hukumu (Yohana 16:8).

Kupitia nguvu za Roho Mtakatifu, siku ile tu ya Pentekoste aliposhuka watu elfu tatu walimwamini Bwana YESU na nguvu zake, uamsho mkuu ambao mitume hawajawahi kuuona, hiyo ni kuonesha kuwa ahadi ya Mungu (yaani Roho Mtakatifu), ina nguvu zaidi ya vitu vyote.

Zekaria 4:6 “Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, BALI NI KWA ROHO YANGU, asema Bwana wa majeshi”.

Je Neno la msalaba umelitii??.. Umesamehewa dhambi?.. umeoshwa dhambi zako kwa damu yake?.. je umekimbilia msalabani upate wokovu?

1Wakorintho 1:18 “Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.

19 Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa”.

Mwamini YESU leo kama bado haujafanya hivo, na tubu kwa kumaanisha dhambi na ubatizwe.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii..

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MANENO SABA YA YESU MSALABANI.

YESU MNAZARETI,  ANWANI YA MSALABA.

MSALABA NI ZANA YA UJENZI WA MAISHA YAKO.

Je! Bwana Yesu alisulubiwa juu ya msalaba au juu ya mti uliokuwa wima?

TAFUTA UTAKASO WA SEHEMU KUU NNE ZA MWILI WAKO.

JE UMEVULIWA KUTOKA MAJINI?

Jina la Mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze pamoja Biblia.

Bwana alipokutana na Petro aliambiwa “TANGU SASA UTAKUWA UKIVUA WATU”.  Hii ni kauli pana, ambayo ni muhimu tuijadili kwa kina kidogo..

Luka 5:10  “na kadhalika Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, waliokuwa washirika wa Simoni. Yesu

akamwambia SIMONI, USIOGOPE, TANGU SASA UTAKUWA UKIVUA WATU”.

Hapa Bwana YESU alifananisha “Uvuvi wa Samaki” na “Uvunaji wa watu” . Kwa ufupi Bwana YESU alifananisha watu na “Samaki”… Kama vile samaki wanavyovuliwa kutoka majini hali kadhalika watu wanavuliwa kutoka upotevuni.

Sasa kama maji yanavyohusika katika “Uvuvi wa samaki” vile vile maji pia yatahusika “uvuvi wa watu” kama ishara.. na hapa ndio tunakuja kuona umuhimu wa UBATIZO.

Wengi hatuoni umuhimu wa Ubatizo katika kukamilisha wokovu, lakini Ubatizo wa maji mengi unasimama kama muhuri wa kukamilisha wokovu wa mtu (Soma Marko 16:16).

Unapobatizwa kwa maji mengi na kwa jina la BWANA YESU ni ishara ya kwamba umevuliwa kutoka katika ulimwengu..

Sasa jiulize, Umeona wapi samaki anavuliwa kutoka katika nchi kavu?.. Vile vile wewe na mimi kama samaki tuliovuliwa ni lazima tuwe na ishara ya kutoka majini, ndio hapa linakuja agizo la ubatizo.

Na samaki akishatoka majini anapoteza uhai wa maisha yake ya kwanza, na vile vile baada ya ubatizo mtu anapoteza uhai wa maisha yake ya kwanza ya dhambi (maana yake yale maisha ya dhambi anayafia, anakuwa kiumbe kipya).

Je umeshabatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO (sawasawa na Matendo 2:38, Matendo 10:48 na Matendo 19:5).. Kama bado unasubiri nini?.. je bado unaendelea kushikilia mapokeo ya dini na dhehebu hata baada ya kuujua ukweli wa Biblia?

Siku ile hatutahukumiwa kulingana na Mapokeo tuliyopokea bali kulingana na maneno yaliyoandikwa katika vitabu vyote sitini na sita vya kwenye Biblia..

Ufunuo 20:12 “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao”.

Maneno ya Mungu ndani ya Biblia ndio yatakayotuhukumu siku ya mwisho, maana yake siku ile tutaulizwa kwa yale yaliyoandikwa kwenye biblia sio kwa yale tuliyoyapokea kwenye dini zetu..

Kwa namna gani?.. Hebu tuingie ndani kidogo kulifafanua hili..

Mtu mmoja alimfuata Bwana YESU na kumwuliza tiketi ya kuurithi uzima wa milele, hebu tusome jibu la Bwana YESU Mkuu.

Luka 10:25 “Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?

26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?”

Tazama jibu la Bwana hapa?.. hakumwambia “umerithishwa nini na wazazi, au umefundishwa nini kwenye dini yako”.. Lakini alimwambia “Imeandikwa nini” lakini sio tu imeandikwa nini, bali pia “Unasomaje”

Ikimaanisha kuwa wakati wa Mwisho, watu watahukumiwa kwa yaliyoandikwa katika Biblia..Na moja wapo ya jambo lililoandikwa katika maandiko ni ubatizo. Sasa kupuuzia agizo la msingi namna hii ni hatari sana, hatutakuwa na la kujibu siku ile, ikiwa tulijua kweli na hatukuifanyia kazi.

shetani amepofusha fikra za watu wengi katika siku hizi za mwisho, na kuwafanya wasijue wala kuona umuhimu wa ubatizo pamoja na baadhi ya mambo mengine ya msingi katika Biblia.

2Wakorintho 4:4 “ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu”.

Bwana atusaidie sisi tusiwe miongoni mwao wanapofushwa fikra na ibilisi.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

AGIZO LA TOBA LINAENDANA NA UBATIZO!.

TOFAUTI YA UBATIZO WA YOHANA NA UBATIZO WA BWANA YESU

Ni sahihi kusema sikuitiwa kuhubiri ubatizo kama Paulo alivyosema (1Wakorintho 1:17)?.

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

WOKOVU UKIHARAKISHA USIUZUIE.