Moja ya ombi kubwa la watu wa Mungu, pale wanapojikuta wameokoka, ni kubadilishwa mazingira waliyopo, wapelekwe kwenye mazingira mengine yenye uwepo wa karibu zaidi na Mungu, Kwasababu wakiangalia kwa sehemu kubwa mambo ambayo yanawakosesha huchangiwa na mazingira yao. Mazingira husika yanaweza kuwa mitaa wanayoishi, shule wanazosoma, maeneo ya kazi/ biashara walipo, watu wanaowazunguka, hata nchi yanayotokea.
Hii ni hali ya kawaida, na hufikia hatua wengi kuwaza mioyoni mwao, “Kama ningekuwa eneo Fulani, basi ningekuwa na mahusiano ya karibu na Mungu, ningekuwa mwombaji sana, ”
Lakini Je! Kuwaza hivyo ni sahihi?
Ndio kuwaza kubadilishwa mazingira yanayokosesha, ni vema, lakini kuwaza kuwa Hapo ulipo huwezi kumpendeza Mungu kwa viwango vyote ni uongo,. Kwasababu maandiko yanatuonyesha Mungu amewaweka watumishi wake katika mazingira yote, yaani mazingira rafiki na yale yasiyo rafiki, kwa mapenzi yake, na kuthibitisha kuwa kote kote, kumpendeza Mungu kunawezekana. Kwasababu dunia moja.
Bwana aliwaweka watakatifu Babeli, alikuwepo Shedraka, Meshaki, Abednego na Danieli.
Hawa waliishi katika taifa la kipagani usiokuwa wa kawaida,ni taifa lenye shinikizo kubwa la mtu kuabudu miungu hata kama hapendi, lenye mikorogo ya kila namna ya maovu. Lakini watu hawa walisimama vema na Bwana.
Waliwezaje?
Yafuatayo ni mambo ambayo yaliyatenda mpaka ufanikiwa kuishi katika viwango vyote vya ukamilifu.
1) Waliitangaza Imani yao mapema.
Mwanzoni kabisa akina Danieli walipochukuliwa Babeli, na kusomeshwa elimu ya wakaldayo,tunaona walipewa vyakula ambavyo ni najisi, lakini Danieli alisimama mapema na kumwomba msimamizi, kulishwa vyakula vingine visivyo najisi. Na Mungu akawa Pamoja nao. Wakatambulika tangu mapema kuwa wao ni watumishi wa wayahudi wasiojichangamana na desturi za kimataifa.
Hawakungoja, miaka ipite baadaye..bali mezani tu, wanaanza kutangaza misimamo yao.
Danieli 1:8-9
[8]Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi. [9]Basi Mungu alimjalia Danieli kupata kibali na huruma machoni pa huyo mkuu wa matowashi.
[8]Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi.
[9]Basi Mungu alimjalia Danieli kupata kibali na huruma machoni pa huyo mkuu wa matowashi.
Hii ni desturi ambayo na sisi, kama watoto wa Mungu babeli, tuwapo katikati ya wasioamini, tujitambulishe mapema. Hiyo itasaidia sana wao kutokukuhusisha katika matendo yao ya giza wakijua kuwa wewe ni mwamini.
Wengi wameshindwa kung’atuka katika mazingira mabovu kwasababu ya kushindwa kujitambulisha wao ni akina nani, kwa wanaowazunguka.
2) Walikuwa waombaji
Danieli akiwa Babeli, alijijengea desturi na kutwa mara tatu, kupiga magoti na kuomba, akijua kuwa nguvu ya kusimama na kuendelea mbele ilitegemea sana maombi…
Ijapokuwa alikuwa na majukumu makubwa kama waziri katika taifa lakini hakuruhusu muda wake mahususi wa maombi kuibwa.
Danieli 6:10
[10]Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
Vivyo hivyo na sisi tuwapo popote pasipofaa, hatuwezi sema hatuna muda wa sala. Ikiwa umebanwa upo muda wa chakula cha mchana kazini unaweza tumika nafasi kusogea mahali tulivu na kuomba.
3) Walikubali kujitwika misalaba yao.
Kujitwika msalaba maana yake ni kukubali kuipokea imani kwa gharama yoyote ile, yaani kama ikitokea nitatengwa kwasababu ya imani yangu, nitafungwa, nitauawa..Je nipo tayari?
Ndivyo ilivyokuwa kwa Meshaki, shedraka, Abednego, Danieli, Yusufu.
Wote hawa walikubali kutupwa kwenye matanuru ya moto, kwenye magereza, matanuru ya simba, walipojaribiwa.
Vivyo hivyo na sisi, lazima tufahamu mapema kuwa, imani haipendwi, ulimwengu sio rafiki kwetu, kama ikitokea tunalazimishwa kuikana imani je! Tutachukua hatua gani?
Wengine wameshindwa na majaribu mbalimbali ya Babeli, wameanguka katika uzinzi,wizi, upagani kwa sababu tu ya kuhofia kupoteza kazi zao, familia zao, heshima zao, mali zao, uhai wao.
Ili uweza kuishi vema Babeli, ufahamu huu wa kujitwika msalaba ni lazima uwe nao tangu mwanzo kabisa wa kuamini kwako. Kumbuka sikuzote nguvu ya kuushinda ulimwengu upo katika msalaba.
4) Waliwajibika kwa bidii na uaminifu.
Utaona hawakuwa wavivu, au walegevu, au watu wasiokuwa na shughuli zao maalumu, bali waliwajibika..Danieli pamoja na wenzake walisoma ili kupata elimu na kuwajibika katika shughuli za kifalme mpaka wakaonekana hakuna wa kufanana na wao kwa hekima na ujuzi,
Yusufu naye alisimama kwenye majukumu yake, wala hakuna mahali alionekana mlegevu. Na wote hawa walitanguliza uaminifu.
Walijua kabisa kutowajibika ni mlango mwingine wa shetani, kuinua majaribu.
Waefeso 4:27-28
[27]wala msimpe Ibilisi nafasi. [28]Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.
[27]wala msimpe Ibilisi nafasi.
[28]Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.
Hivyo na sisi pia tuwapo kwenye Babeli zetu, tuwe makini kuwajibika kwa bidii na uaminifu, tuepuke uvivu, kama watoto wa Mungu ni wajibu kujishughulisha.
Tukifanikiwa kuwa na uwiano huo mzuri, Neema ya Mungu itatusaidia.
Bwana akubariki.
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
MNARA WA BABELI
Ipi tofauti ya Falme, Mamlaka na Wakuu wa giza (Waefeso 6:12)
KWA KUWA FURAHA YA BWANA NI NGUVU ZENU.
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ