Jina la mwokozi wetu YESU KRISTO litukuzwe mpendwa, karibu tujifunze habari za uzima.
Wapo wengi wanaojifariji kuwa baada ya unyakuo watakuwa na nafasi ya pili. Ndugu Kama hutataka kuitii nguvu ya Roho Mtakatifu itokayo kwa Mungu inayokushawishi leo hii umgeukie Mungu, basi fahamu kuwa hutakuwa na tumaini lolote huko mbele baada ya unyakuo biblia imeweka wazi kabisa kuna NGUVU nyingine itakayoachiwa kutoka kwa Mungu juu ya watu waliosalia kuwafanya wauamini uongo wa mpinga-kristo. Nguvu hiyo biblia inaiita nguvu ya upotevu.
Jiulize ni kitu gani kitakachomfanya mpinga-Kristo apate nguvu dunia nzima kwa muda mfupi sana kama huo, Unadhani ni jambo rahisi tu mtu mmoja atokee ateke dunia nzima, halafu ishikamane naye? Ni wazi kuwa kuna nguvu nyingine itaachiliwa hapo ndani ya mioyo ya watu wamwamini yeye, wazikubali sera zake na ustaarabu wake, na mfumo wake bandia, na ishara zake na ajabu zake za uongo.
Ndugu ukiwepo wakati huo hakuna namna utaweza kumchukia, utaungana naye tu, hatakuwa mtu mkatili kama wewe unavyomfikiria, kwamba atakuwa anaua watu ovyo ovyo tu barabarani, hilo halitawezekana ufalme wake utasimamaje sasa, sharti mataifa yamkubali , apendwe na watu wote na serikali zote na majeshi yote duniani..yafanye kazi pamoja na yeye, ili baadaye apate nafasi ya kuwaangamiza wayahudi na baadhi ya watu wachache watakoanekana huku kwenda kinyume na ustaarabu wake mpya.
Ikiwa leo hii bado hauuoni etendaji kazi wake, unatazamia vipi siku ile umtambue, kwasababu biblia inasema tangu kipindi cha mitume SIRI ya kuasi inatenda kazi, bado tu mwasisi wa hiyo ASI kufunuliwa tu, ambaye ndio mpinga-kristo mwenyewe.na hilo sio jambo kubwa kutokea, kama mipango yake yote imeshakita mizizi kinachongojewa ni nini kama sio kufunuliwa.
2Wathesalonike2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; 4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu. 5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo? 6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake. 7 MAANA ILE SIRI YA KUASI HIVI SASA INATENDA KAZI; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa. 8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake; 9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutendakwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; 10 na katika madanganyo yote yaudhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. 11 Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; 12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
2Wathesalonike2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
7 MAANA ILE SIRI YA KUASI HIVI SASA INATENDA KAZI; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutendakwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
10 na katika madanganyo yote yaudhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11 Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;
12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
Unaona hapo? Sasa Mpinga-Kristo huyu atatokea katika utawala wa RUMI biblia imelithibitisha hilo, ndani ya dini yenye wafuasi wengi leo hii duniani, na kiongozi wake anapata sifa na kukubalika sasa na dini zote duniani na mataifa yote, Na katika kiti hicho anachokalia huko VATICAN ndicho hicho hicho mpinga-kristo atakaponyanyukia..
Ndugu, ulimwengu huu upo ukingoni sana, bado unayachezea maisha yako mpaka siku nguvu ya upotevu itokayo kwa Mungu ikuingie, ili uamini uongo uende kuzimu?. Ni jambo la kuogopesha sana. Geuza NIA yao mtazame YESU, UNYAKUO wa kanisa upo karibu.
Mungu akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
UTENDAJI KAZI WA MPINGA-KRISTO.
SIRI YA MUNGU.
ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO.
Rudi Nyumbani
Print this post