Yohana Mbatizaji alizaliwa huko Uyahudi miezi michache kabla ya kuzaliwa Mwokozi wa Ulimwengu Yesu Kristo, Baba yake mzazi aliitwa Zekaria aliyekuwa Mlawi, ambaye alikuwa ni kuhani, akihudumu katika Nyumba ya Mungu illiyokuwepo huko Yerusalemu…Mama yake aliitwa Elizabeth ambaye alikuwa ana undugu wa karibu na Bikira Mariamu mama yake Yesu.
Habari za kuzaliwa kwake kimiujiza, zinapatikana kwa urefu katika kitabu cha (Luka 1:1-60).
Maandiko yanasema Yohana Mbatizaji alijazwa Roho Mtakatifu tangu akiwa tumboni mwa mama yake (Luka 1:15). Na inasadikiwa kuwa miaka michache sana baada ya kuzaliwa kwake wazazi wake wote wawili walifariki. Na hivyo akaondoka na kwenda kukaa majangwani, mpaka siku alipotokea tena hadharani kuhubiri habari za msamaha na toba.
Aliitwa Yohana Mbatizaji kutokana na ufunuo alioupata wa ubatizo. Hapo kabla kulikuwa hakuna mwingine aliyekuwa anafanya ubatizo Zaidi yake, ndio maana alijulikana kama Yohana Mbatizaji, kumtofautisha na wakina Yohana wengine.
Yohana Mbatizaji sio Yohana yule aliyeandika kitabu cha Ufunuo, aliyeandika kitabu cha Ufunuo ni Yohana aliyekuwa mwanafunzi wake Yesu. Yohana Mbatizaji hakuandika kitabu chochote katika Biblia
Yohana Mbatizaji, maandiko yanasema alikuwa ndiye Eliya aliyetabiriwa atakayekuja kumtengenezea Bwana Njia (Luka 1:17). Atakayeigeuza mioyo ya baba iwaelekee Watoto.
1. Yohana Mbatizaji anaigeuzaje mioyo ya mababa iwaelekee watoto?
2. Je! Ni nani atakayeiguza mioyo ya Watoto iwaelekee mababa?
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
About the author