SWALI: Nini maana ya mstari huu Yohana 12:35
Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako.
JIBU: Yesu alipokuwa duniani, alijilinganisha na Nuru ya uimwengu huu (jua), Yohana 11:9-10…Na hivyo mara kwa mara katika mafundisho yake aliwasisitiza wayahudi juu ya jambo hilo, lakini hawakulielewa.
kwa kawaida jua huwa halizimi, lakini pia huwa halitulii mahali pamoja(kwa jinsi ya kawaida). Litachomoza, litazama,.litaendelea hivyo hivyo katika mzunguko wake. Wakati linaangaza upande mmoja, upande mwingine wa dunia ni giza.
Sasa wayahudi walipomwona Kristo, wengine walimpokea, wengine walimpinga, wengine walimwonea wivu, wengine walimwita mchawi.
Lakini wote hawa, Neema bado ilikuwa juu yao. Bado Kristo alikuwa anawakusanya kama vile kuku akusanyaye vifaranga vyake chini ya mbawa zake (Luka 13:34). Yesu hakudhubutu kwenda kuhubiri kwenye mataifa mengine ambayo yalihitaji hata kumfanya mfalme, ijapokuwa walikuwa wanampinga vikali.
Sasa ndio hapa akawaambia..kwambo hili halitaendelea sana…kuna wakati pia nuru hii mnayoiona sasa itawafikie na wengine..
ndio hapo akawaambia..
“Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako”.
Maana yake ni kuwa anawaambia aminini mapema, kwasababu nguvu hii inayowalilia mioyoni mwenu itaondoka … Mkikataa neema, mkikataa kujazwa Roho, Kamwe hamtaweza kulishinda giza kwa nguvu zenu.
Na tunaona ni kweli, jambo hilo liliendelea kwa kipindii kifupi, baada ya Kristo kufufuka, na kupaa, injili kidogo kidogo ikaanza kutoka kwa wahayudi.ikaenda kwa watu wa mataifa yaani mimi na wewe..
Tangu ule wakati, wa mitume, mpaka leo hii inakaribia sasa miaka 2000, wayahudi bado hawajafumbuliwa macho, kwasababu wokovu ni neema kuamini. Sio utashi wa mtu.
Sasa leo hii sisi watu wa mataifa tunayo injili, lakini kanuni ya Nuru ni ileile, huzunguka. Na kwetu pia haitadumu milele. Mungu aliahidi ule mwisho unapokaribia kufika (ambao ndio huu) atawarudia tena Israeli kwa kipindi kifupi. na hivyo kwa upande wetu, hakutakuwa na neema tena ya wokovu itakayokuwa imesalia..
Warumi 11:25-26
[25]Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
[26]Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa,
Mwokozi atakuja kutoka Sayuni;
Atamtenga Yakobo na maasia yake.
Hii ni kutufunisha pia Bwana hasemi na wayahudi tu, bali na anasema sisi pia…
Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako.
Je unaenda katika nuru hiyo? Kama bado wasubiri nini. Geuka leo uoshwe dhambi zako upokee uzima wa milele, usipofanya hivyo kamwe huwezi kulishinda giza.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine
MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.
Nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho,
(Opens in a new browser tab)Mistari ya biblia kuhusu maombi.(Opens in a new browser tab)
About the author