Katika agano la kale, Israeli walikuwa na makusanyiko mengi, ambapo walikutanika kumfanyia Mungu ibada, na kuzishika sikukuu. Lakini pia yalichaguliwa makusanyiko mengine yaliyoitwa mikutano/makusanyiko ya makini. Makusanyiko haya yalifanyika katika siku ya saba ya sikukuu ya Pasaka, na siku ya nane, baada ya sikukuu ya vibanda. Katika siku hiyo hawakuruhusiwa kufanya kazi yoyote. Bali ilitengwa kwa ajili ya kujitakasa, au kujisogeza karibu na Mungu,
Hivi ni vifungu baadhi vinavyoielezea siku hiyo;
Hesabu 29:35 Tena siku ya nane mtakuwa na kusanyiko la makini sana; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; 36 lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kusongezwa kwa moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana; ng’ombe mume mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu saba. Walawi 23:34 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni sikukuu ya vibanda muda wa siku saba kwa Bwana. 35 Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi. 36 Mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yo yote ya utumishi Kumbukumbu 16:8 Siku sita utakula mikate isiyotiwa chachu; na siku ya saba na uwe mkutano mtukufu kwa Bwana, Mungu wako, usifanye kazi yo yote.
Hesabu 29:35 Tena siku ya nane mtakuwa na kusanyiko la makini sana; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi;
36 lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kusongezwa kwa moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana; ng’ombe mume mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu saba.
Walawi 23:34 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni sikukuu ya vibanda muda wa siku saba kwa Bwana.
35 Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi.
36 Mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yo yote ya utumishi
Kumbukumbu 16:8 Siku sita utakula mikate isiyotiwa chachu; na siku ya saba na uwe mkutano mtukufu kwa Bwana, Mungu wako, usifanye kazi yo yote.
Huo mkutano mtukufu ndio kusanyiko la makini.
Hekalu la kwanza pia lilipomalizika liliwekwa wakfu katika siku hii ya kusanyiko la makini
2Nyakati 7:9 Hata siku ya nane wakaita kusanyiko la makini; kwa maana walishika kuitakasa madhabahu siku saba, na sikukuu siku saba.
Sehemu nyingine mikusanyiko hii iliitishwa rasmi, kwa lengo la kujimimina kwa Mungu kuomba, kwa ajili ya maovu na majanga ambayo yanaipata nchi. (Yoeli 1:14 – 2:15). Kusanyiko hili liliitwa pia kama kusanyiko kuu.
Je! Ufunuo wake ni upi leo?
Kama vile tulivyo na mikusanyiko ya aina mbalimbali leo, mfano ya shule ya jumapili, ya semina, ya injili n.k. Vivyo hivyo hatuna budi kuwa na makusanyiko ya makini. Ambayo ni mikusanyiko ya mifungo na maombi. Ambapo tunapata muda wa kujimimina kwa undani kabisa uweponi mwa Mungu, kumtaka aingilie kati mambo yetu.
Je! unaithamini? Mungu aliyesema tusiache kukusanyika pamoja (Waebrania 10:25). Hakumaanisha tu mikusanyiko ya jumapili, lakini pia ya mifungo na maombi.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Rudi Nyumbani
Print this post