Naliupata wenyeji huu kwa mali nyingi, maana yake nini (Matendo 22:28)

Naliupata wenyeji huu kwa mali nyingi, maana yake nini (Matendo 22:28)

Jibu: Habari hii inamhusu Mtume Paulo, kipindi aliposhikwa na kufungwa akiwa Yerusalemu.. sasa ili tuelewe vizuri tuanze kusoma ule mstari wa 25

Matendo 22:25 “Hata walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paulo akamwambia yule akida aliyesimama karibu, Je! Ni halali ninyi kumpiga mtu aliye Mrumi naye hajakuhumiwa bado?

26 Yule akida aliposikia, akaenda akamwarifu yule jemadari, akisema, Unataka kufanya nini? Kwa maana mtu huyu ni Mrumi

27 Jemadari akaja, akamwuliza, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndiyo.

28 Jemadari akajibu, MIMI NALIPATA WENYEJI HUU KWA MALI NYINGI. Paulo akasema, Na mimi ni Mrumi wa kuzaliwa”.

Wenyeji unaozungumziwa hapo ni “URAIA”.. Kwahiyo hapo kiswahili kingine cha andiko hili ni hiki .. “Jemadari akajibu, MIMI NALIPATA URAIA HUU KWA MALI NYINGI”.

Zamani za kanisa la karne ya kwanza, ufalme uliokuwa na nguvu duniani, ulikuwa ni ufalme wa Rumi, na ndio uliokuwa unatawala dunia chini ya Kaisari. Hivyo kutokana na nguvu ya ufalme huo, basi hata raia wake walikuwa na nguvu, na heshima.

Raia wa kirumi (yaani Mrumi) alikuwa hawezi kuadhibiwa bila kushitakiwa, na haki zake zilikuwa zinalindwa sana kuliko raia wa Taifa lingine lolote duniani,..ilikuwa ni kosa kubwa kumhukumu Mrumi kabla ya kumsikiliza.

Sasa hapa Paulo alikuwa ni Mrumi kwa kuzaliwa lakini kwaasili ni Mwebrania (yaani muisraeli), na hapa alikuwa amevunjiwa haki yake kama raia wa kirumi, na hivyo akida pamoja na jemedari wakaogopa, kwasababu ni kosa kumhukumu Mrumi kabla ya kumpandisha kizimbani na kumsikiliza.

Sasa swali la Msingi kwanini, Jemedari aseme Uraia wake kaupata kwa mali nyingi?

Zamani ili uwe Raia wa kirumi ni aidha uwe mzawa (yaani umezaliwa katika Taifa la Rumi) au Umeununua uraia.

Sasa kitendo cha kuununua Uraia hakikuwa rasmi, bali kilikuwa ni kwa njia ya rushwa, na waliopata uraia huo waliupata wakati wa sense, ambapo majina yako yaliongezwa katika orodha ya warumi kinyume cha sheria, baada ya kulipa pesa nyingi,

Na hapa huyu Jemedari aliyeitwa Klaudio Lisia (Matendo 23:26) anaonekana kumwambia Paulo kuwa Uraia wake “Aliununua” maana yake kwa asili hakuwa mrumi, bali alikuwa kuwa mtu wa Taifa lingine, huenda Ugiriki, kwasababu hilo jina la Pili la LISIA ni jina la kigiriki, lakini Paulo yeye alikuwa ni Mrumi kwa kuzaliwa na si kwa kununua uraia.

Upo uraia mwingine ambao ni wa Mbinguni…huo haupatikani kwa fedha, wala mtu haupati kwa rushwa bali bali kwa kuzaliwa mara ya pili.

Yohana 3:3 “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.

4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.”

Je umeupata uraia huu wa mbinguni kwa kuzaliwa mara ya pili?.. kama bado ni nini kinachokusubirisha??

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments