Je kuna haja gani ya kuamini biblia iliyoandikwa na watu?

Je kuna haja gani ya kuamini biblia iliyoandikwa na watu?

Swali: Biblia imeandikwa na watu, (kama Paulo, Petro, Musa, Daudi na wengineo) je tutaamini vipi kitu kilichoandikwa na wanadamu kuwa ni kweli,? vipi kama wametoa tu kwenye akili zao, kwanini tukiamini kitabu cha namna hiyo, chenye mikono ya wanadamu?

Jibu: Kabla ya kujibu swali hili, tusome kwanza maandiko yafuatayo…

Yohana 14:11 “Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, SADIKINI KWA SABABU YA KAZI ZENYEWE”

Hapa Bwana YESU anatoa njia za sisi kumwamini yeye, kwamba kama hatutamwamini kwa yeye kutuambia kwa mdomo wake mwenyewe, basi tumwamini kupitia zile kazi anazozifanya ambazo ni ishara na miujiza.

Hiyo hakika ni hekima kuu sana!… kwamba kama sisi ni kazi sana kumwamini yeye kwa maneno ya kinywa chake, basi tuzipime zile kazi anazozifanya ikiwa ni halisi na za kweli, basi tumwamini kwahizo pasipo hata maneno yake.

Vile vile na hata kuhusiana na waandishi wa Biblia, kama hatuwaamini kuwa wameandika mambo waliyovuviwa na MUNGU, basi kupitia matokeo ya kazi hizo, (jinsi yanavyobadilisha watu wengi leo, na kuponya watu wengi) basi tuamini.

Labda hujaelewa vizuri, tafakari tena mfano huu.

Umeletewa kitabu cha Fizikia, ambacho kimsingi kimeandikwa na watu wengi, ambapo ndani ya kitabu hiko waandishi wameeleza kanuni/fomula za kuunda ndege inayoruka juu sana, sasa kitabu kama kitabu kinakuambia kuwa kwa kupitia kanuni hii inawezekana kutengeneza chombo na kuruka juu mawinguni..(hayo ni maneno ya waandishi wa kitabu, ambao ni wanasayansi).

Sasa kwa maneno yao hivyo tu, hatuwezi kuamini, au tuseme ni ngumu kuamini!, kwamba huwenda yakawa ni maneno ya kutunga tu, au ya watu waliorukwa na akili… lakini anapotokea mtu na kutengeneza chombo kinachoruka angani kupitia kanuni za wanasayansi hao walizoziandika kwenye kitabu chao hiko, basi ndipo tunaweza kuamini kuwa waliyokuwa wanayasema ndani ya kitabu ni kweli, kwani tumeona kabisa ndege ikiruka kupitia kanuni walizoziandika kupitia kile kitabu.

Vile vile tunaweza tusiyaamini maneno ya Paulo, au ya Petro au ya Daudi au ya Mtume mwingine yoyote ndani ya biblia, lakini tutakapoyaona yametumiwa na wengine na kuleta matokeo kama waliyoyasema ndani ya kitabu cha biblia tutawaamini.

Sasa maneno yao (Paulo, Petro, Daudi na wengineo) yamewekwa katika matendo na majaribio ya mamilioni ya watu, na yameleta matokeo yale yale waliyoyasema hao Mitume ndani ya biblia, hicho ndicho kinachotufanya tuwaamini kuwa waliyokuwa waliyoyaandika ni kweli, na uzuri ni kwamba hata mimi na wewe tumepewa nafasi ya kuyatafiti maneno hayo kama ni kweli au uongo..

Walisema na kuandika ndani ya kitabu (biblia) kuwa kwa jina la YESU pepo wanatoka, leo tumejaribu na tumeona ni kweli, na maelfu ya watu wamejaribu na kuona ni kweli, hivyo basi maneno yao ndani ya biblia ni kweli!.

Mitume waliandika kuwa Aminiye na kubatizwa atapokea zawadi ya Roho Mtakatifu (Matendo 2:38), jambo hilo tumelihakiki wenyewe kuwa ni kweli, na wewe unaweza kulihakiki kuwa ni kweli, sasa kuna sababu gani ya kutoaiamini biblia, ijapokuwa imeandikwa na watu?.. kama watu wanaishuhudia kweli, basi kinachofuatwa ni ile kweli wanaousema na si watu.

Ukiona mtu anasema mwanasayansi aliyetoa kanuni ya kuunda ndege ni mwongo na katunga, na huku ndege zinaonekana zikiruka, basi mtu huyo anayepinga huwenda anamatatizo ya afya ya akili, na anahitaji msaada, vile vile ukiona mtu anapinga elimu inayotolewa na mitume wa kwenye biblia na huku matokeo ya elimu hiyo yanaonekana wazi kwa macho, basi mtu huyo huwenda anayo matatizo pia ya afya ya akili za rohoni au hata ya mwilini, anahitaji msaada.

2Petro 1:20 “Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.

21  Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, WAKIONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU”.

Biblia si kitabu kilichoandikwa kwa fikra za watu, kama ulikuwa unafikiri hivyo, basi leo hii anza kubadili mtazamo wako na fikra zao, anza kuisoma Biblia kwa mtazamo mwingine na utamwona MUNGU na si Mtu, kwa msaada wa njia bora ya kusoma biblia tutafute inbox.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments