Swali: Nyaraka za Paulo tunaona ni barua kwenda kwa makanisa yaliyokuwepo wakati huo, kama Korintho, Efeso, Kolosai na Galatia na nyingine kwenda kwa watu waliokuwepo wakati huo, kama Timotheo, Tito na Filemoni sasa iweje nyaraka hizo zituhusu na sisi na hata ziwe ni neno la MUNGU?, na kuzitumia hizo kufundishia sasa?
Jibu: Swali zuri lakini ili tuweze kupata majibu yaliyojitosheleza, hetu tutafakari mifano ya kawaida iliyopo,
Alikuwepo mwanasayansi mmoja wa kijerumani maarufu ambaye sasa ni marehemu ajulikanaye kama Albert Einstein (Mgunduzi wa kanuni ya kutengeneza bomu la Nyuklia), huyu wakati wa vita vya pili vya dunia alimwandikia waraka Raisi wa Marekani aitwaye Roosevelt, kwamba atengeneze silaha ya Nyuklia, kabla Adolf Hitler hajaitengeneza, na katika waraka huo alimpa pia hiyo fomula/kanuni ya kutengeneza silaha hiyo. (Waraka huo uliandikwa mwaka Agosti 2,1939).
Na matokeo ya waraka huo ni Raisi Roosevelt kuunda bomu la Nyuklia, na kwenda kulifanyia majaribio katika miji miwili ya nchi ya Japani (Mji wa Heroshima na Nagasaki).
Lakini ajabu ni kwamba baada ya wakati huo, sehemu za waraka huo zilizobeba kanuni za utengenezaji wa nyuklia zilivuja na kufikia mataifa mengine, na mataifa hayo kama Urusi hayakulaza damu bali nayo pia yakaunda mabomu ya nyuklia yenye kanuni ile ile, zilizokuwepo ndani ya ule waraka.
Na cha ajabu zaidi ni kwamba miaka mingine mingi mbele mataifa mengine kama Ufaransa, Pakistani,India, na mengine machache yakaichukua kanuni hiyo hiyo ya kuunda bomu la Nyuklia na kutengeneza mabomu yao,
Na cha kushangaza zaidi na zaidi ni kwamba mataifa mengine mengi leo yanafanya jitihada kuunda mabomu yao kupita kanuni ile ile ya mwanasayansi huyo Albert Einstein aliyetokea miaka mingi huko nyuma kupitia waraka wake aliomwandikia Raisi wa Marekani.
Sasa swali la kujiuliza, ni hili; kulikuwa kuna haja gani ya Mataifa kama Urusi, Ufaransa, na mengineyo kufuatilia waraka Einstein aliomwandikia Raisi Roosevelt na hata kuzitumia kanuni/fomula alizoziandika ndani yake kutengeneza mabomu yao??..
Tulitegemea waraka wa Einstein kwenda kwa Raisi huyo, uishe matumizi baada ya kusomwa na kutumika na Raisi huyo wa Marekani, lakini ajabu ni kwamba mpaka sasa una matokeo katika ulimwengu wetu, ingawa uliandikwa miaka mingi iliyopita.
Kwahiyo Utaona kwamba sababu pekee ya mataifa mpaka leo hii kuitumia kanuni ya mwanasayansi huyo aliyetokea miaka mingi huko nyuma ni kwasababu alichokigundua Albert Einstein ni kitu cha Kweli chenye manufaa na tija si tu kwa wakati wake tu, au Taifa lake tu bali hata kwa mataifa mengine na kwa vizazi vingi vijavyo.
Na ni hivyo hivyo Nyaraka za Mtume Paulo na za Mitume wengine… kwa jicho la nje zitaonekana kama zimeandikwa kwaajili ya makanisa yale ya wakati ule, au kwaajili ya watu wa wakati ule, lakini kwa jicho la rohoni ni ujumbe kwetu zaidi hata ya watu wa wakati ule.
Kwasababu yaliyoandikwa katika nyaraka za Mitume wa kwenye Biblia ni maneno ya kweli yanayoishi katika vizazi vyote, na tena kwa jinsi muda unavyozidi kwenda ndivyo yanavyohitajika zaidi kwasababu yaliyokuwa yanatendeka zamani, sasa hivi yamezidi mara nyingi sana.
Vita vya kiroho walivyokuwa wanapigana watu wa kanisa la Korintho, Galatia, na mengineyo nyakati hizo ndizo tunazopambana sasa, tena wakati huu zimezidi zaidi, kwahiyo tunahitaji fomula na kanuni za wanasayansi wetu wa kiroho (Mitume na manabii wa kwenye Biblia) kutengeneza silaha zetu za kiroho sasa, na kupambana hivi vita mpaka tushinde.
Lakini tukibaki na kusema zile nyaraka zilikuwa ni za wakorintho tu peke yao na wagalatia tu peke yao, na kwamba sisi hazituhusu tutamalizwa vizuri na shetani, ni sawa na Taifa la Urusi liseme ule waraka wa Einstein aliomwandikia Raisi wa Marekani, kuhusu utengenezaji wa Nyuklia uliwahusu Wamarekani peke yao, wangekuwa na akili hiyo, leo wangeisha, au wangetawaliwa!.
Na sisi ni lazima tuiamini Biblia, kuwa ni Neno la MUNGU linaloishi kwa nyakati zote na vizazi vyote, hakuna wakati litaisha matumizi, au litapitwa na wakati, Mafunuo yaliyokuwemo ndani ya Biblia yana nguvu na Uwezo, kwani waliofunuliwa wamefunuliwa kwa uweza wa Roho Mtakatifu na si kwa akili zao.
Mwisho; Je umempokea YESU kwelikweli au kidini?.. kama maisha unayoishi ni ya uvuguvugu bado hunaye YESU, unamhitaji YESU aingie maishani mwako, unahitaji kujikana nafsi na kubeba msalaba na kumfuata YESU, Fanya mageuzi na acha kuishi maisha ya uvuguvugu, kwani tunaishi nyakati za hatari na muda umeenda sana, na parapanda inalia muda wowote, na mambo yote yatapita.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Timotheo alikuwa wapi wakati anaandikiwa nyaraka zake na mtume Paulo?
Je ni nyaraka zipi mtume Paulo aliziandikia gerezani?
NI NANI TUNAPASWA TUMWONE ZAIDI KILA TUSOMAPO BIBLIA?
Mwandishi na uchambuzi wa kitabu cha Wakorintho wa kwanza (1Wakorintho)
About the author