Mungu ana makusudi makubwa na wewe, kwanza kukuokoa, na pili kukudhihirishia wema wake wote maishani mwako. Maamuzi haya ya kumpokea Bwana Yesu ni ya busara sana ambayo utayafurahia milele yote.
Ili kuupokea wokovu basi hapo ulipo unaweza kuchukua hatua ya imani, kwa kupiga magoti, kisha utafuatisha sala hii kwa imani. Na hakika wakati huu huu utaupokea wokovu bure.
Sema maneno haya kwa sauti:
“Bwana Yesu ninaamini kuwa wewe ni mwana wa Mungu, ninaamini kuwa ulikufa kwa ajili ya dhambi zangu, ukafufuka tena, na sasa unaishi milele. Ninakiri kuwa mimi ni mwenye dhambi, nimestahili hukumu na kifo. Lakini leo ninaungama makosa yangu na dhambi zangu zote, na kuyasalimisha maisha yangu kwako. Ninaomba msamaha wako Bwana Yesu, liandike sasa jina langu katika kitabu cha uzima. Nakukaribisha moyoni mwangu, uwe na Bwana na mwokozi wangu tangu sasa. Nimeamua kukutii na kukufuata wewe sikuzote za maisha yangu. Asante Bwana Yesu kwa kunisamehe na kuniokoa. Amen”
Kwa sala hiyo fupi, tayari Bwana Yesu ameshakusamehe dhambi zako, kumbuka kusamehewa sio kumlilia Mungu sana kwa wingi wa dhambi zako ulizomtenda..Kana kwamba unamshawishi Mungu akusamehe. Hapana.
Mungu tayari alishawasemehe wanadamu kwa kifo cha Yesu Kristo pale msalabani. Hivyo ni jukumu tu la wanadamu kuukubali msamaha wa dhambi mioyoni mwao kwa kuamini Kile ambacho Mungu alikifanya Kupitia Yesu Kristo.
Ndicho ambacho Mungu alikisema hapa
Warumi 10:9-10
[9]Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. [10]Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
Kuamini kunakozungumziwa hapo ndio huko kukubali kwenyewe kazi ya Yesu aliyoifanya ya kuondoa dhambi za watu, kwa kufa kwake pale msalabani.
Ni sawa na mtu anakuja kukwambia nakupa hii almasi, ukiipokea basi umaskini wako wote umeondoka.
Sasa wewe kwa upande wako sio tena kukililia, hapana bali unawajibu tu wa kuamini kile kitu anachokupa, kwamba kinauwezo wa kuondoa umaskini..Ambapo sasa hudhuhihirishwa kwa kukipokea.
Ukishapokea sasa ndio matunda yake unayaona, kinyume chake ni kwamba bila kuamini kamwe huwezi kupokea, na umaskini utaendelea kubali kwako daima.
Ndicho Yesu alichokileta Kwetu. Ambacho ni msamaha wa dhambi. Akasema ukiamini Kuwa nimekufa kwa ajili ya dhambi zako, ili zifutwe kabisa kabisa basi utaokoka. Hivyo pale unapoamini kwa kukubali kumfanya Yesu kuwa ndio Bwana na mwokozi wako tangu huo wakati na kuendelea, na kwamba alikufa kwa ajili yako..Basi dhambi zako zinakuwa zimeondolewa kuanzia huo wakati, haijalishi zilikuwa ni nyingi Kiasi gani.
Hilo tu, ndio maana sala hiyo fupi, ikiwa umeisema kwa dhati yatosha, kukufanya wewe kuwa mwana wa Mungu. Kwasababu tayari Umemkubali Yesu kama Bwana na mwokozi wako. Hilo ni hakikisho lake.
Bwana akubariki.
Nini kinafuata? bofya hapa. >>>
Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo?
Bofya hapa kurudi kwenye mwongozo mkuu wa mafundisho ya mwongofu mpya. >>
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
About the author