MAAJABU YA AGANO LA UPENDO WA KRISTO.

MAAJABU YA AGANO LA UPENDO WA KRISTO.

Wimbo Ulio Bora 8:6-7

[6]Nitie kama muhuri moyoni mwako,  Kama muhuri juu ya mkono wako;  Kwa maana upendo una nguvu kama mauti,  Na wivu ni mkali kama ahera.  Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu.

[7]Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, Wala mito haiwezi kuuzamisha; Kama mtu angetoa badala ya upendo Mali yote ya nyumbani mwake, Angedharauliwa kabisa.

Habari hiyo inamzungumzia Bwana arusi ambaye anataka kuingia katika mahusiano ya ndani na bibi arusi wake, hivyo anaanza kwa kumwomba amkubali Kama “Muhuri” .

muhuri huwa unawakilisha umiliki halali wa kitu hicho..

Hivyo huyu Bwana arusi anamtaka bibi arusi akubali muhuri wake, katika  moyo wake na katika mkono wake…pande mbili…moyoni ikiwakilisha ndani yake ni mkononi nje, yaani upendo wa ndani na ule upendo wa nje…kumilikiwa kwa ndani lakini pia kumilikuwa kwa nje..

Na matokeo Ya kufanya hivyo ndio hapo anaendelea kueleza sifa za huo upendo akisema upendo una nguvu kama mauti…yaani Kama vile mauti isivyo pingika juu ya mtu, kwamba kufa atakufa tu, vivyo hivyo upendo wa kweli ukimnasa mtu haupingiki..atamlinda tu.

lakini pia anasema wivu wake ni mkali kama Ahera,  ni mfano huo huo, maana yake hauvumilii maovu, pale unaponajisiwa…ni lazima utatoa tu matokeo..unakula Kama moto moyoni…ndio Uliomla Bwana Yesu alipoona nyumba ya Baba yake imegeuzwa kuwa pango la wanyang’anyi akatengeneza kikoto na kuanza kuharibu kwa makusudi kazi zote za kipepo zilizokuwa zinaendelea pale hekaluni…wivu wa upendo huharibu lakini vile vilivyo viovu.

Bado anasema ‘maji mengi na mito Haviwezi kuuzima, Kama mtu angetoa badala ya upendo  Mali yote ya nyumbani mwake, Angedharauliwa kabisa’

yaani hata mtu akijaribu kuuzimisha kwa hongo za kifedha anafanya kazi bure…

Ni kufunua nini rohoni?

Nguvu ya upendo wa Kristo kwetu pale tunapoupokea vizuri..tunakuwa salama milele ndani Yake..

Lakini Hatua ya kwanza Kristo anataka kututia muhuri wake moyoni na mkononi…na muhuri huo ni Roho Mtakatifu(Waefeso 4:30), anataka udhihirisho wa Roho uonekane mioyoni mwetu, lakini pia mwilini (kwa matendo yetu).

Utakatifu wa ndani na nje.

Kuna Watu wanampokea Yesu moyoni tu, lakini lakini badiliko la nje hawana habari nalo, wanamkiri kwa vinywa vyao lakini kwa matendo yao wanamkana..

Tito 1:16

[16]Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai.

Hapo bado upendo wa kweli haijafunuliwa…lakini pale tunapodhamiria kumpokea Kristo Kwelikweli, basi nguvu ya upendo wake inatunasa na matokeo yake yanakuwa hata tufani ya namna gani ije, yeye mwenyewe anatushika, hata dunia nzima itutenge bado hatuwezi tikiswa, hata tuahidiwe utajiri na mali zote duniani, bado upendo wetu hauwezi kupungua kwa Kristo, kwasababu ni wewe mwenyewe aliyetunasa kwa agano la muhuri rohoni na mwilini.

Yesu alisema…

Warumi 8:35-39

[35]Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu. 

Bwana akubariki.

Je upo tayari leo kuokoka? Kama ni ndio basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo mwisho wa makala hii kwa msaada huo bure.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JAWA NA UPENDO UNAOTAFUTA.

USIKAWIE- KAWIE KUUFUNGUA MOYO WAKO

Maombi Maalumu ya Kuombea Ndoa.

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments