Kwanini wakristo tunasema Bwana Yesu asifiwe? Au shalom?

Kwanini wakristo tunasema Bwana Yesu asifiwe? Au shalom?

SWALI: Naomba kufahamu tunaposema Bwana Yesu asifiwe tunamaanisha nini? Na ni nani anayepaswa kuisema hiyo salamu, na kwanini wengine wanasema ‘shalom’ badala yake?


JIBU

‘Bwana Yesu asifiwe’ ni kauli inayotangaza kustahili kwa Yesu sifa kwa ile kazi njema aliyoifanya Hapa duniani.

Yesu ndiye Mtu pekee ambaye alikubali kuingia gharama ya kuacha enzi na mamlaka Mbinguni, na kuja kuishi hapa duniani kwa kusudi moja tu la kutukomboa sisi,katika dhambi zetu, akateswa na kujaribiwa sana, akafa baadaye akafufuka na hata sasa yupo hai ameketi kama mpatanishi wa sisi na Mungu,..

Kiasi kwamba kwa kupitia Yeye tunapokea msamaha wa dhambi, tunaponywa magojwa, tunamseta shetani, tunabarikiwa, tunawasiliana na Mungu moja kwa moja bila vikwazo vyovyote kwa damu yake.

Mtu Kama huyu ni lazima astahili kusifiwa..ndio maana inakuwa ni salamu ya Wakati wote BWANA YESU ASIFIWE..

Kwasababu ya nuru tuliyo ipata kwa kazi yake njema ya ukombozi.

Je ni nani anayepaswa kuisema?

Hakuna mtu anayekatazwa kuisema, lakini mtu asipojua kwanini Yesu asifiwe basi anaisema kwa unafki, Na Mungu hapendi unafiki. Kwamfano mtu ambaye hajaokoka, halafu anasema Bwana Yesu asifiwe, ni sharti ajiulize asifiwe kwa lipi wakati hakuna chochote kilichofanya na yeye katika maisha yake..

Ni sawa na mtu aliyeokoka aseme shetani asifiwe.. atasifiwa kwa jambo gani hapo wakati hakuna ushirika wowote alio nao na shetani. Lakini mganga wa kienyeji Akisema hivyo hiyo ni kweli kwasababu kuna faida amezipata Kwa shetani.

Salamu hii pia, au kauli hii, ni sahihi kutumika katika matamshi ya kiibada..mfano kwenye mahubiri, mafundisho, nyimbo, maombezi N.k. kwasababu katika Maeneo haya kazi za Yesu hudhihirishwa.

Lakini shalom Ni neno la kiyahudi linalomaanisha ‘Amani’. Ni Neno ambalo mtu yeyote anaweza kulitumia awe ameokoka au hajaokoka kwasababu ni Neno la kilugha zaidi kuliko kiimani. Ni sawasawa na sisi tunavyosema, ‘habari yako’. Mtu yeyote anaweza kutumia hilo neno. Lakini Bwana Yesu asifiwe ni Neno la kiimani ambalo anayestahili kulitamka ni mtu aliyemwamini Yesu tu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply