Sheria ya uhuru ni ipi? (Yakobo 2:12)

Sheria ya uhuru ni ipi? (Yakobo 2:12)

SWALI: Sheria ya uhuru ni ipi inayozungumziwa na mtume Yakobo kulingana na maandiko?

Yakobo 2:11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria.
12 Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.

Neno hili pia utaliona likitajwa na mtume Yakobo katika vifungu vingine vya juu.

Yakobo 1:25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.

Katika biblia zipo sheria kuu mbili

  1. Sheria ya kwanza ni sheria ya dhambi na Mauti (Warumi 8)
  2. Na sheria  ya pili ni sheria ya Roho wa uzima.

Sheria ya dhambi na mauti ndio ile ya torati, ambayo kazi yake kubwa ni kufichua uovu, kushtaki makosa, lakini haimfanyi  mtu kuwa huru, kwa mfano sheria inasema usizini, mtu atakataa kuzini, sio kwasababu hapendi uzinzi, lakini kwasababu sheria imesema tu hivyo, anaogopa adhabu atakapotenda hiyo dhambi atauawa.

Lakini sheria ya Roho wa uzima, ni sheria ya Mungu, isipokuwa hii mtu anavuviwa na Roho Mtakatifu, nguvu ya kuisha sawasawa na matwaka ya Mungu, bila shuruti Fulani, ni ya uhuru. Mfano labda sheria inasema usiue, mtu haui sio kwasababu sheria imesema, lakini kwasababu moyoni mwake hiyo nia, tamaa, au kiu ya kuua haipo, hivyo hata kama sheria isingesema hilo jambo lisingekubalika ndani yake, Hivyo mtu kama huyu tunasema ni huru na sheria, hayupo ki-sheria, sheria haimtawali  ijapokuwa sheria yenyewe ipo.

Mtu ukishaokoka, anakutana na sheria mpya ya Mungu, ambayo hiyo ni lazima ifuatwe na ishikwe, lakini inakuwa ya uhuru, sio tena ya kifungo, kwasababu Roho Mtakatifu anamsaidia huyo mtu kuuishi..

Ndio hiyo inayoitwa sheria ya uhuru, kwenye kitabu cha Yakobo.

Maana yake ni nini? Sisi kama waamini, Mungu anatarajia tuonyeshe matunda ya Imani yetu katika upendo, huruma, na matendo mema, kwasababu tunaye Roho.

Hivyo inapotokea, hayo hayaonekani, sheria itatuwajibisha, kutuhukumu, au vinginevyo hatukipokea sheria hiyo ya uhuru.. Ni sawa, na mtu aende kuua watu ovyo bila sababu yoyote,

Mtu huyu atahukumiwa, sawa tu na yule ambaye amesukumwa na sababu fulani, labda kisasi, hasira, wivu, chuki n.k.,

Hivyo sisi waamini, tulipokuwa huru na dhambi, hatupaswi kufikiri kuwa ndio tuna uhalali wa Kutenda dhambi. Kinyume chake, tujue kuwa ipo sheria yetu ya uhuru, itakayotuhukumu, kama tu vile wale wengine walivyohukumiwa kwa sheria ya dhambi na mauti (torati).

Ndicho alichokisema mtume Yakobo..

Kwa hitimisho ni kuwa sheria ya uhuru, ni sheria tunayoitimiza kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Ambayo hiyo pia itatuhukumu. Hivyo wewe kama mwamini, hakikisha wokovu wako unathibitika kwa kazi zake njema, chini ya upendo

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kama Bwana anawajua walio wake tangu asili kwanini tunahubiri injili? (Warumi 8:29)

Fahamu maana ya Warumi 7:25 je tunatumikia sheria ya dhambi?

Silaha za Nuru ni zipi? (Warumi 13:12)

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply