Hofu ya Bwana ni nini? (2Wakorintho 5:11)

Hofu ya Bwana ni nini? (2Wakorintho 5:11)

Swali: Hofu ya Bwana inayotajwa katika kitabu cha 2Wakorintho 5:11, ni hofu ya namna gani?


Jibu: Turejee..

2Wakorintho 5:11 “Basi tukiijua HOFU YA BWANA, twawavuta wanadamu; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tumedhihirishwa katika dhamiri zenu pia”.

“Hofu ya Bwana” au “Hofu ya Mungu”.. Ni hali ya kuhofia Hukumu ya Mungu ijayo..

Tukianzia mstari wa juu kidogo katika maandiko hayo tunasoma kuwa kila mtu itampasa kusimama mbele ya kiti cha hukumu na kupokea malipo ya kazi yake.

2Wakorintho 5:9 “Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye.

10 Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya”.

Na mahali pengine Biblia inasema kila atatoa habari zake mwenyewe..

Warumi 14:12 “Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu”.

Hivyo hiyo hali na kutafakari mambo yajayo, kwamba tutasimama mbele ya kiti cha hukumu, inazaa hofu, na hofu hiyo ndio ijulikanayo kama “Hofu ya Bwana” au “Hofu ya Mungu”.. Na wakati mwingine hofu hii haimpeleki mtu kuogopa hukumu ijayo baada ya kifo, bali hata akiwa hai, kwasababu pia Mungu anaweza kumhukumu mtu bado akiwa hai, kwa kuruhusu madhara yampate.

Mfano wa watu katika maandiko walioonekana kuwa na Hofu ya Mungu, ni Yule mnyang’anyi aliyeangikwa msalabani pamoja na Bwana.

Luka 3:39 “Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi.

40 Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, WEWE HUMWOGOPI HATA MUNGU, nawe u katika hukumu iyo hiyo?

41 Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa.

42 Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako”.

Na mfano wa Mtu/Watu katika maandiko waliotajwa kukosa Hofu ya Mungu kabisa ni wale watu wa Sodoma na Gomora na wenyeji wa nchi ya Gerari..

Mwanzo 20:10 “Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Umeona nini hata ukatenda jambo hili?

11 Ibrahimu akasema, Kwa sababu naliona, Yakini hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu”.

Na sisi ni lazima tuwe na “Hofu ya Mungu” siku zote, ili tuikwepe huku ya Mungu..kwani madhara ya kukosa hofu ya Mungu ni makubwa.. Tukiwa na hofu ya Mungu ndani yetu, tutajitenga na dhambi kwa namna yoyote ile.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Nyakati za Mwisho na Tumaini la Utukufu kwa Mwamini Mpya

IFANYE KAZI YA MUNGU PASIPO HOFU!

Hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.

MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.

UMEPATA UHAKIKA WA KUTOKUINGIA HUKUMUNI KATIKA SIKU ILE?

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply