WOKOVU UKIHARAKISHA USIUZUIE.

WOKOVU UKIHARAKISHA USIUZUIE.

Wokovu ni kama farasi ambaye ana uwezo wa kusafiri kwa mwendo wa kasi sana au kwa mwendo wa taratibu sana, inategemea tu, nia ya mwendeshaji.

Halikadhalika Ikiwa wewe ni mshuhudiaji,(mhubiri wa injili) ni vema kufahamu tabia hizi, mara nyingi wokovu mpaka ukamilike ndani ya mtu, yaani kukubali toba, kuamini, kikiri, kubatizwa, kujazwa Roho, huweza kuchukua muda fulani wa wastani au mrefu kidogo, ambao huusisha kushawishi, kufuatilia, kufundisha madarasa mbalimbali imani, ya ubatizo na Roho Mtakatifu, n.k. ndipo aamini na kukamilishwa.

Lakini tembea pia ukijua kuwa si wakati wote hili litakuwa hivyo…

Zipo nyakati Mungu anabadili gia, atataka kukamilisha mambo yote hata kwa siku moja tu…yaani kumwokoa, kumbatiza na leo leo kumjaza Roho…Ukiona jambo hilo kamwe usijaribu kupunguza mwendo huo..Ni Mungu kaamua kuongeza kasi ya usafiri wake.

Je hili lipo kibiblia?

Ndio…wakati fulani Paulo na Sila walikamatwa na kutupwa gerezani, wakiwa kule usiku ule tunaona walianza kumwimbia Mungu na kumsifu sana…na mara vifungo vya gereza vikafunguka..yule askari msimamizi alipoona tukio lile aliogopa sana na kutetemeka…akasema nifanye nini ili niokoke? Wakawaambia wamwamini Bwana Yesu utaokoka. Na usiku ule ule walitubu, na kubatizwa nyumba yote, na kisha wakajazwa furaha ya Roho Mtakatifu yeye na nyumba yake yote..

Yaani kitendo cha usiku mmoja…familia nzima inaokoka, inabatizwa, inapokea tunda la Roho..

Matendo ya Mitume 16:27-34

[27]Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia. 

[28]Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa. 

[29]Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila; 

[30]kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? 

[31]Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. 

[32]Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake. 

[33]Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo. 

[34]Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu. 

Kama ni mchakato, wengine humaliza hata wiki au miezi mpaka nyumba nzima kuamini na kubatizwa, ..lakini hapa ilikuwa ni masaa machache sana…tena ya usiku..

Utaona jambo kama hili lilijirudia kwa Kornelio..Petro alipoenda kwake, hata kabla hajamaliza mazungumzo yake, akidhani kuwa inahitaji madarasa marefu, inahitaji vyuo vya kuufafanua msalaba…pale pale katikati ya mazungumzo watu wakashukiwa na Roho Mtakatifu wakajazwa, wakapewa ile hatua ya mwisho kabisa ya wokovu ndipo wakaenda kubatizwa…(Matendo 10).

Mambo ambayo yamkini yangechukua madarasa ya muda na maombezi ya kuwekewa mikono ya kipindi kirefu..

 Na yule mkushi aliyekutana na Filipo gaza naye vivyo hivyo hakusubiri kwanza alike kushi, pale pale njiani alibatizwa.

Matendo ya Mitume 8:36-39

[36]Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? 

[37]Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.] 

[38]Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. 

[39]Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi. 

Vivyo hivyo, fahamu kuwa kuna nyakati Mungu anaisukuma mioyo ya watu kwa nguvu sana..tena sana kiasi kwamba mioyo yao hufunguka na kutamani kukamilishwa katika yote…

Ukiona hivyo, msaidie haraka, usifikiri kwamba inahitaji maarifa mengi ili mtu kuokolewa…bali moyo uliowazi..hilo tu..

Pengine wewe ni kiongozi..unaona mtu ameamini…usingoje ratiba za mwisho wa mwaka za ubatizo kanisa kwako…ndipo ambatize huyo mtu, angalia tu mwitikio wake…Ndio lipo pia kundi lingine ambalo litahitaji mafundisho kwanza…kutokana na viwango vyao vya upokeaji, ila usilisahau hili pia.

Jifunze kwenda na kasi zote za injili.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Uinjilisti kama agizo kuu la Bwana.

NI KIPI KINAKULEWESHA?

Biblia inaposema watu wakali hushika mali sikuzote, ina maana gani? (Mithali 11:16)

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply