MAANA YA “KUISHI” YESU ANAKOKUMAANISHA?

MAANA YA “KUISHI” YESU ANAKOKUMAANISHA?

Kuishi ni tufoauti na kuwa na uhai. Hata mti ni hai, lakini hauishi.  Kuishi ni maisha, yaani unasifa ya kuwa na  mfumo au ustaarabu Fulani ambao unatembea nao, unaweza kuchagua mahali pa kukaa, unafanya kazi, unapumzika, unajenga, unapanda, unajichagulia burudani  mfano miziki, michezo, vyakula, unafanya ibada, unauza, unanunua.. mambo kama hayo kiumbe kikitenda tunasema kinaishi.

Lakini kuwa kifungoni, ndani ya gereza huoni jua wala mwezi siku zako zote uwapo duniani, hatuwezi kusema unaishi, tunasema wewe upo hai, lakini hauishi.. Au unapokaa kwenye kitanda cha wagonjwa mauti-uti, umepooza, huwezi kuongea wala kutembea, umekata kauli, kwa sikuzote uwapo duniani, hayo si maisha ijapokuwa upo hai.

Sasa kuna maneno Yesu aliyasema, ambayo si wengi hujaelewa kwa undani na upana.. Tusome;

Yohana 11:25-26

25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?

Hii kauli ukiisoma vizuri, unaweza ukasema inajichanganya, Embu tafakari, jambo la kwanza Yesu anasema, tukimwamini tukifa tutakuwa tunaishi, lakini pia tukiwa hai na kuamini hatutakufa kabisa hata milele.

Je! Sisi tuliomwamini hatufi?

Jibu ni Ndio hatufi kabisa, bali tunahamishwa makao.  Hicho kinachoitwa kifo, ni macho ya wanadamu yanaona hivyo, lakini sisi tunakuwa kama tumefumba macho, kisha tukafumbua na kujikuta katika ulimwengu mwingine kabisa, Ndio maana lugha ambayo hutumika kueleza hali hiyo kwa watakatifu ni  kulala (Matendo 7:54-60, 1Kor 15:51-58, Yohana 11:11-19)

Sisi tuliomwamini Yesu hatutaona kitu kinachoitwa kaburi, wala hatutajikuta kwenye gereza Fulani , bali kwenye ulimwengu mwingine mzuri sana uitwao pepo, sio tukiwa hai, bali tukiwa tunaishi kabisa huru.

Maana yake, tunaendeleza maisha, ikiwa kuna kutembea, huku na huko au kushughulika kwa vitu vya kimbingu, kufanya hivi, kufanya vile..Tutakuwa tunayafanya.  Hayo ndio maisha anayosema mtu akimwamini yeye, ajapokufa (lala), atakuwa anaishi.. Si atakuwa na uhai

Tutakaa huko pepo, kwa kipindi chote, ambacho tunamsubiria Yesu, kulikamilisha kusudi la watakatifu wote, kisha baadaye,(mwisho ukifika), atakuja mwenyewe kuwachukua walio hai Pamoja na miili yetu tuliyoiacha duniani, na sote kwa Pamoja tutaanza ziara mpya ya kuelekea mbingu ya tatu. Makao yetu ya milele yalipo  (2Wakorintho 12:2-4)

Lakini waovu wanapokufa, wenyewe watajiona kwanza wakiingia makaburini, kisha wakishuka kuzimu, Uhai wao ukitunzwa  kwenye vifungo vya giza wasijue chochote, wala wasitende kazi yoyote, mpaka siku ya hukumu itakapofika, ambapo watatolewa huko kisha watasimama kwenye kiti cha enzi cheupe cha mwana-kondoo kwa ajili ya hukumu, (Ufunuo 20) baada ya kuhukumiwa ndipo watakapotupwa kwenye ziwa la moto, na kuangamia milele.

Sasa wakiwa huko kuzimu, ambapo kwa jina lingine kunaitwa Jehanamu, ni mahali pa shida, dhiki nyingi na mateso yasiyoelezeka, huko hakuna maisha, ni mateso tu vifungoni.

Hivyo ndugu, unapomwamini Yesu ipo faida kubwa zaidi ya unavyofikiri, unapokea MAISHA YA MILELE, Tangu ukiwa hapa duniani, ndani yako hakuna kitu kinachoitwa kifo, wala hutakihisi hata kidogo. Kwanini leo usimkaribishe maishani mwako? Ikiwa upo tayari basi wasiliana nasi kwa namba hizi kwa ajili ya mwongozo wa sala ya Toba, bure.

Au sema sala hii kwa Imani, na Moja kwa moja Yesu ataingia moyoni mwako.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

AINA ZA FARAJA BWANA AZIACHILIAZO KWA WATUMISHI WAKE.

TAFUTA UTAKASO WA SEHEMU KUU NNE ZA MWILI WAKO.

ASIYEMPENDA BWANA NA AWE AMELAANIWA.

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply