Swali: Turejee…
Jibu: Zaburi 1:5 “Kwa hiyo wasio haki HAWATASIMAMA hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki”.
Andiko hili halimaanishi kwamba wasio haki (yaani watu waovu) hawatasimamishwa siku ya hukumu, La! haimaanishi hivyo, bali kinyume chake inamaanisha “watasimamishwa” lakini hawataweza kujitetea wala kushinda hukumu.
Neno “kusimama” linamaanisha “kushinda au kufanikiwa”… kwahiyo Wasio haki wote watahukumiwa, na sehemu nyingine nyingi katika maandiko zinathibitisha hilo..
2Petro 2:9 “basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, NA KUWAWEKA WASIO HAKI KATIKA HALI YA ADHABU HATA SIKU YA HUKUMU; 10 na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu. na kudharau mamlaka”.
2Petro 2:9 “basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, NA KUWAWEKA WASIO HAKI KATIKA HALI YA ADHABU HATA SIKU YA HUKUMU;
10 na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu. na kudharau mamlaka”.
Ni njia moja tu mtu anaweza kuitumia kuepuka hukumu ya MUNGU, nayo ni Kumwamini Bwana YESU KRISTO na kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, na kubatizwa kwa maji na kwa Roho Mtakatifu (Marko 16:16).
Yohana 5:24 “Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; WALA HAINGII HUKUMUNI, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani”.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Ni kwa namna gani YESU KRISTO atawahukumu walio hai na waliokufa?
Je biblia inajichanganya kwa habari ya hukumu ya Mungu (Yohana 12:47 na Yohana 5:22, 27).
Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.
Nini maana ya Hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma?
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ