SWALI: Nini maana ya “hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma”?(Yakobo 2:13)
Yakobo 2:13 Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.
JIBU: Ukianzia kusoma tokea ule mistari wa kwanza utaona Yakobo, anajaribu kulionya kanisa juu ya Upendo, yaani kufanya mambo bila upendeleo, akatolea mfano wa waaminio wawili, mmoja Tajiri mwingine maskini, halafu, ikatokea kanisa limstahi yule Tajiri kwa kumpa heshima kubwa ya viti vya mbele, na yule maskini likamweka sehemu mbaya, Yakobo anahoji anasema; Kanisa halioni kama litakuwa linahukumu vibaya?
Ndipo hapo sasa akaja kusema mbeleni, kuwa hukumu huwa haina huruma kwake yeye asiye na huruma.. Ikiwa na maana kuwa, mfano wewe ukampiga mwenzako mpaka akafa bila kumuhurumia, usitegemee kuwa sheria itakusamehe kwa kosa hilo? Haiwezi kukuhurumia, hata kama utaomba msamaha vipi, kinyume chake ni lazima itakuwajibisha kulingana na kosa ulilolifanya..
Vivyo hivyo, mbele za Mungu, ikiwa hatutawahurumia wengine naye Mungu hatatuhurumia sisi, ikiwa tutawependelea wengine naye Mungu atawapendelea wengine badala yetu sisi siku ile itakapofika..
Bwana Yesu alisema katika
Luka 6:36 “Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma. 37 Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa. 38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa”.
Luka 6:36 “Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
37 Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa.
38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa”.
Unaona, tukiwa na huruma, maana yake ni kuwa hukumu haiwezi kuwa na nguvu juu yetu. Ndipo linapotimia hili neno “Huruma hujitukuza juu ya hukumu”.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
BASI, IWENI NA HURUMA, KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA
Biblia inamaanisha nini inaposema “Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake”?
Kwanini Paulo, alihukumu wakati hukumu hairuhusiwi?
NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?
Rudi nyumbani
Print this post
Amina mtumishi!
Amen