Swali: Je mtu akifanya dhambi katikati ya mfungo, mfano dhambi ya uzinzi, je ule mfungo unakuwa umeharibika?
Jibu: Awali ya yote ni vizuri kufahamu kuwa kufunga ni kitendo cha kuuyatiisha chini mapenzi ya mwili na kuruhusu mapenzi ya roho yaje juu, kwasababu roho siku zote hushindana na mwili..
Wagalatia 5:16 “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka”
Sasa unapokula chakula katikati ya mfungo, huo mfungo unakuwa umeharibika, kwasababu unakuwa umeyaruhusu mapenzi ya mwili, hali kadhalika unapofanya dhambi kama ya uzinzi katikati ya mfungo, pia mfungo huo mfungo unakuwa umeharibika kwasababu uzinzi ni dhambi inayohusisha mwili kwa asilimia zote.
1Wakorintho 6:18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe”.
Kwahiyo mtu anayefanya zinaa anakuwa ameuharibu mfungo wake, na hivyo anapaswa atubu kwa kumaanisha kuacha hiyo dhambi kisha kwa uongozo wa Roho Mtakatifu apange mfungo mwingine.
Kwa urefu kuhusiana na njia bora ya kufunga, fungua hapa >>>NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
About the author