Kilio kibiblia ni mafadhaiko, machozi, au maonezi yanayoendelea kwa muda mrefu, bila kuchukuliwa hatua, au kupatiwa utatuzi stahiki, Lakini sio tu machozi bali pia shangwe ovu..zinazoendelezwa kwa muda mrefu mbele za Mungu bila kuachwa nazo pia huitwa vilio.
Sasa Makosa kama haya,(ambayo huzaa vilio) ni tofauti na makosa mengine, kwasababu haya hujilimbikiza mpaka kuzama moyoni mwa Mungu, Na adhabu zake huwa ni nzito sana, kulingana na matukio kadha wa kadha tunayoyasoma katika maandiko.
Tutakwenda kuona aina tano (5) vilio ambavyo vinatajwa katika biblia. Na yamkini pengine umekuwa mmojawapo uliyesababisha hivyo, Basi utubu mapema ili mabaya yasije kukukuta wakati wowote
Yakobo 5:1-6
[1]Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia. [2]Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo. [3]Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho. [4]Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi. [5]Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo. [6]Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi.
[1]Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia.
[2]Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo.
[3]Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho.
[4]Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi.
[5]Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo.
[6]Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi.
Mstari wa nne anasema. ‘Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna’
Hii ni aina ya kilio cha wafanyakazi Wote wa chini (humaanisha pia waajiriwa wote).
Ukweli Ni kwamba asilimia kubwa ya waajiri, huwadhulumu wafanyakazi wao mishahara au wanawatumikisha kupita kiasi na kuwapa mishahara midogo, Lengo ni ili wajilimbikizie mali, kwa manufaa yao wenyewe…
Sasa hilo ni jambo baya sana, kwasababu huku chini Mungu anasikia kilio chao hata kama hawasemi au hawaoni…mwisho wake utakuwa mbaya, hizo mali zitakutafuna kama yule tajiri wa Lazaro.
Hakikisha kuwa yule unayemwajiri, mpe stahiki zake, si tu kwenye ngazi za mashirika au makampuni lakini pia hata nyumbani kwako ikiwa umemwajiri msaidizi wa kazi, mpalilia bustani, msafisha choo, hakikisha iliyo haki yake unampa kwa wakati ili Bwana asiharibu ulivyo navyo. Vilio vyao vina nguvu sana mbele za Mungu.
Tunaona Kaini alipomuua ndugu yake, alidhani kila kitu kimekwisha…lakini Mungu akamweleza kinachoendelea katika ulimwengu Wa roho, kuwa damu yake inamlilia..Na adhabu yake ikawa ni mbaya sana…kulaaniwa na kukataliwa na nchi.
Mwanzo 4:10-13
[10]Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. [11]Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; [12]utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani. [13]Kaini akamwambia BWANA, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
[10]Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
[11]Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
[12]utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
[13]Kaini akamwambia BWANA, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
Kamwe usiue mtu. Au kuchochea mauaji Yasiyo na hatia
Wana wa Israeli, walipokuwa Misri walitumikishwa na kuteswa na kunyanyaswa na Farao..wakamlilia Mungu, Bwana akasikia kilio chao
Kutoka 3:7-9
[7]BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; [8]nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. [9]Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.
[7]BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;
[8]nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.
[9]Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.
Matokeo yakawa ni Misri kupoteza kila kitu, ambacho walikisumbukia kwa muda mrefu, pamoja na vifo vingi. Kamwe Usimtese mtu yeyote, awe mke wako, mtoto wa kambo, mkwe, kijakazi, yatima, mjane, fukara.
Hilo usiliruhusu kwasababu Vilio vyao vikimfikia Mungu, utakuwa mashakani.
Ufunuo 6:9-10
[9]Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. [10]Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?
[9]Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.
[10]Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?
Watakatifu waliapo, ni mbaya zaidi, kuliko hata makundi mengine yote wamliliapo Mungu. Adhabu yake, Mungu huikusanya, ambayo sehemu ya hiyo inamwagwa hapa hapa duniani(Ufunuo 16:4-7), lakini pia sehemu kubwa zaidi inakuwa ni baada ya haya maisha.
Kamwe usimtese mtu wa Mungu, usimdhulumu, usimwaibishe, usiwe mwiba kwake..Kwasababu vilio vyao Mungu huvisikia kwa haraka sana.
5) Kilio (Shangwe) cha waovu.
Anasa, na matendo mabaya ambayo watu wanayafanya…wakidhani ndio maisha…kubwe hawajua ni kilio kikubwa kinachoufikia moyo wa Mungu kwa haraka, kikisema mbona huji kuteketeza? Ndivyo ilivyokuwa kwa Sodoma na Gomora.
Mwanzo 18:20-21
[20]BWANA akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana, [21]basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua.
[20]BWANA akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana,
[21]basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua.
Hii ni hatari ambayo ndio inayoendelea sasa karibu dunia nzima. Matendo ya Sodoma na Gomora (ulawiti & ufiraji), anasa, ulevi, starehe, huvuta haraka sana, hukumu za Mungu. Na kama tunavyojua hizi ni nyakati za mwisho, moja ya hizi siku hukumu ya Mungu itamwagwa Duniani.
Je! Umemwamini Yesu?
Je una uhakika kubwa Kristo akirudi Leo utakwenda naye?
Ikiwa bado hujaokoka na upo tayari kufanya hivyo sasa.. Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo mwisho wa makala hii.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Je! Yohana alimtilia shaka Bwana YESU? (Mathayo 11:3)
ENDELEZA UPONDAJI.
USHUHUDA WA MATENDO NI MKUU KULIKO WA MANENO.
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ