Maisha ya mwilini mara nyingi hubeba mafundisho ya rohoni, ndio maana Bwana Yesu alitumia sana mifano ya kidunia kuwafundisha siri za ufalme wa mbinguni.
Katika jamii ili mtu aitwe profesa au daktari(kitaaluma) anapaswa awe ni msomi wa kukaa darasani kwa muda mrefu, awe na ujuzi lakini pia na uzoefu wa tafiti nyingi..yaani kwa ufupi haiwezekani ukaitwa daktari(kitaaluma) halafu usiwe msomi wa elimu za juu.
Lakini kuna udaktari ambao mtu anaweza kupewa kwa kutunikiwa, na mara nyingi huu huja pale mtu anapotoa mchango fulani mkubwa katika jamii…mtu kama huyu anaweza kutunukiwa udaktari hata kama yale mafunzo ya ndani ya kitaaluma hana.
Sasa kiroho ni vivyo hivyo unaweza pia ukawa mkufunzi, mwenye ukomavu mkubwa, zaidi ya mababa zako wa kiroho, hata zaidi ya wachungaji wako, au maaskofu wako, au wazee wako wa kiimani, kwa namna gani?
Mstari ufuatao unatupa jibu;
Zaburi 119:99-100
[99]Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo. Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.
[99]Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote,
Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo. Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.
Ukitafakari huo mistari, utaona ni mwanafunzi anayejisifia kuwa ana akili zaidi ya waalimu wake…sio kwamba ameshahitimu, hapana bado yupo chini ya waalimu wake lakini akili zake zimewapita, bado ni kijana lakini ufahamu wake umeshawazidi wazee wake.
Imewezekanikaje?
JE anasoma sana? Au ana kiwapa cha asili tofauti na wengine? Hapana…anasema kwasababu shuhuda za Mungu ndizo anazozitafakari, lakini pia anayashika mahusia ya Mungu .
Hiyo ndio siri yake, usiku na mchana ni kufikiri juu ya “KWELI”, Yaani Neno la Mungu, na na namna ya kulifanya kuwa sehemu ya maisha yake..(kujiepusha na dhambi.)
Hiyo ndio namna inayomkomaza mtu kiroho kwa haraka sana kuliko hata maarifa mengi ambayo wengi hudhani, au mafunuo mengi, au kuhubiri kwingi, au kufundisha kwingi…
Mtu mmoja anaweza akawa na uelewa mkubwa, mwalimu mzuri, mtume mwenye ushawishi mkubwa, lakini bado asimkute mwanafunzi wake ambaye maisha yake anajitahidi kuliishi Neno la Mungu.
Hivyo ndivyo Mungu anavyowatambua wakufunzi wake (kiroho), uwezo wa “kumcha Mungu” haijalishi utapoteza sifa nyingine zote za maarifa,mafunuo, lakini akiwa na hiyo huyo amefika mbali sana.
Kwasababu Biblia inasema hakuna mwisho wa usomi, (kujua maarifa), ila mtu akizingatia kumcha Mungu na kuziishika amri zake, ni zaidi ya usomi wa vitabu vyote.
Mhubiri 12:12-13
[12]Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili. [13]Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
[12]Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili.
[13]Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa;
Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
Tuwekeze nguvu zetu zote katika kuliishi Neno na neema ya Mungu itusaidie..
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
JE! UNATAKA UITWE MSOMI NA MUNGU?
USIKWEPE CHUO CHA UTAKATIFU.
HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU.
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ