SWALI: Mara nyingi biblia inataja “shuhuda za Mungu” Je hizi shuhuda ni zipi?
Mfano katika vifungu vifuatavyo Neno hilo utaliona;
Zaburi 119:2
[2]Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote.
Zaburi 119:22
[22]Uniondolee laumu na dharau, Kwa maana nimezishika shuhuda zako.
Zaburi 119: 24
[24]Shuhuda zako nazo ndizo furaha yangu, Na washauri wangu.
Zaburi 119:99
[99]Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo.
Soma pia…Zab 119:119, 144, 132:12
Hizi shuhuda ni zipi?
Shuhuda ni neno linalozaa ushuhuda au kushuhudia.
Ni kitendo cha kuthibitisha ukweli wa jambo.
Kwamfano nikisema yule “mtu ni mkarimu”. Hapo nimemshuhudia kwasababu nimeona kitu hicho ndani yake, aidha amenitendea mimi ukarimu au kamtendea mwingine..
Tofauti na kama angejisemea mwenyewe..
Hivyo Mungu naye ana vitu amevihakiki kuwa ni kweli, na hizo ndizo zinazoitwa shuhuda zake..
Mpaka jambo Mungu amelihakiki mwenyewe ni kutuhakikishia kuwa hatupotei tukilifuata, tofauti na kama tungeshuhudiwa na wanadamu…kwasababu shuhuda za wanadamu zina udanganyifu mwingi nyuma yake.
Yesu Kristo ni mwana wa Mungu na ndiye uzima wetu.
1 Yohana 5:7-12
[7]Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. 9… Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe. [10]Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe. [11]Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. [12]Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.
[7]Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.
9… Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe.
[10]Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.
[11]Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.
[12]Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.
Huu ndio ushuhuda mkuu wa Mungu, na huu ndio tuliopewa tuuhubiri kwa ulimwengu pia kwamba kwa Yesu kuna ukombozi, na uzima..
Matendo ya Mitume 4:33
[33]Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote.
Sisi (tulioamini) ni wana wa Mungu Huu ni ushuhuda mwingine wa Mungu mwenyewe ndani yetu kupitia Roho wake Mtakatifu.
Warumi 8:16-17
[16]Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; [17]na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
[16]Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;
[17]na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
Si Kristo tu peke yake ni mwana wa Mungu, na sisi pia tunapomwamini tunafanyika watoto wake (Yohana 1:12 )watoto wa Mungu mfano wa Kristo.
Hivyo tunapopitia mateso kama yeye, hatupaswi kuwa na hofu au manung’uniko, kinyume chake ndio tujipige vifua vyetu kushangilia, kwani hata yule wa pekee(Yesu), aliyapitia hayo…kwasababu kama vile alivyopata mateso na alivyorithi utukufu vivyo hivyo na sisi tutarithi utukufu wake.
Mungu anataka tutembee kwa ujasiri hapa duniani, tusiishi kama yatima, tuishi tukijua kuwa tunaye Baba mbinguni anayetutazama na kujishughulisha sana na mambo yetu yote, kwasababu yeye mwenye ametuthibitisha kuwa sisi ni wana wake…Kama yeye ametuthibitisha nafsi yako kwanini ipinge? Wanadamu kwanini wapinge, ulimwengu kwanini upinge?
Hivyo kwa hitimisho ni kuwa tunaposema tumezishika shuhuda zake maana yake ni kuwa tumeamini wokovu na uzima utokao kwa Kristo Yesu, lakini pia tumekubali kuwa wana wa Mungu, yaani tukubali dhiki kwa ajili ya jina lake, tuishipo maisha ya kumpendeza yeye, lakini pia kupokea tumaini la utukufu lililo mbele yetu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
DHAMBI HAIWEZI KUKAA NA MSHAHARA WAKO.
USHUHUDA WA RICKY:
FUNGUA KINYWA CHA ROHO MTAKATIFU KIHUDUMU.
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ