Maisha ya Imani, hayafuti dhiki, hayafuti hisia za kibinadamu, haijalishi mtu atakuwa na ukomavu mkubwa kiasi gani, bado mahangaiko ya ndani na nje, zipo nyakati atakutana nayo.
Mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo, pamoja na kuwa walitumiwa na Mungu kipekee sana na neema ya Mungu kubwa kukaa juu yao. Bado walikiri kwa wazi kabisa bila maficho dhiki ziliwasonga kote kote,
2 Wakorintho 7:5
[5]Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tulidhikika kote kote; nje palikuwa na vita, ndani hofu.
Paulo anasema nje kulikuwa na vita, maana yake maadui, walioshindana naye, kuipinga imani, kutaka kumuua, kumfunga walikuwa ni wengi sana…lakini pia ndani anasema kulikuwa na hofu si nje tu,..akiwa na maana hofu ya kwenye nafsi..mfano wa hizi ni kama vile hofu za majukumu, hofu za kusalitiwa, hofu za kuvunjwa moyo, kuachwa peke yako, za kuvamiwa na wezi, mashaka ya ugenini, kushtakiwa, hofu za mwili kudhoofika, kuugua n.k. ambazo kimsingi kazi yake ni kukufanya ukate tamaa, usisonge mbele, usizae matunda.
Ndivyo ilivyo hata kwa watumishi wa Mungu wa kweli leo, mbele ya macho ya watu wanaweza kuonekana ni watu walio- mbali na mateso, lakini kwa mujibu wa kibiblia mioyoni mwao, vipo vita vingi na hofu kote kote…
Sasa swali ni je! Wanaweza kuishi na kuendelea na imani au huduma bila kukata tamaa wakiwa katika viwango vilevile ilihali nje vita ndani hofu?
Jibu ni kuwa Bwana..huwatumia faraja kwa njia mbalimbali, na faraja hizo ni kama zifuatazo;
Paulo katika dhiki zake anasema;..Mungu, mwenye kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuja kwake Tito.
2 Wakorintho 7:5-7
[5]Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tulidhikika kote kote; nje palikuwa na vita, ndani hofu. [6]Lakini Mungu, mwenye kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuja kwake Tito. [7]Wala si kwa kuja kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu, akituarifuhabari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidii yenu kwa ajili yangu, hata nikazidi kufurahi.
[6]Lakini Mungu, mwenye kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuja kwake Tito.
[7]Wala si kwa kuja kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu, akituarifuhabari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidii yenu kwa ajili yangu, hata nikazidi kufurahi.
Ni ukweli usiopingika zipo nyakati ambazo unajihisi kama kuishiwa nguvu ya kuendelea aidha na wokovu au huduma, kwasababu ya hali fulani ngumu zinazokuzunguka..
Majira kama haya, Mungu hufanya njia, habari njema za faraja zinaweza kukufikia na kukutia nguvu na hatimaye kuendelea mbele kwa hamasa mpya.
Kwamfano Paulo alikuwa katika nyakati hizo mbaya, akiona kama taabu yake kwa Mungu ni bure, hakuna matunda, lakini ghafla analetewa taarifa na Tito ya wanafunzi wake huko Korintho wamebadilika, wamesimama imara zaidi sana wana shauku naye. Hilo lilimtia nguvu tena hata kujiona tena hayupo katika dhiki.
Kwamfano unaweza ukawa unafanya huduma kwa muda mrefu, na pengine huoni matokeo uliyoyategemea, lakini ghafla unakutana na mtu anakuambia nimebadilishwa sana na huduma yako au mafundisho yako. Wakati ule unafanya maombezi nilipona ile ugonjwa, ulipokuwa unahubiri niliguswa moyoni na sasa nimeokoka.
Hiyo ni faraja kubwa sana, na kama ulikuwa umelegea unaamka tena unasema…oh! Kumbe Bwana yupo pamoja nami.
Nyakati za uzito, nyakati za dhiki, Bwana huachilia mafunuo kwa njia mbalimbali ili kukufariji katika wokovu wako au huduma yako aidha anaweza kutumia ndoto au maono, au Neno, au hata fundisho fulani kama hili unalolisoma sasa…
Paulo alipokuwa kama mfungwa anaelekea Rumi, njiani Meli ilipata shida mpaka wakakata tamaa ya kuishi..lakini Mungu alimtokea na kumtia nguvu kwa maono.
Matendo ya Mitume 27:23-24
[23]Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami, [24]akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe.
[23]Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami,
[24]akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe.
Ni kawaida ya Mungu, kutufariji kwa njia za mafunuo, wewe ni mchungaji Bwana kukuonyesha ukichunga watu wengi, litakuwa ni jambo la kawaida, au anaweza kukupa andiko ambalo, litakupa sababu ya kusimama au kuendelea mbele. Au wakati mwingine hata kutumia mtumishi wake kukufundisha, na lile fundisho likawa ni nanga kubwa sana kwako, kutembea katika aina yoyote ya mapito.
Hii ni namna nyingine ambayo Mungu huwafariji watumishi wake, huwafungulia milango ya kifedha, aidha kusaidiwa na watu wa amani mahali fulani kimahitaji.
2 Wakorintho 11:9
[9]Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote najilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena najilinda.
Ni kawaida ya Mungu, nyakati fulani kufungua milango ya kupokea vitu kwa watu wake, lengo lake ni kukufariji, kukutia moyo ili usonge mbele katika kazi yake.
Hii ni njia nyingine ambayo Bwana huitumia sana, kutukumbusha mioyoni mwetu kuwa hizi taabu ni za kitambo, Bwana wetu ametuandalia makao na siku moja atarudi, nasi tutaishi naye milele na milele mbinguni.. katika maisha ya milele yasiyokuwa na fujo..Bwana anataka tuyakumbuke hayo, tufarijike.
1 Wathesalonike 4:16-18
[16]Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. [17]Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. [18]Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
[16]Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
[17]Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
[18]Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
Sikuzote kumbuka kuwa furaha yetu, urithi wetu, utajiri wetu upo kule ng’ambo unatungoja, hapa duniani ni wasafiri, hivyo hatutaona shida tuwapo katika dhiki za muda mfupi…Ni sawa na umeingia katika nyumba ya wageni, halafu ukaona mazingira si safi, aidha ya choo au vyumba..huwezi kulalamika na kuanza kusoneneka na kutaabika sana, kana kwamba umeingia kwenye matatizo makubwa…hapana utavumilia tu.kwasababu unajua hapo sio kwako, unapita tu utalala siku moja kesho yake utaondoka..na kurudi kwako palipo pasafi..hivyo utavumilia.
Bwana akutie nguvu. Songa mbele katika imani.
Amen.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MAANA HUYAWAZI YALIYO YA MUNGU, BALI YA WANADAMU
WALAKINI MIMI SI PEKE YANGU.
LAKINI DAUDI ALIJITIA NGUVU KATIKA BWANA, MUNGU WAKE.
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ