Tofauti na inavyodhaniwa na wengi kuwa Nabii Eliya mwenyewe ndiye atakayerudi.
Ili kuelewa vizuri juu ya jambo hilo hebu tafakari mfano ufuatao.
Ametokea kiongozi mmoja mashuhuri sana wa mambo ya kisiasa na akaleta mabadiliko makubwa sana katika taifa hilo, tuchukulie mfano Aliyekuwa Raisi wa Taifa la Tanzania, Hayati J. K. Nyerere baada ya kufa kwake, mwananchi mmoja akatabiri, Miaka ya huko mbeleni watazaliwa wakina Nyerere wengi ambao watafanya kama alivyofanya Baba wa Taifa.
Je! kwa sentensi hiyo ni sawa na kusema, Nyerere atazaliwa tena yule yule aliyefariki na kuishi na kuja kuwa Raisi tena?..Ni wazi kuwa hiyo siyo tafsiri yake, tafsiri yake ni kwamba atazaliwa au watazaliwa watu ambao watakuja kuwa mashujaa kama Nyerere
Na ndivyo ilivyo kwa unabii wa ujio wa Eliya, sio kwamba ni Eliya yule yule atazaliwa tena hapana bali atakuja mtu au watu watakaobeba huduma inayofanana na ya Eliya.
Na mtu wa Kwanza aliyeibeba huduma hiyo baada ya Eliya mwenyewe alikuwa ni Nabii Elisha na baada ya Elisha alifuata Yohana Mbatizaji..Na pia atakuwepo mwingine ambaye atakuwa na huduma kama ya Eliya nyakati za mwisho sana karibia na unyakuo.
About the author