Kwanini Bwana Yesu alisema pale msalabani naona kiu?

Kwanini Bwana Yesu alisema pale msalabani naona kiu?

JIBU: Kulikuwa na sababu kuu mbili kwanini Bwana Yesu kuzungumza maneno yale, Sababu ya kwanza ilikuwa ni ili kutimiza maandiko kama Yohana alivyoandika katika Injili yake.

Yohana 19:28 “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.”

Unaona hapo?. Ikumbukwe kuwa sehemu kuwa ya unabii aliomuhusu Yesu katika agano la kale ulitimia ndani ya wakati huu wa Mateso ya Bwana Yesu. Yaani matukio mengi sana yaliyokuwa yanatendeka na kutokea ndani ya kile kipindi kifupi cha wiki moja ya mwisho yalikuwa ni mfulilizo wa matukio ya kinabii..Jaribu kifikiria kitendo kama kile cha Yesu tu kupigwa kofi (Yohana 18:22), tayari kilishatabiriwa kitafanyika (soma Ayubu 16:18),kutemewa mate(Ayubu 30:10),kusalitiwa,vazi lake kupigwa kura, kudhihakiwa. (Zab 22)n.k…

Vivyo hivyo na kusema hili nina KIU tayari lilishatabiriwa kama tu vile yale maneno mengine kama“Eloi Eloi Lama sabakthani” yalivyotabiriwa kwahiyo alisema maneno yale ili kutimiza maandiko. Pia Ikumbukwe kuwa Bwana Yesu alikaa msalabani muda wa saa 6, licha ya mahangaisho yale ya huku na kule kubebeshwa misalaba na jana yake na pamoja usiku uliopita alikuwa akikesha katika majonzi mengi na kupigwa bila kula wala kuonja chochote, ni wazi kuwa Kiu kilimshika sana Tunasoma katika…hakuna mwanadamu wa kawaida ahangaishe hivyo halafu asisikie kiu..haiwezekani…Na unabii wa kuchoka kwake ulitabiriwa pia katika Biblia kitabu cha zaburi.

Zab 22:15 ‘Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti”

Unaona hii ni kuonyesha kuwa mwili wake alikaukiwa na maji mpaka mdomo wake ukawa mkavu kiasi cha ulimi wake kuganda kwenye taya zake.. Na ndio maana akasema nasikia kiu. Lakini pia sababu nyingine ya pili ambayo ni ya rohoni, ilikuwa ni kuonyesha kuwa sasa shughuli yote imekwisha, ni wakati sasa wa kunywa, maadui wamekwisha shindwa. Sikuzote kiu huwa kinakuja baada ya kufanya kazi Fulani ngumu ya kuchosha,au mazoezi n.k.. na ndio maana tunamwona Samsoni Siku ile wayahudi walipomfunga kamba na kumpeleka kwa wafilisti kwa usalama wa nchi yao,waliona ni heri wampoteze mtu mmoja ili taifa letu zima lisiangamie mikononi mwa wafilisti, kama tu vile wayahudi walivyomfunga Bwana Yesu na kumpeleka kwa watu wa mataifa wamsulibishe,walisema ni heri mmoja afe ili taifa zima lisiangamie mikononi mwa Warumi. Lakini tunajua ni kitu gani kilitokea pale mara baada ya vita kuisha pale Samsoni alipowapiga wale wafilisti 1000 kwa taya ile moja ya Punda, Tunasoma Samsoni aliona KIU sana.

Waamuzi 15:15 “Naye akaona mfupa mbichi wa taya ya punda, akautwaa, akapiga watu elfu kwa mfupa huo;16 Samsoni akasema, Kwa taya ya punda chungu juu ya chungu, Kwa taya ya punda nimepiga watu elfu.17 Ikawa, alipokuwa amekwisha kunena akautupa ule mfupa wa taya mkononi mwake; na mahali pale pakaitwa Ramath-lehi.18 Kisha akaona kiu sana, akamwita Bwana akasema, Wewe umetupa wokovu huu kwa mkono wa mtumishi wako; na sasa nitakufa kwa kiu, na kuanguka katika mikono ya watu wasiotahiriwa.19 Lakini Mungu akapasua mahali penye shimo palipo katika Lehi, pakatoka maji; naye alipokwisha kunywa, roho yake ikamrudia, akaburudika; kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Enhakore, napo pa katika Lehi hata hivi leo.20 Naye akawa mwamuzi wa Israeli: katika siku za Wafilisti muda wa miaka ishirini.”

Hivyo kitendo cha Yesu kutoa kauli ile ilikuwa ni ishara ya rohoni kuonyesha kuwa tayari shetani kashashindwa vita..Na ndio maana maneno yaliyofuata baada ya pale yalikuwa ni haya IMEKWISHA!.(Yohana 19:30).

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

KITENDAWILI CHA SAMSONI

KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?

BASI MUNGU AKAMUADHIMISHA SANA.

MAAGIZO YA BWANA YESU NI BORA KULIKO MAAGIZO YA DAKTARI:

MPAKA UTIMILIFU WA MATAIFA UTAKAPOWASILI.

AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments