Kwanini tunakwenda kanisani?

Kwanini tunakwenda kanisani?

Maisha ya wokovu, hayatoshi tu kusema nimeokoka, halafu basi, nitamwabudu Mungu kivyangu. Hapana, Mungu hajaagiza hivyo, na kuna hatari kubwa ya kuenenda kwa namna hiyo, tutaona ni kwanini?

Ni sawa na mwanafunzi anayesema mimi sihitaji shule, nitajisomea tu nyumbani peke yangu, nitapata elimu yote, na maarifa yote kupitia vitabu na tafiti zangu. Ukweli ni kwamba si rahisi akipate anachokitafuta, kwasababu shuleni wapo waalimu atawahitaji wamfundishe vitu asivyovijua, atauliza maswali pale ambapo hajaelewa, wapo wanafunzi wenzake atajadiliana nao, zipo nidhamu atajifunza, ipo hamasa ataipata, tofauti na akiwa peke yake, na mambo mengine kadha wa kadha, .

Vivyo hivyo na maisha ya rohoni. Wokovu ni mtu binafsi, lakini kusimama katika wokovu na kuendelea mbele na kukua kunahitaji kanisa. Mungu aliagiza hivyo akasema, tusiache kukusanyika pamoja.

Waebrania 10:25  wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia

Akasema pia, heri walio wawili kuliko mmoja, kwasababu katika wingi, kuna kutiana nguvu ya kuendelea mbele.

Mhubiri 4:9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.

10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!

11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?

12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.

Mkusanyikapo pamoja mtatiana moyo, mtaomba pamoja n.k.

Vilevile Kanisa la kwanza lilikuwa na desturi ya kukusanyika pamoja, kusikiliza fundisho la mitume, kumsifu Mungu na kumega mkate,  nyumba-nyumba kwa nyuma pamoja na Kutambuana.

Matendo 2:46  Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,

Lakini pia kusaidiana kimahitaji, Kutiana moyo  (Warumi 1:12), Kuonyana  (Wagalatia 5:13)

Lakini pia kufaidiana kwa karama za Roho Mtakatifu. Yaana kuruhusu uweza wa Mungu kutenda kazi katikati ya waamini.(Waefeso 4:11, 1Wakorintho 12) Mambo ambayo huwezi kuyapata ukiwa peke yako.

Hivyo huwezi kutenganisha maisha ya wokovu na kanisa. Kila mwamini ni lazima awe na mkusanyiko, kwa uthabiti wa maisha yake ya rohoni. Usiabudu kivyako vyako.

Amen.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WALA TUSIACHE KUKUSANYIKA PAMOJA

FUNDISHA NENO KANISANI NA NYUMBANI.

(Opens in a new browser tab)WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA; NAO WATAMWOMBOLEZE

NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?(Opens in a new browser tab(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments