Swali: Je sisi wakristo tunaruhusiwa kutumia emoji katika kufanya mawasiliano kwa njia ya kidigitali?.
Jibu: Biblia inasema…
Tito 1:15 “Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia”.
Chochote kile (hata kiwe kizuri) endapo kikitumika vibaya kinaweza kuleta madhara au kikaingiza roho ya ibilisi ndani ya mtu, hata biblia ikitumika vibaya inaweza kumharibu mtu moja kwa moja, kuliko kumjenga, ingawa biblia si kitabu kibaya..
Sasa swali “Emoji” ni nini?…na je ni sahihi kutumiwa na mkristo?.
“Emoji” ni vijitaswira vidogo vidogo vyenye maumbile ya mfano wa mtu au vitu, ambavyo vinatumika kwenye simu za mikononi au komputa, vinavyosimama badala ya maneno au hisia.
Emoji hizi zinapotumika basi mtu anayevitazama anaweza kuelewa kirahisi ujumbe wa mwandishi au hisia za mwandishi.
Lakini pia ipo hoja kuwa emoji hizi zinapotumika basi nyuma yake zinakuwa na taswira nyingine au alama nyingine za ibilisi tofauti na zile zinazoonekana pale, hivyo mkristo au mtu yeyote anapozitumia anakuwa anapokea ile roho iliyopo nyuma ya vile viemoji, au anasambaza ile roho iliyopo nyuma ya emoji zile.
Je jambo hili lina ukweli?
Kabla ya kuona ukweli wa jambo hili, hebu tutafakari kwa pamoja jambo hili lingine.
Mtu anayetumia emoji fulani na kufikiri nyuma yake kuna alama/roho ya ibilisi je! anao uhakika gani kuwa ile herufu “A” au “B” au “C” anayoitumia kuandikia meseji kwenye simu/kompyuta nyuma yake hakuna roho ya ibilisi?.
Au ana uhakika gani kuwa herufi “Y” au “X” katika simu yake, nyuma yake haina alama ya ibilisi (freemason)?…na kwamba kila anapoandika ujumbe wenye herufi hizo anakuwa anasambaza roho ya ibilisi….je una uhakika gani kuwa haiko hivyo??…Kwa maana zote ni lugha za kompyuta.
Sasa kama mtu huyu ataona emoji zina shida na herufi anazozitumia (kama A,B,C ni salama (yaani hazina hatari yoyote)….basi bado hajatafakari vizuri.
Na kama ataona herufi pamoja na emoji zote za kwenye simu zimebeba roho nyuma yake basi matumizi yote ya simu si salama kwa mkristo, wala matumizi yote ya kompyuta, kwamaana yote yamejawa na hivyo vitu (viemoji na jamii ya hivyo)…kwamaana hata nembo ya whatsapp, au tweeter au application nyingine yoyote ya simu ni jamii ya hivyo vitu..
Sasa usalama upo wapi?… au tufanye nini? kama ile alama ya kibao cha barabarani nyuma yake ni alama ya freemason?..kama zile alama za msalani zinazoelekeza kuwa huku ni jinsia ya kiume na kule ya kike nyuma yake kuna roho ya ibilisi je tufanye nini?? (je tusitumie vyoo??)… tusitumie tena barabara?..tusinunue bidhaa zenye nembo hizo masokoni???..au tufanye nini?
Je tuondoke ulimwenguni???…maana kila mahali pana hatari (hakuna usalama)…
Yohana 17:15 “Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu”.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba matumizi ya herufi, au emoji katika simu au kompyuta si dhambi wala hazimwingizii mtu roho ya ibilisi, wala hazimsambazii mtu mwingine roho…ikiwa herufi hizo au emoji hazina maudhui ya machafu ya dunia.(kama zinaa, ushabiki, mizaha, magomvi, matusi n.k)
Lakini kama mtu atakuwa ni mchafu kwa utu wa ndani (maana yake hajatakasika)..hata pasipo matumizi ya hizo emoji kwake yeye yupo hatarini kupokea roho ya ibilisi na hata kusambaza kwa wengine, lakini kwa aliye mkamilifu hawezi kupokea roho kwa hizo wala kusambaza..
Lakini pamoja na hayo yote, si sharti kutumia hizo herufi wala emoji, wala si sharti wala amri kutumia simu wala kutumia kompyuta, wala chochote chenye alama hizo alama ikiwa mtu anapenda kujizuia na matumizi ya mambo hayo (kwa sababu zake binafsi) hafanyi dhambi.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Rudi Nyumbani
About the author