SWALI: Naomba kufahamu Je! dunia Ni duara, tufe au ipo kama sahani imefunikwa na glasi kwa juu?.
JIBU: Jambo la msingi kufahamu kuhusu biblia ni kwamba, Biblia si kitabu cha kisayansi, au cha taaluma nyingine yoyote, kana kwamba unaweza vumbua elimu ya kidunia kupitia hicho. ukitegemea biblia ikupe majibu ya kitaaluma, kwa bahati mbaya unaweza usifikie lengo lako, kwasababu hakikuandikwa na Roho Mtakatifu kwa dhumuni hilo.
Biblia ni kitabu kinachoeleza sifa na tabia za Mungu, na jinsi mwanadamu anavyopaswa aoane nazo ili aweze tembea kama Mungu mwenyewe atakavyo. Ni kitabu kinachomrejesha mtu kwa muumba wake. Kwa hiyo mtaala wake ni tofauti kabisa na elimu za ulimwengu huu na mavumbuzi yake.
Ni ajabu kuona mkristo analazimishia kutafuta kanuni za kibiashara kwenye biblia. Huwezi ona huko “demand and supply” au “cash flow” au masoko ya hisa. Nenda tu darasani utafundishwa vema kanuni za uwekezaji na utafanya vema.
Vivyo hivyo na kwenye sayansi, huwezi ona aina za atomu au miamba, au mionzi, au chembe hai nyeupe za seli, au asprin huko . Nenda tu darasani utafundishwa vema yote hayo.
Ndio, hatuwezi kukataa zipo sehemu chache chache sana, zinazozungumzia elimu ya ulimwengu huu, lakini sio kwa lengo la kutufundisha kanuni zake, bali kwa lengo la kuelezea kwa undani jambo la kiroho katika tukio husika.
kwasababu biblia yenyewe inasema, hekima ya huu ilimwengu ni upumbavu mbele za Mungu, vilevile hekima ya Mungu ni upumbavu kwa ulimwengu. haviingiliani
1 Wakorintho 1:20
[20]Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu?
Kuhusu mapinduzi yote ya kiteknolojia ya wanadamu ambayo tunayaona sasa, na hata yatakayokuja huwezi yapata kwenye biblia, huwezi ona facebook, internet, vikizungumziwa kwenye biblia, sio kwamba Mungu hakuyaona au kuyajua, aliyajua sana, lakini yote hayo yamejumuishwa katika neno moja kuwa “maarifa kuongezeka” (Danieli 12:4)
Sasa tukirudi kwenye swali, ambalo linauliza je dunia ni tufe, duara au kama sahani imefunikwa na glass juu. Jibu ni lile lile hakuna taarifa za kutosha kwenye biblia zinazofafanua juu ya hilo lakini haya ni maandiko machache yanayotuambia kuhusu uhalisia wa dunia..
Isaya 40:22
[22]Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa;
Kwa andiko hili, tunaonyeshwa kuwa dunia ipo katika duara, aidha kama tufe au mpira. lakini ni mzunguko, na sio kama sahani yenye glasi juu.
Hivyo tukirudi katika sayansi, ukisoma huko ndio utaelewa vizuri zaidi kuwa dunia ni mfano wa tufe, na sisi tukiwa tumenata-nata juu yake sio ndani yake.
Lakini tukumbuke kuwa haya ni maarifa ya mwanadamu, aliyopewa na Mungu ya kutafiti, na maarifa yake yanatabia ya kuboreka na kupinduka. Lakini kwa upeo wao wameweza kuthibitisha hilo.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
MUNGU WETU, JINSI LILIVYO TUKUFU JINA LAKO DUNIANI MWOTE!
Heshima ni nini kibiblia?
NYOTA ZIPOTEAZO.
Rudi Nyumbani
Print this post