Nini maana ya kizazi cha Nne kitarudi hapa? (Mwanzo 15:16)

Nini maana ya kizazi cha Nne kitarudi hapa? (Mwanzo 15:16)

Jibu: Turejee..

Mwanzo 15:16 “Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado”.

Ili tuelewe vizuri tuanzie ule mstari wa 13..

Mwanzo 15:13 “Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.

14 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi.

15 Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.

16 NA KIZAZI CHA NNE KITARUDI HAPA, MAANA haujatimia uovu wa Waamori bado”

Katika mistari hiyo Bwana MUNGU anamwambia Abramu kuhusiana na uzao wake kwamba utaenda utumwani katika nchi isiyo yake (ambayo ni nchi ya  Misri) na utamtumikia Farao kwa muda wa miaka 400, na baada ya miaka hiyo watatoka Misri.

Sasa wakati Bwana anamwambia Abramu hayo maneno, Abramu alikuwa tayari yupo katika nchi hiyo ya ahadi, isipokuwa bado alikuwa hajaimiliki kwani uzao wake ulikuwa bado mdogo na ilikuwa ni sharti uende kwanza Misri, ukaongezeke huko na kukua,  ndio maana  Mungu anamwambia kuwa utapelekwa utumwani na kisha utarudi tena katika hiyo nchi Abramu aliyopo muda huo, na itawaondoa wenyeji wa nchi hiyo.

Sasa swali nini maana ya “Kizazi cha Nne kitarudi”..

Jibu: Zamani kizazi kimoja kilihesabika kwa miaka 100, hiko ni kizazi kimoja, kwahiyo vizazi vinne maana yake ni miaka 400.. na mwisho wa hiyo miaka 400 ndio wana wa Israeli walitoka Misri.

Lakini swali lingine ni hili: Ni kwasababu gani uzao wa Abramu ukae Misri miaka muda mwingi hivyo? (400).. Jibu tunalipata katika ule mstari wa 16 unasema..“Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado”

Kumbe ilihitajika UOVU WA WAAMORI UTIMIE!!..Na hiyo yote ni kuonyesha huruma za MUNGU, kwamba si mwepezi wa hasira, mpaka aachilie ghadhabu yake maana yake ni kwamba kiwango cha maasi kimezidi sana..kile kikombe cha ghadhabu kinakuwa kimejaa..

Kwahiyo hapo aliposema haujatimia uovu wa Waamori, maana yake kiwango cha maasi cha Waamori bado hakikuwa kingi kiasi cha kupigwa na MUNGU..  Lakini baada ya miaka 400 kile kiwango cha maovu na maasi ya Waamori, na ya watu wengine waliokuwa wanaishi Kanaani kilifika kilele, na ndipo MUNGU akaachilia hukumu yake kwa kuwaondoa.

Utazidi kuona MUNGU anawakumbusha wana wa Israeli kuwa sababu ya wenyeji wa Kanaani kuondolewa katika ile nchi, si kwasababu ya utakatifu wa wana wa Israeli, bali ni kwasababu ya maasi ya waliokuwa wanaikalia ile nchi.

Kumbukumbu 9:3 “Basi jua siku hii ya leo kuwa Bwana, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakavyowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia Bwana.

4 USISEME MOYONI MWAKO, BWANA, MUNGU WAKO, ATAKAPOKWISHA KUWASUKUMIA NJE MBELE YAKO, UKASEMA, NI KWA HAKI YANGU ALIVYONITIA BWANA NIIMILIKI NCHI HII; KWANI NI KWA AJILI YA UOVU WA MATAIFA HAYA BWANA AWAFUKUZA NJE MBELE YAKO.

5 Si kwa haki yako, wala kwa unyofu wa moyo wako, hivi uingiavyo kuimiliki nchi yao; lakini ni kwa uovu wa mataifa haya Bwana, Mungu wako, awafukuza nje mbele yako; tena apate kuliweka imara hilo neno Bwana alilowaapia baba zako Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo.

6 Basi jua ya kuwa Bwana, Mungu wako, hakupi nchi hii nzuri uimiliki kwa ajili ya haki yako, kwa maana u taifa lenye shingo ngumu”.

Umeona?… Na MUNGU ni yule yule hajabadilika, kama alivyowavumilia Waamori, na waanaki na Wahiti waliokuwa wanaikalia ile nchi ya ahadi kwa miaka 400, anatuvumilia hata sasa, lakini uvumilivu wake ni ili  sisi tutubu, kwasababu hapendi hata mmoja apotee..

Warumi 2:4  “Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?

5  Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu”.

Je umeitikia wito wa YESU?, Kama bado hujageuka na kumfuata YESU basi usipoteze muda Zaidi, huu ndio wakati, duniani imefikia kilele kabisa cha maovu na maasi, muda wowote parapanda italia na kile kikombe cha ghadhabu ya MUNGU kitamiminwa duniani.

Bwana atusaidie tusiwe miongoni mwa watakaokabiliana na mkono wa BWANA.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments