Kujihudhurisha mbele za Bwana ndio kufanyaje (Ayubu 2:1).

Kujihudhurisha mbele za Bwana ndio kufanyaje (Ayubu 2:1).

Swali: Maana ya kujihudhurisha mbele za MUNGU kulingana na Ayubu 2:1 ndio kufanyaje?.


Jibu: Turejee…

Ayubu 2:1 “Tena kulikuwa na siku hao wana wa Mungu walipokwenda KUJIHUDHURISHA mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao, ili kujihudhurisha mbele za BWANA”.

Kujihudhurisha ni kitendo cha kujisogeza mbele za MUNGU.. Neno hili msingi wake ni “kuhudhuria”… Kama vile askari anavyohudhuria kituoni kila siku, ni hivyo hivyo pia kwa hawa wana wa MUNGU kibiblia.

Sasa katika biblia kuna mahali Malaika wanatajwa kama wana wa Mungu na kuna mahali wanadamu (wanaomcha MUNGU) wanatajwa kama wana wa MUNGU. (Mfano. Wote waliomwamini Bwana YESU ni wana wa MUNGU, soma Yohana 1:12).

Makundi haya yote mawili, huwa yanajihudhurisha mbele za MUNGU kwa malengo mbalimbali kwa ufupi tuangalie jinsi yanavyojihudhurisha mbele za MUNGU.

   1. MALAIKA

Malaika wanajihudhurisha (yaani wanajisogeza) mbele za MUNGU kupeleka taarifa zetu njema, wao ni mawakili wema kwetu, wakati shetani na majeshi yake yanajihudhurisha kupeleka mashitaka juu yetu kwa Mungu, malaika watakatifu wenyewe wanapeleka taarifa njema.

Mathayo 18:10 “Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni”.

Soma pia Yuda 1:9 na Waebrania 1:14, utaona huduma za hawa Malaika watakatifu kwetu, na soma pia Ufunuo 12:10 na 1Petro 5:8 utaona huduma ya shetani juu yetu kuwa ni mashitaka tu (anajihudhurisha mbele za MUNGU kutushitaki usiku na mchana).

Na ndicho kilichotokea hapa kwa Ayubu, wakati Malaika watakatifu (wamejihudhurisha kwa MUNGU) kupeleka taarifa njema za watakatifu waliopo duniani, shetani naye alijihudhurisha kuwachafua..

Ndio maana utaona baada ya Bwana kumwuliza umetoka wapi na baada ya kumwuliza habari za Ayubu, hakuanza kumtetea Ayubu badala yake kumchochea kwa MUNGU..

Ayubu 2:3 “BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu”.

Umeona hapo hapo shetani alimchochea MUNGU ili.amwangamize Ayubu (kwani yeye ni mshitaki tu siku zote).

  2. WANADAMU.

Kama Malaika (watakatifu na walioasi) wanavyojihudhurisha mbele za MUNGU, na hali kadhalika wanadamu wanaweza kujihudhurisha mbele za MUNGU.

Njia zifuatazo ndizo mtu anaweza kuzitumia kujihudhurisha mbele za BWANA.

     1. Maombi.

Maombi binafsi ni njia ya kwanza ya mtu kujihudhurisha mbele za  MUNGU.

Mathayo 6:6 “Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”

Mtu anapoomba katika roho anajisogeza mbele za MUNGU, Zile hoja anazozipeleka zinamfikia MUNGU katika kiti chake cha enzi, sawasawa tu na Malaika wanavyomfikia MUNGU na kusema naye.

   2. Kukusanyika na wengine.

Mkusanyiko pamoja na wengine unahusisha watu zaidi ya mmoja ikiwemo kanisani.

Mathayo 18:20 “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao”.

Kama Bwana YESU yupo katikati ya mahali walipokusanyika watu wawili au zaidi, maana yake hiyo ni sehemu sahihi ya kujihudhurisha mbele za MUNGU, na sehemu hiyo ni rahisi kupokea majibu ya maombi kwani alisema wawili wenu wakipatana jambo lolote na kumwomba Baba wa mbinguni watatendewa.

Mathayo 18:19 “Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni”.

Pamoja na hayo yapo mambo ambayo pia hayatuhudhurishi mbele za Bwana sawasawa na 1 Wakorintho 8:8.

1 Wakorintho 8:8 “Lakini chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu; maana, tusipokula hatupunguziwi kitu, wala tukila, hatuongezewi kitu”

Kwa urefu kuhusiana na kitu kisichotuhudhurisha kwa Bwana fungua hapa >>>

Nini maana ya “chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu”?

Mwisho: Je wewe unajihudhurisha mbele za Bwana?..unaomba?, unakusanyika na wengine katika Bwana?..

Bwana akubariki.

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments