Je yale Makabila kumi na mawili ya Israeli, kila kabla lilikuwa na kazi gani maalumu?

Je yale Makabila kumi na mawili ya Israeli, kila kabla lilikuwa na kazi gani maalumu?

Wana kumi na mbili wa Yakobo ndio waliozaa makabila 12 ya Israeli. Majina yao ni kama yafuatavyo;

  1. Reubeni
  2. Simeoni
  3. Lawi
  4. Yuda
  5. Dani
  6. Natali
  7. Gadi
  8. Asheri
  9. Isakari
  10. Zabuloni
  11. Yusufu (Manase & Efraimu)
  12. Benyamini

Zipo kazi au majukumu ambayo makabila yote yaliwajibika kuyatekeleza mfano wa hayo ni kama kumwabudu Mungu, kuihudumia hema, ambayo baadaye ikawa hekalu, ulinzi kwa taifa (msaada wa kijeshi), kuendeleza Sheria ya Mungu kwa vizazi vyote.

Lakini pamoja na hayo, yapo majukumu ambayo yalitekelezwa Zaidi na kabila husuka kuliko mengine. ambapo mengine yaliagizwa na Mungu Moja kwa moja na mengine yalikuja Kama kipawa, walichokirimiwa . Na hatimaye yakawa ni majukumu yao.

  1. Reubeni

Reubeni alipaswa kuwa na jukumu la kiuongozi, kama mzaliwa wa kwanza, lile kusudi lote la ukuhani lingepaswa liwe la lake lakini kwasababu alizini na mke wa Baba yake, akapoteza haki ya mzaliwa wa kwanza akaondolewa nafasi hiyo (mwanzo 35:22, 49:3-4).

Ijapokuwa alishushwa daraja lake. Bado alibakia kutimiza kusudi la kiulinzi upande wa mashariki mwa Israeli kwani jeshi lake, lilikiwa na watu hodari, lakini hawakuwa viongozi wa kijeshi.

  1. Simeoni

Kabila la Simeoni nalo lingepaswa lichukue nafasi kuu katika Israeli, lakini lilishushwa chini kwasababu ya ukatili wao pamoja na Lawi, walipokwenda kuwaua wale washekemu ambao hawakustahili Kufanyiwa mauaji yale, kwa kosa la kumnajisi dada yao.(Mwanzo 34)

Hivyo kabila hili halikuwa na uongozi wowote wa kiroho katika Israeli, zaidi lilimezwa katika kabila la Yuda, kutimiza unabii wa Baba yao (Mwanzo 49:5-7),  likabakia kuwa mchango kwenye eneo la kijeshi Israeli.

  1. Lawi

Lawi lilichukua nafasi ya kikuhani, lilihudumu katika hema na Hekalu, kufanya Upatanisho kwa wana wa Israeli, kwa sadaka mbalimbali pamoja Kufundisha Torati. (Kutoka 32:26-29).

Lawi hawakuwa urithi Israeli, bali walisambazwa katika makabila yote ya Israeli, kama Simeoni, kutimiza unabii wa Baba yao juu ya hasira walioionyesha Isiyo na huruma.(Mwanzo 49:5-7)

  1. Yuda

Kabila la Yuda lilisimama Kama kabila la Kifalme, na la kikuhani halisi wa milele (2Samuel 7:16)

Ndilo lililoandaa njia ya masihi kuja Duniani,(Mwanzo  49:10).Yuda lilichukua nafasi zote za juu, kutokana na kuwa Reubeni, Lawi na Simeoni kupoteza uwezo wa kuzishika, kwa matendo yao yasiyofaa.

Kabila Hili lilikuwa pia na askari hodari wa vita, na likasimama Kama kitovu cha kiutalawa, kivita na kiibada katika Israeli. Halikadhalika Yuda ilisimama kutunza urithi wa Israeli kwa vizazi vingi baada ya kutawanywa Kwenye mataifa yote, ndio  lenyewe tu lililoweza kurudi Israeli.(Mwanzo 49:9-12)

  1. Dani

Kabila la Dani lilikuwa na jukumu la kimahakama katika Israeli, (Mwanzo 49:16-18). Lilikuwa ninasimama katika nafasi ya maamuzi. Kuhakikisha Sheria na taratibu zake zinafuatwa ipasavyo.

Lakini pia lilisimama kusaidia Israeli, mahali popote walipoweka marago na kuondoka lilihusika kukusanya vitu vyote muhimu, na kuhakikisha watu wasiojiweza wanatembea Na kundi. (Hesabu 10:25).

Pamoja na hilo lilisimama kama mashujaa wa nyuma wa jeshi la Israeli, pale linapokwenda vitani lilisimama kulinda dhidi ya wavamizi wa nyuma.

lakini baadaye lilikuja kupoteza sifa yake ya kiuamuzi, kwasababu ya kwenda kusimamisha miungu ya kigeni na kuiabudu (Waamuzi 18).

  1. Naftali

Kabila la hekima na nguvu.

Ni kabila Ambalo lilikuwa na mchango mkubwa Katika eneo la kivita. Tunaweza kuona katika kipindi cha waamuzi kabila hili kwa uongozi wa  Debora na Baraka (Waamuzi 4:6), lilimshinda Sisera.

Lakini lilisimama Kama washauri wa kiroho kwa Israeli.

Mwanzo 49:21

[21]Naftali ni ayala aliyefunguliwa; Anatoa maneno mazuri.

Katika wakati wa Kristo, eneo La wanaftali ambalo lilikuwa sehemu ya Galilaya lilidharauliwa sana, na kuonekana nyonge,(Yohana 1:46,7:52) si tu kimaendeleo lakini pia kuwa na wapagani wengi, lakini ndio mahali Ambapo palikuwa mji wa makazi ya Masihi Yesu Kristo, sawasawa na unabii alioutoa Isaya.(Mathayo 4:13-16).

  1. Gadi

Gadi lilikuwa hodari katika vita, lisilojisalimisha kirahisi kwa maadui, lilisimama Kama Walinzi wa lango la mashariki la taifa la Israeli, pembezoni mwa Reubeni.

Mwanzo 49:19

[19]Gadi, jeshi litamsonga, Lakini atawasonga wao mpaka visigino.

  1. Asheri

Ni kabila ambalo halikujikita Sana katika mchango Wa kijeshi. Bali Lilikuwa ni kabila la kibiashara Tajiri, lenye kulinda uchumi wa nchi.

Mwanzo 49:20

[20]Asheri, chakula chake kitakuwa kinono, Naye atatoa tunu za kifalme.

  1. Isakari

Ni kabila Lilipewa neema katika kutambua Nyakati na kutoa mashauri sahihi ya kufanya. lilisimama kama washauri Wa taifa.

1 Mambo ya Nyakati 12:32

[32]Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.

  1. Zabuloni

Walichangia maaskari wa vita, kwasababu walikaa katika fukwe, iliwafanya wawe hodari katika biashara na uchuuzi.

Mwanzo 49:13 Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni.

  1. Yusufu(Efraimu na Manase)

Ni kabila lililopewa nguvu, kiutawala na kijeshi  , lilitimiza kusudi la kulisimamisha taifa la Israeli, hata wakati Israeli ilipogawanyika, makao makuu ya kabila zile 10, yalikuwa Ni samaria mji wa Efraimu. (Mwanzo 49: 22-26)

  1. Benyamini

Ni kabila Lililokirimiwa watu hodari wa vita watumiao mashoto (Waamuzi 20:16), ambao walisimama vema katika vita, ijapokuwa lilikuwa dogo, lililojichanganya katika kabila la Yuda ndio kabila la kwanza kutoa mfano Israeli (Sauli), na baadaye mtume Paulo.

La kujifunza: Kuwa mdogo haimaanishi kuwa utakuwa wa mwisho. Bwana anasema walio wa mwisho Watakuwa wa kwanza na wa kwanza watakuwa wamwisho.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kwanini kabila la Dani na Efraimu hayaonekani yakiorodheshwa miongoni mwa yale makabila 12 ya Israeli katika Ufunuo 7?

KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.

Yakobo alimaanisha nini kusema ‘ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu’ Mwanzo 28:21

WEWE U MWALIMU WA ISRAELI,NA MAMBO HAYA HUYAFAHAMU?

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments