Kwanini Mwanadamu hakuumbwa kwa Neno tu kama viumbe wengine?

Kwanini Mwanadamu hakuumbwa kwa Neno tu kama viumbe wengine?

Swali: Katika kitabu cha Mwanzo tunaona viumbe vyote viliumbwa na Mungu kwa kutamka tu Neno!, lakini kwa mwanadamu haikuwa hivyo, alimwumba kwa mikono yake, je sababu ni nini?


Jibu: Turejee

Mwanzo 1:19 “Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.

 20 MUNGU AKASEMA, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.

 21 MUNGU AKAUMBA nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 

22 Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi. 

23 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.

24 MUNGU AKASEMA, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo

25 MUNGU AKAFANYA mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.”

Hapa tunasoma kwamba MUNGU AKASEMA, na kisha MUNGU AKAFANYA..  Kwahiyo kumbe MUNGU alianza kwanza kwa kusema ndipo “akafanya”..Naam hata wewe unaweza kusema “utajenga nyumba” ikawa ni kauli, na wakati utakapofika ukaanza kukusanya malighafi na kuitengeneza ile nyumba.. Kwahiyo kuna “KUSEMA” na “KUFANYA” ndiyo kanuni Bwana MUNGU aliyoenda nayo pia.

Sasa biblia haijaeleza kwa urefu alifanyaje fanyaje, kwenye huo udongo wakatokea wanyama, na viumbe..Kwamba ile kauli ya kinywa chake ndio ilienda kubadili ule udongo na kuwa Twiga, na Simba, na Tembo, au kwamba baada ya kusema alienda kuchukua udongo kwa vidole vyake na kufanya wanyama wale wote hakuna anayejua, lakini tunachojua ni kwamba wanyama walitokea ardhini kwa neno lake hilo.

Lakini tukiendelea na mstari wa 26 alipomwumba mtu, tunaona jambo jipya.. MUNGU ANASEMA, na kisha ANAUMBA kwa maelezo  marefu zaidi tofauti na ilivyokuwa kwa wanyama.

Mwanzo 1:26 “MUNGU AKASEMA, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 

27 MUNGU AKAUMBA mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba”.

Soma tena Mwanzo 2:7 na Isaya 45:12 utaona maelezo ya ziada juu ya uumbaji wa mtu.

Kwa wanyama Bwana MUNGU hakuelezea kawaumba kwa mfano wa kitu gani, na kwa sura ya kitu gani, huenda labda waliumbwa kwa mfano wa baadhi ya viumbe vya mbinguni (kwani kuna malaika mbinguni wenye uso kama wa tai, na wengine wenye uso kama wa simba na ndama, na pia mbinguni kumetajwa uwepo wa farasi, soma Ezekieli 1:10, Ufunuo 4:7 na Ufunuo 19:11), lakini hiyo yote biblia haijaeleza, ni makisio tu..

Lakini alipoumbwa mwanadamu, biblia imetoa maelezo ya wazi kabisa ziada kaumbwa kwa mfano wa MUNGU, na kwa sura  ya MUNGU, kuonyesha umaalumu wake na utofauti wake na viumbe vingine vyote.

Na kama jinsi MUNGU alivyo Mkuu mbinguni na tena anatawala mbinguni, hali kadhalika na yule aliyetengenezwa kwa mfano wake duniani, atakuwa na nguvu na utawala kama wa kwake duniani.

Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi”.

Lakini pamoja na kwamba Adamu aliumbwa ili atawale duniani, bado alimwuzia shetani nafasi yake hiyo, lakini habari njema ni kwamba YESU KRISTO alishinda na kuirejesha nafasi ya mwanadamu ya utawala..

Na wote wamwaminio Bwana YESU wanatawala naye si tu duniani, bali hata mbinguni.. kwani tumeketi naye mbinguni katika ulimwengu wa roho.

Waefeso 2:5 “ hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.

6  Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu”

Lakini ukiwa nje ya Kristo, huna mamlaka yoyote, kwani shetani ndiye anayekutawala..Mpokee leo KRISTO na upande viwango vingine vya kiroho.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments