Mistari ya biblia kuhusu sadaka

Mistari ya biblia kuhusu sadaka

Hii ni mistari ya biblia inayogusia utoaji wa sadaka wa namna mbalimbali.

Sadaka kama ibada na utiifu.

Mithali 3:9 Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. 10 Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.

Mwanzo 4: 3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. 4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; 5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.

Sadaka za kupenda:

Kutoka 25:2 Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu.

2Wakorintho 9:7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.

Kumbukumbu 16:17 Kila mtu na atoe kama awezavyo, kwa kadiri ya baraka ya Bwana, Mungu wako, alivyokupa

Kutoka 35:5 Katwaeni kati yenu matoleo kwa Bwana; mtu awaye yote aliye na moyo wa kupenda, ayalete matoleo; dhahabu na fedha na shaba;

2Nyakati 31: 5 Mara ilipotangaa amri, wana wa Israeli wakatoa kwa wingi malimbuko ya nafaka, na divai, na mafuta, na asali, na mazao yote ya mashamba; na zaka za vitu vyote wakazileta nyingi.

Sadaka za kushukuru:

Zaburi 50:14 Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye juu nadhiri zako.

Walawi 22: 29 Tena mtakapomchinjia Bwana dhabihu ya shukrani, mtamchinja ili mpate kukubaliwa. 30 Italiwa siku iyo hiyo; msisaze kitu chake hata asubuhi; mimi ndimi Bwana.

Sadaka za Zaka na malimbuko:

Malaki 3:10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

Walawi 27: 30 Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana.

Sadaka za kugharimika:

Marko 12:43 Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina; 44 maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia  vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.

Wafilipi 4:18 Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.

Luka 6:38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.

Sadaka zimpendezazo Mungu:

Yesu Kristo.

Pamoja na kuwa na sadaka za aina nyingi, lazima tufahamu, Sadaka halisi zimpendezazo Mungu. Na ya kwanza ni Yesu Kristo. Yeye alitolewa kwetu kama dhabihu kamilifu kwa ajili ya dhambi zetu. Hivyo mtu yoyote anayeitoa sadaka hii kwa Mungu basi, hukubaliwa na yeye asilimia mia. Na tunaitoa kwa kumpokea mioyoni mwetu kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu. Imefanyika bora kuliko dhabihu zote na matoleo yote.

Waebrania 10: 4 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. 5 Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari;

Sambamba na hizo, sadaka nyingine zilizobora kuliko matoleo ni pamoja na kujitoa miili yetu katika utakatifu, kutenda haki, kuonyesha fadhili na rehema, kwa Bwana.

Warumi 12:1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.

Hosea 6:6 Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.

Mika 6:6 Nimkaribie Bwana na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimkaribie na sadaka za kuteketezwa, na ndama za umri wa mwaka mmoja? 7 Je! Bwana atapendezwa na elfu za kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! Nimtoe

mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu? 8 Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!

Je! Unatoa sadaka zote hizi? Kwa Bwana?

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

FUKUZA TAI WOTE JUU YA SADAKA YAKO.

NINI NI KILICHOMFANYA IBRAHIMU AKUBALI KUMTOA MWANAWE SADAKA?

Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ya namna gani?

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments