EPUKA KUJIFANYA HUJUI.

EPUKA KUJIFANYA HUJUI.

Jina la Mwokozi YESU libarikiwe karibu tujifunze biblia.

Tabia ya kujifanya hujui na ilihali unajua ni mbaya na hatari, kwani ni sawa na kumjaribu  MUNGU.. Kipo kisa kimoja kwenye biblia cha watu waliojifanya hawajui mbele ya Bwana YESU na matokeo yake hayakuwa mazuri.

Marko 11:27 “Wakafika Yerusalemu tena; hata alipokuwa akitembea hekaluni, walimwendea wakuu wa MAKUHANI, NA WAANDISHI, NA WAZEE,

28 wakamwambia, Ni kwa mamlaka gani unatenda mambo haya? Naye ni nani aliyekupa mamlaka hii uyatende haya?

29 Yesu akawaambia, Nitawauliza neno moja, nanyi mnijibu, kisha nitawaambia ni kwa mamlaka gani nayatenda haya.

30 UBATIZO WA YOHANA ULITOKA MBINGUNI, AU KWA WANADAMU? NIJIBUNI.

31 Wakasemezana wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema, Ulitoka mbinguni, atasema, Mbona, basi, hamkumwamini?

32 Ila tukisema, Ulitoka kwa wanadamu, waliogopa watu; maana watu wote walimwona Yohana kuwa nabii halisi.

33 WAKAMJIBU YESU, WAKASEMA, HATUJUI. YESU AKAWAAMBIA, WALA MIMI SIWAAMBII NINYI NI KWA MAMLAKA GANI NAYATENDA HAYA”.

Watu hawa walikuwa wanajua kabisa ubatizo wa Yohana ulikuwa umetoka kwa MUNGU, lakini wakawa wanajifanya hawajui, na walipomwuliza Bwana YESU wakitegemea kuwa atawapa jibu la moja kwa moja, kinyume chake Bwana aliwajibu “WALA MIMI SIWAAMBII NINYI NI KWA MAMLAKA GANI NAYATENDA HAYA”.

Kwahiyo kumbe kuna maombi, au haja au dua au maulizo ambayo tunaweza kumpelekea Bwana YESU na tusipewe majibu yake!.

Ndio! kama maandiko yamesema wazi kuwa wizi ni dhambi, na tunalijua hilo hatuwezi tena kwenda tena na kumwuliza MUNGU kama kuiba ni dhambi au la! Kwani tayari tumesoma na tunajua… ukienda kumwuliza ni kumjaribu na hakuna majibu yoyote yatakayotoka..

Kama maandiko yamesema wazi kuwa uzinzi na uasherati ni dhambi,  na tunajua hilo, hatuwezi tena kwenda kurudia kumuuliza MUNGU atufunulie kwenye ndoto au tuisikie sauti yake ikisema kuwa ni dhambi…hapo itakuwa ni kumjaribu.

Kama dhamiri yako inakushuhudia kabisa kuwa hilo unalolitenda, au hiko unakokivaa au unakokishikilia ni dhambi, na maandiko yamekudhihirishia wazi, huwezi tena kwenda kumwuliza MUNGU akuhakikishie, unaweza usipate majibu yoyote, na ukaishia kusema MUNGU hasikii maombi.

Sio kwamba MUNGU hasikii maombi, ni kwamba MUNGU anataka usikie kwanza Neno lake na kulitii, lililoadikwa katika kitabu chake kitakatifu BIBLIA.

Biblia ni sauti ya MUNGU isiyo na marekebisho, na iliyo ya wazi kabisa..  ukitaka kuisikia sauti ya MUNGU ya wazi kabisa, soma Biblia, wala usiende kwa mchungaji, wala askofu, wala usisubiri uote ndoto, wewe soma Biblia tu!, utapata utamsikia MUNGU.

Mwisho acha kujifanya hujui kama kuna Jehanamu, acha kujifanya hujui kuwa kuvaa kidunia ni makosa, acha kujifanya hujui kwamba ibada za sanamu ni makosa, acha kujifanya hujui kuwa matambiko na makosa, acha kujifanya hujui kuwa kuishi na mke/mume wa mtu ni dhambi!.

Usimwulize Bwana MUNGU kama pombe unazouza ni mapenzi yake au la!, na ili hali unajua kabisa pombe ni makosa, hutapata majibu yoyote, zaidi unaweza ukaisikia sauti ya shetani kinyume chake.

Yakobo 4:17 “Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kama Kristo alizichukua dhambi zetu na kutusamehe kwanini kila siku tunatubu?.

KILA SILAHA ITAKAYOFANYIKA JUU YAKO HAITAFANIKIWA.

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA MFUNGO.

Mwandishi na uchambuzi wa kitabu cha Wathesalonike wa kwanza.

IFUATE KANUNI SAHIHI YA MUNGU

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
David Masine
David Masine
1 day ago

Nimebarikiwa sana