SAA INAKUJA NA SASA IPO.

SAA INAKUJA NA SASA IPO.

Jina la Mwokozi wa pekee YESU KRISTO libarikiwe.

Je unajua tupo katika kipindi cha UFUFUO?.. Utauliza ufufuo gani?.. Turejee maandiko yafuatayo..

Yohana 5:25 “Amin, amin, nawaambia, SAA INAKUJA, NA SASA IPO, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.

26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake”.

Hapo Bwana YESU (Mkuu wa uzima) anasema “SAA INAKUJA” na “SASA IPO”  Je unaielewa vizuri hii kauli?

Anaposema “Saa inakuja” maana yake kipindi Fulani cha mbeleni kinachokuja…. Na anaposema “sasa ipo” maana yake ni kipindi alichopo yeye.

Sasa swali alikuwa ana maana gani kusema vile?

SAA INAKUJA: Hiki ni kipindi cha mwisho wa dunia, (wakati wa unyakuo wa kanisa) ambapo wafu waliokufa katika Kristo watatoka makaburini na kuvikwa miili ya utukufu na kisha kumlaki Bwana mawinguni.

1Wathesalonike 4:13 “Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.

14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba YESU ALIKUFA AKAFUFUKA, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, MUNGU ATAWALETA PAMOJA NAYE.

15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.

16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; NAO WALIOKUFA KATIKA KRISTO WATAFUFULIWA KWANZA.

17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele”.

Hiko ni kipindi cha Ufufuo wa siku za mwisho ambacho yoyote aliyekufa hapaswi kukikosa..kwani si wote watakaofufuliwa na kwenda kwenye unyakuo.

NA SASA IPO: Hiki ni kipindi ambacho Bwana YESU alikuwepo duniani, ambapo watu walikuwa wanafufuliwa roho zao zilizokufa katika dhambi..

Kitendo cha kumwamini YESU na kutubu na kubatizwa ni sawa na kufufuka kutoka katika WAFU, utauliza kwa namna gani?..

Turejee kidogo ile habari ya mwana mpotevu ambaye alitapanya mali kwa maisha ya uasherati na alipozingatia kurudi kwa baba yake kutubu, baba yake alimtafsiri kama aliyekuwa amekufa na sasa amefufuka.

Luka 15:29 “Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu

30 lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona.

31 Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako.

32 Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako ALIKUWA AMEKUFA, NAYE AMEFUFUKA; alikuwa amepotea, naye ameonekana”.

Umeona? Si kwamba huyu kijana alikuwa amekufa kimwili, La! Bali kiroho, na alipotubu na kugeuka akahesabika kama aliyefufuka..

Je bado na wewe ni MFU na ilihali tunaishi katika SAA YA UFUFUO?.. Kumbuka usipofufuliwa sasa utu wa ndani kama huyu kijana mpotevu, hutaweza kuupata ufufuo wa siku ile ya Mwisho Bwana YESU atakaporudi, na siku hiyo imekaribia sana..

Maisha unayoishi ya dhambi ni uthibitisho wa MAUTI iliyopo ndani yako, na hiyo itaathiri hata mambo yako mengine uyafanyayo.

Fufuka leo kwa kumwamini BWANA YESU KRISTO, ili akuoshe dhambi zako kama maandiko yasemavyo..

Waefeso 5:14 “Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza.

15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;

16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.

17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana”.

Saa ya UFUFUO Ni SASA… Saa ya Ufufuo ni Sasa, Saa ya UFUFUO NI SASA!

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

 

Nini maana ya “SAA INAKUJA” na “SASA IPO” (Yohana 4:23).

YEYE AJAYE ATAKUJA WALA HATAKAWIA.

TUNAYE MWOMBEZI.

MFALME ANAKUJA.

NINI MAANA YA KUISHI KWA KUUKOMBOA WAKATI?.

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments