Wanethini ni kundi la watu ambao walitumika katika hekalu, ambao sio asili ya wayahudi. Wanatajwa sana kwenye kitabu cha Nehemia na Ezra. Maana ya neno ‘Nethini’ kwa kiyahudi linamaanisha “waliotolewa”. Wakimaanisha watu waliotelewa kuwasaidia walawi katika shughuli za hekaluni.
Hivi ni baadhi ya vifungu vinavyowataja;
Ezra 8:20 na katika Wanethini, ambao Daudi, na wakuu, walikuwa wamewaweka kwa ajili ya utumishi wa Walawi, Wanethini mia mbili na ishirini; wote wametajwa kwa majina yao.
Nehemia 7:73 Hivyo makuhani, na Walawi, na mabawabu, na waimbaji, na baadhi ya watu, na Wanethini, na Israeli wote, wakakaa mijini mwao. Hata ulipowadia mwezi wa saba, wana wa Israeli walikuwa wakikaa katika miji yao.
Soma pia, (Ezra 2:43, 2:58, 7:24)
Biblia haituonyeshi moja kwa moja asili yao ni wapi, lakini wanazuoni wengi huamini walitokea katika chimbuko la wale wagibeoni waliowadanganya Israeli wakati ule mpaka wakafanya nao maagano, Ambao Yoshua aliwapa kazi ya kupasua kuni, na kuteka maji.
Yoshua 9:27 Siku iyo hiyo Yoshua akawafanya kuwa ni wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano, na kwa ajili ya madhabahu ya Bwana, hata siku hii ya leo, katika mahali hapo atakapopachagua
Mbali na hawa wagibeoni wengine wanaweza wakawa ni wageni au mateka., ambao baadaye wakaja kuwekwa kwenye utumishi wa hekaluni.
Wanethini hawakufanya kazi zozote za kikuhani, ikumbukwe kuwa ilikuwa ni kosa, mtu ambaye sio myahudi tena wa kabila la Lawi kufanya shughuli zozote za kihekalu, Hawa walikuwa wanafanya kazi za usaidizi ule wa nje, kama vile kutweka maji, kukusanya kuni, usafi, na kazi nyingine zilizohitaji msaada wa pembeni.,Ili kuwaruhusu walawi wasilemewe wajikite zaidi katika kazi za hekaluni.
Maandiko yanaonyesha walikuwa na makao yao maalumu palipoitwa Ofeli kule Yerusalemu karibu na hekalu (Nehemia 3:26)
Hata Baadaya ya uhamisho wa Babeli, tunaona mabaki yaliyorudi Israeli kufanya shughuli za kihekalu, hawa wanethini pia walirejea
Kwa ufupi wanethini walikuwa ni la watu (wasio-wayahudi) waliowekwa kwa ajili ya kusaidia shughuli za hekaluni.
Licha ya kwamba Mungu ameliita kanisa lake na amelitenga, limtumikie lenyewe katika shughuli zote za kimadhabahu. Lakini Bado Bwana anaweza kunyanyua watu wengine nje ya kanisa, kusaidia kanisa kusonga mbele. Mfano wa hawa ni Yule akida wa kirumi ambaye alilipenda taifa la Israeli na kulijengea sinagogi (Luka 7:1-5). Hakuwa myahudi lakini aliwasaidia wayahudi.
Hata sasa wanethini wapo wengi, hawapaswi kuzuiliwa, endapo wanasaidia kanisa au kazi ya Mungu, kwasababu ni Bwana ndiye aliyewavuta.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
About the author