Kabla ya Bwana wetu YESU KRISTO, Mkuu wa Uzima, Mfalme mwenye Nguvu, Mwamba Mgumu, na Mkombozi, na Mfalme wa wafalme, kuutoa uhai wake, ili baadaye aurudishe tena (Yohana 10:17), yapo maneno saba (7) aliyasema pale msalabani, ambayo tunayapata katika zote nne (yaani Mathayo, Marko, Luka na Yohana), na maneno hayo ni kama yafuatayo.
1. BABA UWASAMEHE, KWA KUWA HAWAJUI WATENDALO.
Luka 13:34 “Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura”.
Hili ndilo Neno la Kwanza Bwana YESU kulisema akiwa pale msalabani, kuonyesha upendo wa hali ya juu na huruma kwetu, ijapokuwa yeye tayari alishawasamehe, lakini alijua pia umuhimu wa kuwaombea msamaha kwa Baba, kwani si kila msamaha unaoweza kutoa wewe ukawa pia umetolewa na MUNGU, waweza kumsamehe mtu lakini Baba wa mbinguni akawa hajamsamehe huyo mtu bado, hivyo tunajifunza hata sisi kuwaombea wengine msamaha kwa Baba yetu wa mbinguni, kama alivyofanya Bwana wetu YESU KRISTO.
2. AMIN, NAKUAMBIA LEO UTAKUWA PAMOJA NAMI PEPONI.
Luka 13:42 “Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.
43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”.
Hili ni neno la Pili Bwana kuzungumza msalabani, kuonyesha huruma za Bwana YESU hata katika hatua za mwisho kabisa za maisha ya mtu.
3. MAMA TAZAMA MWANAO, NA KISHA AKAMWAMBIA YULE MWANAFUNZI TAZAMA MAMA YAKO.
Yohana 19:26 “Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao.
27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake”.
Hili ni neno la tatu, lenye ujumbe wa kuangaliana sisi kwa sisi, kwani kwa kufanya hivyo tunaitimiza amri ya Kristo la upendo.
4. MUNGU WANGU, MUNGU WANGU MBONA UMENIACHA?
Mathayo 27:46 “Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
Hili ni neno la nne, lenye kuonyesha Uzito wa dhambi Bwana wetu alizozibeba kwaajili yetu, zilikuwa ni nyingi kiasi cha kuuzima uwepo wa MUNGU mbele zake pale msalabani.
5. NAONA KIU.
Yohana 19:28 “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu”.
Hili ni neno la tano, lenye kuonyesha uzito wa mateso ya Bwana YESU kuwa yalikuwa ni makuu.
6. IMEKWISHA
Yohana 19:30 “Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake”.
Hili ni neno la sita, lenye kutangaza mwisho wa utumwa wa dhambi.. na kuanza kwa majira mapya, hakuna tena mateso, wala kilio wala uchungu kwake YESU, na kwa wote watakaokuwa ndani yake.
7. BABA MIKONONI MWAKO NAIWEKA ROHO YANGU.
Luka 23:46 “Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu”.
Hili ni neno la mwisho, kabla ya kukata roho.
Maneno haya yalifunga kauli ya Bwana duniani na baada ya siku tatu, alitoka kaburini, Mauti ilimwachia, na akaja na ushindi MKUU, Wokovu kwetu, Haleluyaa!…
Je bado upo dhambini?.. bado huoni ni gharama gani aliyoiingia YESU kwaajili yako?.. Tubu leo na kumkaribisha maishani mwako kabla ya nyakati mbaya na hatari zinazoikaribia dunia kufika.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kwanini tarehe ya pasaka inabadilika kila mwaka?
PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA?
Nini tofauti kati ya kileo na divai?
Je kibiblia ni sahihi kuadhimisha jumapili ya mitende?
Ipi tofauti kati ya Sheria na kanuni kibiblia.
About the author