Nini tofauti kati ya kileo na divai ?

Nini tofauti kati ya kileo na divai ?

1Samweli 1:5 Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi  sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za Bwana.

Divai na kileo ni vinywaji vya kulewesha, na vyote vilitumika zamani katika Israeli, ambavyo hata sasa vinatumika.

Tofauti kati ya Divai na kileo ni hii;

DIVAI:

Divai, ilichachushwa kutoka katika matunda ya zabibu tu.

Kwa wayahudi divai ilikuwa kama kinywaji cha kitamaduni kilichotumika sana sana katika karamu mbalimbali za kijamii,  tunaona mfano wa sherehe ile aliyoalikwa Bwana Yesu kule Kana,  katikati ya sherehe walitindikiwa Divai, ndipo Yesu akaenda kuyageuza yale maji kuwa divai. Kuonyesha kuwa divai ilikuwa ni kinywaji kilichoruhusiwa kitamaduni Israeli, katika karama. (Yohana 2)

 Lakini pia ilikuwa kama kinywaji cha kiibada, katika karamu za kidini, kwa mfano sikukuku za pasaka, wana wa Israeli walikunywa  divai pamoja na mikate isiyotiwa chachu. Tunaona hilo Kristo alilidhihirisha kipindi kile cha pasaka alipoketi na wanafunzi wake akawapa mkate na divai, kama ishara ya mwili wake na damu yake, imwagikayo kwa ajili ya ondoleo la dhambi za watu wengi. (Mathayo 26.27-29)

Lakini pia divai ilisimama kama kiashiria cha furaha, au baraka.

Zaburi 104: 15 Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung’aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake.

MVINYO:

Mvinyo ulitengenezwa kwa  ngano, shayiri, makomamanga, au tende tofauti na divai iliyozalishwa katika zabibu tu.

Mvinyo ulikuwa na kilevi kikali kuliko divai, na matumizi yako hayakuwa rasmi Israeli, Ilitumika sana sana katika karamu za ulafi na ulevi, lakini sio katika shughuli zozote za kijamii au kidini.

Makuhani hawakuruhusiwa kuinywa walipokuwa wakihudumu katika hema (Walawi 10:9)

Lakini maandiko yanasema nini kuhusu ulevi?

Mithali 20:1 Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.

Katika andiko hilo tunaona Hana, aliposhutumiwa na Eli kuhusu ulevi, yeye akamwambia mimi sikunywa divai wala kileo. Kuonyesha kuwa alitilia umakini ibada yake na sala zake kwa Mungu.

Hata leo, ni vema tufahamu kuwa hatulewi tena kwa mvinyo, bali kwa Roho Mtakatifu tuliyepewa ndani yetu (Waefeso 5:18), Yeye ndiye divai yetu na mvinyo yetu.

Hivyo ni wajibu wa mwamini yoyote kudumu katika Maombi, kutafakari Neno, na ibada, ili ajazwe vema Roho.

Mungu akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Paulo alimwambia Timotheo atumie mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lake, Je! tunaruhusiwa na sisi pia kutumia pombe?

Je! mabalasi Bwana Yesu aliyoyatumia kugeuzia maji kuwa divai, yalitumika tu kwa kazi hiyo?

Kwanini Bwana YESU ageuze maji kuwa Divai? Na ni ujumbe gani tunapata?

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments