SADAKA INAONDOA MADHARA YA MAUTI

SADAKA INAONDOA MADHARA YA MAUTI

Sadaka inayotolewa kwa mwongozo wa Neno la MUNGU ina matokeo makubwa sana kwa anayeitoa. Yapo madhara yanayoondoka kwa maombi tu peke yake, lakini yapo mengine yanahitaji sadaka pamoja na maombi.

Hebu turejee Biblia kidogo tujifunze jambo..

Wakati ambapo Nabii Samweli anataka kwenda kumpaka mafuta Daudi ili awe mfalme mahali pa Sauli..biblia inatuambia kuwa alipofikiri kwenda tu hofu ilimwingia..

Na hofu hiyo ni kwamba alimwogopa Mfalme Sauli, kwani alijua kabisa endapo Sauli akisikia mtu mwingine anaenda kupakwa mafuta ya kifalme kuchukua sehemu yake, wivu utamwingia na atataka kumwua nabii Samweli na yule atakayeenda kupakwa mafuta.

Sasa ili zoezi la Daudi kupakwa mafuta likamilike bila kuleta madhara yoyote kwa Nabii Samweli na Daudi anayeenda kupakwa mafuta ya kifalme, SADAKA ILIHUSIKA!.

Utauliza ilihusika vipi?…turejee maandiko…

1 Samweli 16:1 “BWANA akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.

2 Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi BWANA akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea BWANA dhabihu.

3 Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako”

Je umeiona nafasi ya sadaka katika kuyaokoa maisha ya Samweli na Daudi?.

Hapo MUNGU hakushindwa kumwambia nabii Samweli aende hivyo hivyo na kwamba atamlinda!…La! Hakufanya bali alimwambia aende na dhabihu..

Jambo hilo Bwana MUNGU wetu aliliruhusu pia ili tuelewe umuhimu dhabihu/sadaka.

Unapomtoleo MUNGU kwa ufunuo wa Neno, bila kushurutishwa na mtu wala uchungu, kuna mambo mengi katika ulimwengu wa roho yanafanyika, kama ni nira za mauti zinalegea na kama kuna vifungo vya dhambi pia vinaondoka.

Na kumbuka sadaka kwa BWANA inapelekwa kwa BWANA, maana yake mahali ambapo BWANA anatumikiwa (mfano kanisani au mahali panapofanyika kazi ya MUNGU ikiwemo mikitano ya injili)..hapo ndipo penye neema.

Usipeleke sadaka yako maalumu mahali pengine kama kwa marafiki, au watu au maskini wa barabarani…ni vizuri kufanya hivyo na kuna baraka zake lakini vya Bwana vinapaswa vipelekwe kwa Bwana ndivyo maandiko yanavyofundisha..

Tenga kiasi chako kungine peleka kwa maskini na wenye uhitaji, lakini hakikisha una sadaka yako maalumu kwa BWANA utakayopeleka aidha kanisani au mahali popote kazi ya MUNGU inapofanyika kwa usahihi.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments