USIGEUZE JIWE KUWA MKATE.

USIGEUZE JIWE KUWA MKATE.

Je unaujua uhusiano wa JIWE na MKATE kibiblia?.. Hebu leo tujifunze…

Mathayo 7:8 “ kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.

9 Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, MWANAWE AKIMWOMBA MKATE, ATAMPA JIWE?”

Ni hakika, hakuna mzazi yoyote mwenye akili timamu, ambaye mtoto wake akimwomba MKATE atampa JIWE. Hayupo mzazi wa namna hiyo, wala wanyama hawawezi kufanya mambo ya mfano huo wa watoto wao.

Lakini tunaona wakati fulani shetani alijaribu kumchonganisha Bwana YESU na Baba yake wa mbinguni kwa kumwambia, AGEUZE JIWE LIWE MKATE, kana kwamba Baba wa mbinguni alikuwa amemwekea yale mawe kule jangwani kuwa chakula chake (uvunjifu mkubwa wa heshima)!

Luka 4:2 “akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa.

3 Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, LIAMBIE JIWE HILI LIWE MKATE”.

Hili lilikuwa ni jaribu kubwa la shetani kwa Bwana YESU kutaka kumwingizia roho ya kumwona Baba wa mbinguni kama ni mkatili, ambaye anampa mwanae mawe badala ya mkate kupindi cha njaa, na hivyo adui sasa anamfundisha ayageuze yale mawe kuwa mkate.

Na adui alijua kuwa endapo KRISTO angefanya vile (kwaasababu huo uwezo wa kugeuza jiwe kuwa mkate alikuwa nao) angempokonya uhusiano wake mwema aliokuwa nao na Baba yake, na tangu ule wakati angejua Baba anatoa mawe kwa watoto wake badala ya mkate.

Lakini Kristo kwasababu alikuwa amejaa Roho Mtakatifu aliyajua mafumbo yote ya shetani, hivyo hakudanganyika,  na ndio maana hapo baadae katika Mathayo 7:9 akawaambia wanafunzi wake kuwa Baba mwema hawezi kumpa mtoto wake JIWE badala ya MKATE, sasa kwanini alisema vile?..kwasababu alishakutana na jaribu la namna hiyo hiyo jangwani.

Hali kadhalika unapopitia hali Fulani ya majaribu, usianze kutanga tanga na kuruhusu hofu, na kuona kama kila kitu kilichoko mbele yako hata kisicho na uhai ni fursa kutoka kwa MUNGU, sio kila kitu ni fursa kwako wakati wa majaribu!…vingi ni mitego ya ibilisi kwasababu anajua upo katika hali ya uhitaji wa hali ya juuu….hiyo ndiyo kawaida ya shetani.. alitaka pia kumwaminisha Bwana YESU kuwa yale mawe ni fursa ya kuondoa njaa yake.

Si kila kazi inayokuja mbele yako wakati wa vipindi vigumu ni fursa kutoka kwa MUNGU, kazi nyingine ni za Ibilisi (ni mawe). Mungu hawezi kukupa hayo kama riziki, ziache zipite!.. kazi za Bar ni mawe!, kazi ya Saloni za kiduni ni mawe!, kazi inayohusisha rushwa ni jiwe!, kazi inayohusisha kuuza utu wako ni jiwe!, kazi inayohusisha kuabudu miungu mingine ni jiwe!.. usizigeuze MAWE hayo kuwa MKATE!, hata kama una njaa ya kukaribia kufa!..ziache zipite, si majibu kutoka kwa MUNGU, bali ni majaribu kutoka kwa shetani, kwani huwezi kumwomba Baba wa mbinguni MKATE akakupa JIWE.

Huwezi kumwomba akupe kazi nzuri halafu akakuletea kazi ya kujiuza mwili wako!.. huyo sio MUNGU, bali ni ibilisi…Njaa yako, udhaifu wako, changamoto zako ambazo ni za muda tu!, zisikufanye ukaharibu mahusiano yako na MUNGU moja kwa moja.

Je tayari umeshampokea YESU?.. Kama bado fahamu kuwa tunaishi siku za mwisho, na YESU amekaribia kurudi, na dunia inaenda kuisha, ni heri leo ukayasalimisha maisha yako kwake, ili usamehewe dhambi zako na jina lako liandikwe kwenye kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

HERI YULE ATAKAYEKULA MKATE KATIKA UFALME WA MUNGU.

Je ni kweli Bwana YESU hajui siku ya kuja kwake? (Mathayo 24:36)

IFAHAMU NGUVU YA MAOMBI.

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA MFUNGO.

MANENO SABA YA YESU MSALABANI.

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments