Huyu Imanueli tunayemsoma katika Isaya ni nani?
Swali: Tukisoma kitabu cha Isaya 7:14 tunamsoma Imanueli ambaye kimsingi ni Bwana YESU lakini tukiruka sura moja mbele (ile ya 8:8), tunamsoma Imanueli mwingine, juu huyu naye ni YESU au?
Jibu: Awali turejee mistari hiyo..
Isaya 7:14 “Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli”.
Ni wazi kuwa huyu si mwingine zaidi ya Bwana wetu YESU KRISTO.
Lakini hebu tuendelee na Isaya 8:8..
Isaya 8:8 “naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hata shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee IMANUELI”.
Na hapa tunamwona Imanueli, sasa swali huyu naye ni Bwana YESU?.
Jibu ni la huyu si Bwana YESU.. awali ya yote ni vizuri kujua maana ya Imanueli..
Maana ya Imanueli ni “Mungu pamoja nasi”… hiyo ndio maana ya Imanueli, na ndio maana si ajabu neno hilo kuonekana katika biblia zaidi ya mara moja.
Sasa huyu Imanueli katika Isaya 8:8 ni Taifa la YUDA. Na hapa ametajwa kama Imanueli, kumaanisha uwepo wa Mungu kati ya Taifa hilo.
Ikiisoma habari hiyo kwa undani utaona kuwa ni kipindi ambacho mataifa mawili (Israeli na Shamu), yaliungana kutaka kupigana na Taifa la Ashuru, na kwasababu hiyo mataifa hayo mawili yalitaka kulishurutisha pia Taifa la Yuda liungane nao ili kwa pamoja wakampige Ashuru.
Lakini mfalme wa Yuda aliyeitwa Ahazi ushirika huo, na mataifa hayo mawili yakapanga njama kuvamia Yuda ili yamwue Ahazi na kumweka mfalme mwingine atakayekubaliana na wazo lao hilo la muungano…
Na matokeo yake mfalme Ahazi akataka msaada kwa waashuri, dhidi ya hayo mataifa mawili yaliyoungana..
ndipo Isaya nabii kwa ujumbe wa Bwana akawaambia Ahazi na Yuda yote kuwa wasimtegemee huyo mfalme wa Ashuru katika kutafuta msaada, wala wasiogope hayo mataifa mawili yaliyoungana (yaani Israeli na Yuda) kwani wao ni IMANUELU yaani MUNGU yu pamoja nao.
Kwahiyo yeyote mwenye MUNGU ni Imanueli (iwe mtu au Taifa)..ni Imanueli, wote walio okoka ni Imanueli kwasababu MUNGU yu pamoja nao.
Je upo ndani ya YESU?.
Kumbuka Mungu hawezi kuwa pamoja nawe kama wewe hujafungua mlango wa kuwa pamoja naye
Yohana 15:4 “Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu”
Fungua mlango leo wa kumkaribisha YESU maishani mwako, nawe utamwona MUNGU katika viwango vingine vya kiroho.
Ufunuo 3:20 “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami”.
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
About the author