Haya ndio mambo ambayo baada ya kuokoka, wokovu hufanya juu ya maisha ya mtu
Yohana 3:3
[3]Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
Maana yake ni kwamba pindi tu unapookoka, ni lazima ufahamu si kwamba unarekebisha yale maisha yako ya kale, na kuwa mtu mwema hapana bali unakuwa mtu mwingine kabisa. Kama mtoto mchana aliyekuja duniani, katika mazingira mapya kabisa.
Kwasababu ukristo sio nembo, au kikundi, au mtindo fulani au aina fulani ya dini hapana bali ni ulimwengu mwingine kabisa ambao mtu anaanza kuuishi.
2 Wakorintho 5:17
[17]Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Wakolosai 1:13
[13]Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
Maana yake ni kuwa tunakuwa tayari kutoka chini ya utawala wote wa shetani, yaani kufuatisha mambo Ya kidunia, na anasa, wizi, tunaacha, Kama tulikuwa na vikoba vya kiganga, hirizi, mazindiko Yote hayo tunayaondoa, na kuanza kumtumikia Kristo, mfalme mpya.
Wafilipi 2:12-13
[12]Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
[13]Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.
Maana yake ni lazima Tujue wokovu ni mwendelezo ijapokuwa tunaokolewa pindi tu tunapookoka, lakini hatuupokei tu, na kusema tayari imekwisha hapana bali unapaswa udumu Moyoni mwetu, na kuhakikisha kila siku tunaweka umakini kwa kuuzalia matunda, kwa kufanya bidii kuishi maisha yampendezayo Mungu.
Hivyo kwa ufupi wokovu sio tu, kipawa cha Mungu Kwetu, lakini pia kukubali maisha mapya, mfalme mpya, na njia mpya.
Maana yake ni nini?
Tangu siku hii ya leo wewe uliyookoka hakikisha unayaweka kando mambo yote ya kale ambayo ulikuwa unayafanya yasiyompendeza Mungu, kwasababu hiyo ndio TOBA pekee, kama ulikuwa mzinzi acha mara moja, ulikuwa mlevi, ulikuwa mwizi, ulikuwa mlanguzi acha, kama alivyofanya Zakayo alipokutana na Kristo. Kisha endelea kuishi maisha ya utakaso kila siku, ili Wokovu wako uzidi kuwa thabiti.
Bofya hapa kurudi kwenye mwongozo mkuu wa mafundisho ya mwongofu mpya. >>
Nini kinafuata? bofya hapa. >>>
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
About the author