Kwanini MUNGU aangamize watoto kwenye gharika ya Nuhu?

Kwanini MUNGU aangamize watoto kwenye gharika ya Nuhu?

Swali: Tunajua watoto wachanga hawana dhambi sasa kwanini ile gharika ya Nuhu ilizomba mpaka vichnga?..kwanini Mungu aangamize mpaka watoto wasio na hatia?..napata utata na gharika ile ya Nuhu, na kwenye ile miji ya Sodoma na Gomora je na watoto nao walifanya dhambi ya kustahili kuchomwa na kugharikishwa vile?


Jibu: Ni kweli Biblia inaonyesha ile gharika iliua wote wenye roho ya uhai puani, ikiwemo watoto wachanga na wanyama… na waliosalia ni watu nane tu! Kati ya Dunia iliyokuwa imejaa mabilioni ya watu.

Mwanzo 7:22 “kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu”

Sasa kwanini Mungu aangamize hadi watoto wadogo, na ilihali tunajua kuwa watoto hawana dhambi.

Jibu la swali hili ni kwamba, “mtu anaweza kubeba adhabu ya dhambi ya mwingine lakini asibebe ile dhambi” ili tuelewe vizuri tutafakari huu mfano.. “Mama mjamzito kafanya kosa likamsababishia kifo, ni wazi kuwa na mtoto aliyeko tumboni naye atakufa” kwahiyo adhabu wameshiriki wawili lakini aliyefanya kosa ni mmoja.

Ni hivyo hivyo kipindi cha gharika na kipindi cha Sodoma na Gomora, Watoto walibeba adhabu za wazazi wao ingawa si dhambi!..(wao hawakufanya dhambi yoyote), lakini kutokana na maasi kuwa mengi ikawasababisha nao kushirikishwa katika adhabu hiyo, lakini hiyo haimaanishi kuwa hawataokolewa siku ya mwisho.. huwenda watakaokolewa katika ufufuo wa mwisho kwasababu Mungu ni Mungu wa haki hawezi kumhukumu mtu asiye na kosa.

Lakini kwa wengine (watu wazima) waliosalia ambao ndio waliowasababisha watoto wao kuangamizwa na maovu yao, hao biblia imesema kuwa ipo hukumu nyingine itawapata ya kuhukumiwa kwa mara nyingine na kutupwa katika lile ziwa la moto.

Mathayo 10:15 “Amin, nawaambia, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma na Gomora kustahimili adhabu ya siku ya hukumu, kuliko mji ule”.

Hapo anasema itakuwa rahisi Sodoma na Gomora kustahimili, maana yake ipo adhabu nyingine kwa watu wa Sodoma na Gomora zaidi ya hiyo iliyowapata ya kuteketezwa kwa moto kutoka mbinguni..

Ndio maana Biblia inasema tumwogope yeye awezaye kuuua mwili, na akiisha kuua mwili (kwa moto au maji au kitu kingine) bado anauwezo wa kushughulika na roho tena na kuihukumu katika ziwa la Moto.

Luka 12:5 “Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo”

Watu wa Sodoma na Gomora, pamoja na watu wa gharika ya Nuhu waliuawa katika mwili, lakini bado tena ipo adhabu nyingine inakuja juu yao, jambo linalotisha sana..

Kwahiyo jambo kuu la kujifunza ni kuwa adhabu inaweza kurithiwa au kushirikishwa na mwingine hata pasipo kufanya kosa, na kinyume chake ni kweli Baraka zinaweza kurithiwa hata pasipo mwingine kufanya mema.. Mzazi unaweza kuwa chanzo cha Baraka au matatizo kwa mtoto wako.

Fahamu kuwa Kama utakuwa mwovu kupindukia basi fahamu pia watoto wako hawatakuwa salama kwa uovu wako, ndicho kilichomtokea Mfalme Daudi baada ya kwenda kulala na mke wa Uria, Biblia inasema mtoto aliyezaliwa alikufa, ijapokuwa mtoto hakufanya kosa lolote… lakini alilazimika kubeba adhabu ya baba yake.

Vile vile kuna mambo mema unaweza kuyafanya yakawa akiba njema kwa watoto wako, au watu wanaokuzunguka wakati wa sasa au wa baadaye.. Kwahiyo ni lazima kumcha Mungu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je gharika ya Nuhu iliangamiza hadi samaki wa baharini na nyangumi?.

JE! NI CHEMCHEMI IPI INATOKA NDANI YAKO, YA MITO AU YA KISIMA?

USIPINDUE MAMBO

Je! Adamu na Hawa walizikiwa wapi?

JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments